2018-06-04 15:04:00

Kujitoa kikamilifu ni Waraka mpya wa Baraza la Kipapa Walei familia na maisha


Kanisa ni nyumba ya mchezo, kiwanja cha maisha na imani. Kujitoa kikamilifu ndiyo jina na  Mada ya Waraka ulio wakilishwa kwa vyombo vya habari na Baraza la Kipapa, la Walei, Familia na Maisha. Waraka ni mzito wa mafundisho ya Mapapa na Kanisa juu ya Mchezo, wakiweka wazi juhudi za ushindani na shughuli za maisha ya kikristo. Mchezo unaunda mtu, ukiwa na usafi, wa kibindamu na haki. Katika sura 5 zenye kurasa 50 hivi za Waraka, zinatoa kwa ufupi historia ya matukio ya mchezo na kutoa fursa ya kusomwa kwa kina nini maana ya mtu kwa mtazamo wa thamani na changamoto zitokanazo na mchezo. Kati ya changamoto hizo ni pamoja na madawa ya kutia nguvu na rushwa, hadi kufikia nafasi ya Kanisa kuingilia ndani ya sekta hii, inayodhaniwa kama mtindo mpya wa “uwanja wa watu wa Mataifa”.

Jambo msingi ambalo waraka unataka kufafanua zaidi ni kwamba, haupo mchezo wa kikristo, badala yake ni maono ya kikristo katika mchezo.  Kwa njia hiyo wanasema Kanisa, kama ilivyo fundisha mara nyingi katika miaka ya mwisho kwa namna ya pekee wakati wa Mtakatifu Yohane Paulo II, hawasiti kuwatia moyo wa upyaisho wa mazoezi ya mchezo, bali wanataka kuwa ndani ya mchezo na kutambuliwa mchezo wa mtu, kwa maana hiyo ni nafasi ambayo unaweza “kujitoa kikamilifu” na ndiyo mada inazaliwa hadi kuichambua katika urafiki, mazungumzo, usawa, heshima na mshikamano. 
Katika sura ya pili inajikita kueleza juu ya historia ya mchezo kwa kuelezea asili ya neno lake, mfano kuanzia  lugha ya kifaransa itokanayo na lugha ya kilatini, maana ya mchezo  ni furahisha. Mantiki ya burudani mwili, mashindano inasadia katika mchezo tangu mwanzo wa historia ya mtu. Lakini mzizi wa mabadiliko umefikia katika karne mbili za mwisho, wakati mchezo ulianza taratibu kuwa matukio ya wimbi na olimpiadi kusambaa hadi miisho ya dunia na wakati maendeleo ya vyombo vya habari imewezesha mchezo uwe wa kidunia. Katika maendeleo hayo ilikomaa dhamiri ya shughuli za mchezo kama zana ya ushirikishwaji wa mafunzo, ambayo kwa mwili unaunganisha ule wa binadamu na kushindana kama vile matokeo ya kuhamasisha utambulisho wa usawa kati ya binadamu.

Katika swali la kujiuliza nini maana ya mchezo, Waraka unapendekeza moja ya maelezo yanayowezekana, mara baada ya kuona tabia za mchezowakati uliopita. Kwa maana hiyo waraka unasema mchezo ni aina ya shughuli yoyote ya kimwili katika mwendo binafsi au kikundi, ambao wana tabia ya burudani na ushindani   inayo tambulishwa na mfumo wa sheria, lakini ikiwa inawezekana kukabiliwa na hali moja au nyingine sawa zenye fursa. Hiyo lakini siyo mipangilio ya kidharia unathibitisha waraka, kwasababu katika sura ya tatu waraka umetoa umakini juu ya thamani ya shughuli za mchezo zilizofikiriwa kwa namna ya kusema, zinafanana katika kuheshimu zile za imani ambapo moja kati ya zote ni ile yenye umakini wa maendeleo ya pamoja na ushirikishwaji wa mtu, mwili na roho.

Pia Mtakatifu Yohane Paulo II alitoa ushauri wa dhati alipoona katika mchezo, kama mtindo wa mazoezi ya mwili na katika roho, kwamba mchezo siyo nguvu tu za kimwili na ufanisi wa misuli, bali hata roho, na lazima ioneshe uso wake kamilifu! Waraka pia unajikita zaidi juu mwendo sambamba wa mchezo na imani, ambapo kuna na vipengele 9 vya kulezea suala  hilo. Kati ya vile vya kwanza, waraka unasisitiza, ni jinsi gani mchezo unakumbusha uhuru hata uwajibikaji ambao unaleta thamani na kwamba adhabu inahusisha changamoto za muda mrefu kwa kujitolea na sadaka. Na ndiyo kama maisha ya kikristo yanayo wajibisha kuwa na uvumilivu, kwa  kuifanya ifananane zaidi na mbio zenye kuwa na ushindani wa mwendo kasi. Hata hivyo kuna sheria za kushirikisha, matunda ya ubunifu kwa yule aliye fanya mashindano hayona aliyeandaa mashindano kwa maana bila hiyo mashindano yasinge weza kutokea!

Kwa njia hiyo kipengele hicho kinajikita kufafanua kwa kina katika mchezo wa haki, ambao unazaliwa na dharura ya kuhakikisha mchezo unakuwa msafi na kwamba, wachezaji wanafundishwa kuwa makini na kuheshimu wapinzani /maadui wao, zaidi ya kuogopa kuhukumiwa. Yote hayo katika Waraka unathibitisha kwamba mchezo unakuwa na fursa ya mafunzo kwa ajili ya jamii nzima. Kwa namna ya pekee vijana ambao wanaozidi kukosa mwelekeo na kupoteza thamani, wanamichezo wanaweza kupata hata nafasi ya kuwa walimu kwa wengine.

Waraka unaendelea pia kueleza kuwa, mchezo ni kujifunza mengi na uzuri wa mchezo kwa timu, mahali ambapo mchezaji anajiweka kuwa makini akiweka talanta zake katika timu, ambaye  anaweza kutoa jibu la nguvu katika dhana za kisasa zenye ubinafsi. Wakati huohuo adabu ambayo mwana mchezo anapaswa kuwa nayo wakati wa kufanya mazoezi kwa kujitolea na unyenyekevu, akionesha hayo kama yale yanayo jitokeza katika maisha ya imani ambayo sadaka na mateso yana nguvu ya kufanya mageuzi. Bila kusahau kwamba kando ya matatizo ya changamoto ngumu ni kuishi katika mchezo mantiki ya furaha na ile ya umoja, kwa sababu shughuli za mchezo zinapta nafasi ya kuwa mchangiaji wa ustawi wa usawa. 

Waraka unaendelea kuandikwa: uharibifu mkubwa wa mtu unaweza kujitokeza katika kuingiliwa na suala la masoko jambo linalo jihusisha sana na baadhi ya michezo, kutokana na utegemezi wao juu ya mitindo ya kisayansi iliyo enea  na kuleta wasiwasi wa maadili mahali ambapo mwili umegeuka kuwa kitu na mtu amefikiriwa kuwa bidhaa. Katika mantiki ya mchezo, ndipo kuna uwezekano wa kufikia mantiki ya maisha, lakini hiyo inategemea pia na yule anayejikita katika mashindano. Hawali ya yote ni jasiri, hasa anapong’aa akiendelea kujitoa kikamilifu pamoja na kwamba anakuwa katika uwezekano wa kushida au usawa na heshima ya lazima kwa kila aina ya mashindano. Kutokana na hili, Waraka unatamba wanamichezo wengi wamefanya kampeni ya kuhamasisha dhidi ya ubaguzi na kuanzisha kampeni za kushirikishanama, amani,mshikamano  na wale waliobaguliwa. Baba Mtakatifu Benedikto XVI alikuwa amesema: mchezo unaweza kuunganisha katika roho ya urafiki watu na tamaduni. Mchezo ni ishara ya amani na uwezekano.

Pamoja na thamani yake kuu, mchezo pia unaweza kutumika dhidi ya hadhi ya kuwa binadamu na dhidi ya haki za mtu. Katika waraka sura ya nne ni fupi lakini yenye uzito wake katika kukabiliana kile ambacho kinaharibu sekta hiyo. Yote hayo yanatokana ma kutaka kushinda mchezo kwa gharama zozote. Aidha kuanzia na hatari kwa ajili ya afya, wapo wanamichezo waliogeuka kuwa bidhaa tu, kama asemavyo Baba Mtakatifu Francisko, kupitia pia unyanyaswaji kimwili, kijinsi au kihisia zilizofanyiwa wadogo, mahali ambapo inahitajika uangalizi makini na usalama, hadi kufikia tabia isiyo kuwa ya kimichezo kwa washibiki. Kwa maana hiyo waraka unaweka bayana hali halisi hatarishi ya uzuri wa uso wa binadamu na haki ya mchezo. Aidha wanasema inahitaji uwajibikaji ambao unafikia kikomo cha kutambua kwa dhati mahitaji ya heshima kuu ya kazi ya uumbaji, umakini hata wa wanyama ambao wanahusishwa wakati mwingine katika mashindano.

Katika Kanisa Waraka umeonesha sehemu nne za kuingilia kati kwa ajili ya kuzuia kuambukiwa na seketa za mchezo ambazo zimejaribiwa na tabia za matendo nje ya sheria.  Ya kwanza ukosefu wa kukua kwa mwili unajitokeza katika baadhi ya wanamichezo kutoakana na kwamba kuna kesi nyingi za kutaka kufanya mazoezi makubwa kabla kabla ya kufikia umri wao  ambapo husabaisha hatari ya afya. Waraka unataja baadhi ya michezo hiyo ambayo inahitaji vyakula vya aina yake yake, na ambavyo lakini vinaweza kuharibu mwili wa kijana. Na sehemu nyingine ni ile inayo husu utumiaji wa madawa ya kuongeza nguvu mwilini na kuharibu mwili; kwa upande huo waraka unataja wanaohusika hata katika wengine kwa ngazi za kimataifa, vyombo vya habari, fedha na kisiasa. Pia hali hiyo inajihusisha katika rushwa na aina ya uchumi, ambapi waraka unathibitisha ni mama,na  changamoto ya tatu ya kujikita katika kautafua ufanisi wa uzuri wa michezo ule uongo mkubwa na watendaji wa ndani katika sekta hizo kwa kulinda sheria kwa dhati na uwazi.

Mantiki ya nne ni ile inayotazama washabiki na watazamaji… kwa njia hiyo waraka unatoa wito kwa washabiki kujiangaliwa katika jumuiya iliyo ungana ya washabiki ambao wanataka kutoa mchango wao wa upendo na ili sehemu hiyo iweze kuwa kisima cha maajabu, furaha na uzuri.
Sehemu ya tano na ya mwisho, imejikita katika shughuli za Kichungaji za Kanisa kwa ngazi zote za dunia ya mchezo. Uwepo wa Kanisa katika sekta ya mcheza inaendelea kuwa thabiti katika mwazo wa karne ya XX, kwa lengo si tu kutoa muundo wake kwa ajili ya shughuli za uendeshaji, bali hata kama washiriki kikamilifu ili kutoa maana , thamani na matarajio katika mazoezi ya mchezo. 

Kwa maana hiyo vipengele vitano vya sura hiyo ivinafafanua na kufanya utafiti kwa mantiki ambayo shughuli ya kichungaji inaalikwa kufanya. Katika familia ambapo mchezo ni kisima cha mahusiano kati ya baba na watoto, lakini pia inapaswa kushirikishwa katika  misa katika parokia, vituo vya michezo , ambavyo ni thabiti katika mpango wa mafundisho na uchungaji, katika shule na vyuo vikuu ( mchezo unaelekeza maendeleo kamili ya mwanafunzi) katika vituo vya kufanyia mazoezi ya viungo kama vile hata sekta ya kisayansi, madawa na michezo, katika sekta inayojikita kama daraja ya vyombo vya kiutamaduni na kijamii, na mwisho kati ya vyama vya kimichezo na zaidi katika dhana ya wataalam, ambao kwao, waraka unatoa wito wa dharura ya kuwa na mafunzo yanayostahili kwa wachungaji wa michezo. Kutokana na mambo yote hayo kwa namna ya pekee Kanisa linaaliwa kuwasindikiza wataalam wa michezo na kuwatia moyo walioko katika shughuli ya kuweza kuhifadhi roho nyoofu ambayo ina thamani ya bure katikaurafiki, uzuri, na wale ambao wamemaliza muda wao katika mchezo, watambue kuweka talanta zao ili kuondokana na utupu na sikitiko la moyo, ambalo wakati mwingine linaweza kumshambulia mwanamichezo aliye maliza muda wake.

Kwa wote walio mstari wa mbele katika sekta hizi, waraka unajikita kuelezea umuhimu wa mkakati wa elimu ambayo itasaidi walimu wa michezo, wazazi, watu wa kujitolea, mapadre na watawa. Pamoja na hayo Waraka huo unatoa ushauri wa msingi kwa ajili ya mpango ambao unatakiwa katika katika mchezo kwa ajili ya wema wa kichungaji.  Pamoja na hayo yote, mchezo ni kama zana kwa jili ya kujenga mshikamano wa elimu unaoonekana kama huduma ya kibinadamu ambayo inaweka hawali ya yote kiini cha mchezo na ili kwa wote waweze kuwa na maono ya ekolojia. Sehemu ya mwisho ni maneno ya hotuba ya baba Mtakatifu Francisko katika Kituo cha Mchezo Italia 2014: Kujiweka katika mchezo na wengine na Mungu bila kutilia maana juu ya kuwa sawa kwa kadri. Kwa maana hiyo ni kujitoa kikamilifu kwa ajili ya kile kinacho dumu daima! 

Sr Angela Rwezaula
Vatican News
All the contents on this site are copyrighted ©.