2018-06-01 16:04:00

Papa ahimiza upyaisho kiinjili katika matendo ya kimisionari !


Tarehe 1 Juni 2018 Baba Mtakatifu Francisko, amekutana na wakurungezi wa Shughuli za Kipapa za kimisionari mjini Vatican na kuwakaribisha kwa furaha katika tukio lao la Mkutano wa Mkuu na hasa kushukuru hotuba  ya utangulizi ya Kardinali Fernando Filoni, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu, mwenyekiti mpya wa Shughuli za Kipapa za Kimisonari Askofu Mkuu Gianmpiero Dal Toso ambaye kwa mara ya kwanza anaudhria mkutano huo wa mwaka na wote kuwashukuru kwa namna ya pekee katika shughuli zao za kuhamasisha umisionari  kwa watu wa Mungu na kuwahakikishia sala zake.

Baba Mtakatifu pia ameelezea juu ya matajarajio ya hatua ya maandalizi ya Mwezi Maalum wa Kimisionari utakao fanyika  Oktoba 2019, ambao yeye binafsi aliutangaza wakati wa Siku ya Kimisionari Duniani mwaka 2017. Anawatia moyo kwa nguvu zote  ili waweze kuishi hatua hizi za maandalizi kama fursa kubwa ya kupyaisha shughuli za kimisionari kwa Kanisa zima. Pia amesema ni fursa ya Mungu kwa ajili ya kupyaisha shughuli za Kimisionari za Kipapa. 

Ameonesha Baba Mtakatifu jinsi  gani wao wanatambua wasiwasi wake mkubwa alio nao juu ha hatua za shughuli yao, na hasa  ambayo inaweza kugeuka kufikiria mantiki ya fedha za kusadia na zana hadi  kufikia kuwa kama mashirika mengine tofauti, hata  kama yale ambayo yanajiita ya kikristo. Kutokana na hiyo Baba Mtakatifu anawakumbusha kwamba lengo la waanzilishi wa Shughuli za Kipapa na Papa Pio XI  halikuwa hivyo, kwa maana walianzisha kwa ajili ya huduma ya mfuasi wa Petro.  Na ndiyo maana walitoa mapendekezo kama sasa  na dharura  ili kupyaisha kwa utambuzi wa umisionari wa Kanisa zima leo,  kwa utashi mkuu na  kijasiri wa Papa Benedikto XV aliyetoa Waraka wa Maximum Illud kwamba:upo ulazima wa kupyaisha utume Kiinjili katika Kanisa ulimwenguni.

Pamoja na lengo hilo, Baba Mtakatifu anathibitisha kwamba, lazima lisaidie shughuli za Kimisionari kuishi kwa nguvu umoja wa roho na kushirikiana kwa lengo la kusaidia. Iwapo upyaisho utakuwa wa dhati, ubunifu na uthabiti, mageuzi ya Shughuli hizo  utajikitia katika mabadiliko ya kweli na kugeuka kuwa mapya kwa mujibu wa dharura ya Injili. Hiyo lakini haina maana kwa urahisi kufikiria tena, sababu  ili kuweza kutenda  vema  kile ambacho tayari wamefanya. Uongofu wa kimisionari katika miundo ya  Kanisa, (taz Wosia Evangelii gaudium, 27) unataka utakatifu binafi na ubunifu wa kiroho. Si katika kupyaisha vile vya  kizamani, kinyume chake  ni kuruhusu Roho Mtakatifu aunde  na kutengeneza kila kitu kipya ( taz Zab 104,30; Mt 9,17; 2 Pt 3,13; Mdo 21,5). Kwa maana hiyo, Baba Mtakatifu ameshauri kwamba, wasiwe na hofu ya mambo mapya yanayokuja kutoka kwa Bwana Msulibiwa na Mfufuka. Wawe mahodari na jasiri katika utume na wakishirikiana na Roho Mtakatifu daima katika muungano na Kanisa la Kristo Cristo (taz Wosia Furahini na Shangilieni, Gaudete et exsultate, 131).

Je Shughuli za Kipapa zinaweza kuleta maana gani kwao ambapo pamoja na Baraza la Kipapa la Uinjilishi wa watu wanaandaa Mwezi Maalum wa Kimisonari ili kupyaishwa kiinjili?  Akijibu swali hili Baba Mtakatifu anaamini kwa urahisi  kwamba ni uongofu wa kimisionari. Hiyo ni kwasababu kuna haja ya kupyaisha kuanzia katika utume wa Yesu; kupyaisha nguvu zote zilizo kusanywa na kugawanywa katika msaada wa zana kwa mwanga wa utume na mafunzo ambayo yanatakiwa ili dhamiri, utambuzi na uwajibikaji wa kimisionari, uweze kurudi kuwa sehemu ya kuishi kawaida kwa watu wote waamini wa Mungu.
 
Kadhalika Baba Mtakatifu Francisko amefafanua juu ya kauli mbiu  wabatizwa na kutumwa:Kanisa la Kristo katika utume duniani kwamba,  ndiyo kauli mbiu waliyo chagua iongoze Mwezi Maalum wa Kimisionari 2019. Na hiyo ni kutka kusisitiza kwamba, kutumwa kwenda katika utume ni wito unaojikita katika Ubatizo, hata kwa wabatizwa wote. Kwa nana hiyo utumea ni wito kwa ajili ya wokovu ambao ni shughuli ya uongofu wa yule aliyetumwa na yule anayelengwa. Maisha yetu yako ya kweli yako katika Kristo na utume wa dhati! Sisi wenyewe ni utume kwa sababu sisi ni upendo wa Mungu uliotangazwa, sisi ni utakatifu wa Mungu tulio umbwa kwa sura na mfano wake. Kwa maana hiyo utume ni utakatifu wetu na dunia nzima tangu kuumbwa ( taz Ef 1,3-6). Ukuu wa kimisionari katika Ubatizo wetu unajikita katika ushuhuda wa utakatifu ambao utoa maisha na uzuri duniani.

Kupyaisha shughuli za kimisionarai za kipapa maana yake ni kujikita kwa moyo wote katika shughuli nyeti na ujasiri; utakatifu wa kila mmoja; wa Kanisa kama vile wa familia na jumuiya. Kwa maana hiyo  Baba Mtakatifu Francisko ameomba kupyaisha kuanzia katika usafi wa ubinufu wa sili na matendo ya Kimisionari,  na  kujikita katika huduma ya utume ili hatimaye mioyo yenye yene wasiwasi iweze  kuwa na utakatifu wa maisha kama ya  wafuasi wa kimisonari. Na ili kuweza kushirikana katika wokovu wa dunia, lazima kuipenda (taz Yh 3,16) na kuwa tayari kutoa maisha ya  kumtumikia Kristo Mwokozi wa ulimwengu. Hatuna vitu vya kuuza Baba Mtakatifu anabainisha, lakini tunayo maisha ya kutangaza yaani, Mungu, maisha ya Mungu, upendo  wa huruma yake  na utakatifu wake.

Akiendelea na hotuba yake amesema, kama wajuavyo vema kwamba mwezi Oktoba 2019, katika Mwezi maalum wa kimisionari wataadhimishapia  Sinodi ya Maaskofu wa Amazon. Hiyo imetokana kukusanyua wasiwasi wa waamini wengi, walei na wachungaji na ndiyo maana akapendelea kukutana, ili kusali na kutafakari changamoto za uinjilishaji katika ardhi ya Amerika ya Kusini, mahali ambapo Kanisa linaishi kipindi muhimu.  Kutokana na matukio hayo kwenda sambamba, Baba Mtakatifu ameongeza kusema, kipindi hicho kiwasaidie kuwa na mtazamo wao juu ya Yesu Kristo katika kukabiliana na matatizo, changamoto utajiri na umaskini; kiwasaidie katika kupyaisha shughuli za huduma ya Injili kwa ajili ya wokovu wa wanaume na wanawake wanaoishi katika ardhi hiyo. Kadhalika  wamwomb Mungu ili Sinodi ya Amazon iweze kupyaishwa kiinjili katika utume, hata katika kanda zote za dunia ambazo zinajaribiwa, zinanyonywa bila hatia, pia  wenye kuhitaji wokovu wa Yesu!

Mama Maria alipokwenda kwa Elizabeth hakufanya  ishara hiyo kama binafsi, na kama mmisionari. Yeye alikwenda kama mtumishi wa Bwana kwa kupeleka kile alichukwa amebeba tumboni mwake. Hakusema lolote, bali alipeleka Mwanae na kumsifu Mungu. Jambo la haki na  kweli ni kwenda kwa haraka. Yeye natufundisha uaminifu wa uharaka. Hiyo ndiyo tasaufi ya haraka ya umanifu na kuabudu. Hakuwa mstari wa mbele, lakini mtumishi mmojawapo akiwa  mstari wa mbele katika utume,  na ndiyo picha itusaidie, Baba Mtakatifu amemalizia!

Ikumbukwe: Tarehe 30 Novemba 2019 itakuwa ni siku ya kukumbuku ya kutangazwa kwa Barua ya kitume ya (Maximum Illud), mahali ambapo Papa Benedikto wa XV alipendelea kutoa uamsho na uwajibikaji kimisionari katika kutangaza Injili. Ilikuwa mwaka 1919 baada ya kumalizika kwa vita ya Kwanza ya dunia ambayo yeye binafsi alielezea kwamba, ni vita isiyo kuwa na manufaa na kuonesha ulazima wa kuhamasisha Injili katika utume duniani hasa katika kusafisha vidonda na majeraha  yaliyokuwa yamesababishwa na ukoloni katika dunia. Kwa njia hiyo, kwa mujibu wa maombi ya Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu, Baba Mtakatifu anaelekeza Mwezi maalum wa Kimisionari Oktoba 2019 kwamba, lengo lake ni kuwa na utambuzi zaidi wa Misio ad Agentes na kuanza kwa upya mageuzi ya kimisionari katika maisha na maisha ya kichungaji ulimwenguni.

Na Sr Angela Rwezaula

Vatican News!

 

 
All the contents on this site are copyrighted ©.