2018-06-04 14:11:00

Papa akutana na Wanachama wa Kupambana na Ugonjwa wa Misuli Italia


Tarehe 2 Mei 2018, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wajumbe wa Chama cha Umoja wa Italia cha  kupambana na ugonjwa wa misuli (distrophy Muscular), ambapo amewakaribisha kwa furaha na kumshukuru Mwenyekiti wa Muungano wa chama hicho kwa hotuba yake kwa niaba yao na kutoa sifa kubwa ya ukarimu wa shughuli ya chama hicho, watu wa kujitolea katika vituo vyote kwenye kanda mbalimbali  zilizoko katika mikoa ya taifa zima, kwa huduma ya watu ambao wanasumbuliwa na ugonjwa wa misuli  na magonjwa mengine yatokanayo mfumo mzima wa neva za misuli. Baba Mtakatifu amesema kuwa wao wanawakilisha kama mishale ya  mwanga wa jua ya kuletamatumaini katika kuwasaidia kwenye kipindi cha upweke na kukata tamaa, ili wakiwatia moyo waweze kukabiliana na  magonjwa kwa imani na utulivu.

Kadhalika amesema, tendo la kukaa nao karibu, ni kuwahakikishia urafiki na kutoa msaada mkubwa wa huduma kwa mantiki ya udaktari na kijamii. Zaidi ni kutoa msaada wa dhati ili kukabiliana na maisha ya kila siku kama vile usafiri, mazoezi ya viungo, kuwatembelea nyumbani mwao, mambo ambayo ni muhumu wa kuleta joto la kibinadamu, mazungumzo kindugu na huruma ambayo wanaoinesha kwa wagonjwa katika vituo vyao. Mazoezi ya viungo yanaweza, na lazima kusindikizwa hata kiroho hasa ule ukaribu, ili kupambana si tu dhidi ya uchungu wa mwili, lakini pia dhidi ya mateso ya kiroho kwa kuachwa na upweke.

Baba Mtakatifu Fracisko ametaja tabia za kila mtu katika nafasi ya kujitoa bure kwamba: kati ya tabia ya huduma yao ni ile ya kujitoa bure, jambo ambalo linakwenda kinyume na upendeleo wa manufaa binafsi au itikadi za pembeni katika dunia hii. Kujitoa bure lakini inapaswa isindikizwena utaalam na kudumu. Mambo ambayo yanaombwa kwa wanachama wote pamoja na  zaidi pia kuna  fadhila za busara, umakini, utayari na uthati wa kujikita katika dharura , uwezo wa kutambua matatizo yasiyo elezwa na mgonjwa, unyenyekevu, kutilia maanani, uamuzi, kuwahi, uvumilivu na heshima kwa mgonjwa na dharura zake. Kwa maana hiyo anawatia moyo waendelee na njia hiyo , wakiwa daima mashuhuda wa mshikamano na upendo wa Kiinjili. Shughuli yao yenye thamani katoka katika chama chao, katika kuhamasisha na udhati katuka matsnso  dhati, inawafanya jamii iwe makini katika hadhi ya binadamu na matarajio yake yote.

Kwa njia ya shughuli zao, wanaweza kufanya uzoefu iwapo kama wanapenda na kujitoa kwa wengine, ili mwingine aweze kujikamilisha. Yesu Mwana wa Mungu aliyejifanya mtu, anatangaza sababu ya kina ya kufanya uzoefu huo wa kibinadam. Yeye alionesha  sura ya Mungu kuwa ni Upendo (1 Yh 4,8). Yeye anamwonesha binadamu amri kuu ya kuwa ni upendo. Katika maisha yake Yesu alijionesha katika huruma na na kunyenyekea, kwa maana alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa kuwa namna ya mtumwa, na akawa mfano wa wanadamu (Fil 2,7), kwa kushirikishana hadi kifo ambacho ni hatua ya maisha yetu, kwa njia hiyo Yesu anatufundisha kutembea katika upendo.

Upendo unajionesha katika mtindo wa dhati wa ushuhuda wa kiinjili kwasababu ya kutoa jibu la mahitaji ya dhati na kuonesha upendo wa Mungu kwa watu ya kwamba yeye ni upendo  na Baba, vile vile anajidhihirishwa kwa kila mmoja. Kwa kufuata mafundisho hayo, watu wangi wakristo katika karne nyingi wameandika kurasa za kushangaza, kuhusiana na upendo wa jirani. Baba Mtakatifu ametaja baadhi ya watu kama vile watakatifu Giuseppe Cottolengo, Luigi Guanellla na Luigi Orione. Upendo wao umeacha chapa  kubwa katika jamii ya Italia amethibitisha! na hivyo hata kwa nyakati zetu, Baba Mtakatifu ameuliza ni watu wangapi wanajikita kusaidia jirani, hadi kufikia  kugundua imani, kwa maana mgomjwa anakutana na uso wa Kristo Mwana wa Mungu. Yeye anaomba aweze kutumikiwa kwa njia ya ndugu walio wadhaifu. Yesu anazungumza katika moyo wa yule anayejikita kusaidia wagonjwa ili hatimaye waweze kufanya uzoefu wa furaha ya upendo isiyo na kifani, upendo ambao ni kisima cha furaha ya kweli.

Kwa wahusuka wote, vyama na watu wa kujitolea, Baba Mtakatifu amewashuru kwa moyo wote na kuwatia moyo waendelee katika hija hiyo na familia zao, marafiki na wote wanaoishi karibu yao. Wanaweza kuiga mfano wa Bikira Maria aliyekwenda kwa haraka kumsaidia binamu yake Elizabeth, yeye alikuwa mjumbe wa furaha na wokovu (Lk 1,39-45)  kwake yeye anawakabidhi ili wajifunze mtindo wake wa  upendo wa unyenyekevu, upendo ambao Bwana  anajionesha kwa wanaoteseka. Na kwa upande wa wagonjwa waliokuwapo ameonesha ukaribu na kuwabariki wote.

Na Sr Angela Rwezaula 
Vatican News
All the contents on this site are copyrighted ©.