2018-06-01 16:30:00

Barua ya Papa kwa Kard. Farrell juu ya Waraka wa Kujitoa kikamilifu


Tarehe 1 Juni 2018 katika kumbukumbu ya Mtakatifu Justini, Baba Mtakatifu Francisko ametuma barua kwa Kardinali Kevin Farrell Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Walei, Familia na Maisha kufuatia fursa ya kutolewa kwa Waraka wa “kujitoa kikamalifu”( To Give the Best of Oneself). Baba Mtakatifu Francisko katika barua yake, anafurahi kupata habari za kutangazwa kwa Waraka “kujitoa kikamilifu” katika mantiki ya ukristo kwenye mchezo na maisha ya binadamu, ambapo Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha wameandaa kwa lengo la kuonesha nafasi ya Kanisa katika ulimwengu wa michezo na jinsi gani mchezo unaweza kuwa chombo cha makutano, mafunzo, utume na utakatifu.

Baba Mtakatifu Francisko wamefafanua vipengele muhimu hivyo katika mchezo kama chombo cha makutano, mafunzo, utume na utakatifu kwamba: Mchezo ni sehemu ya kukutana na watu wa kila ngazi, kwa maana hali ya kujamii wanaungana ili kuweza kupata matokeo ya pamoja. Katika utamaduni unao taliwa na ubinafsi na ubaguzi kwa vijana,kizazi endelevu  na wazee, mchezo ni dhana msingi, mahali ambapo watu hukutana  bila kujali rangi, dini na  itaikadi, na mahali ambapo hufanya uzoefu wa  furaha ya kushindana ili kufikia mafanikio ya pamoja, kushirikiana katika timu, katika ushindi au hata kushindwa , lakini kwa kushirikiana ili kupata kushinda;

Hiyo inasaidia kusukuma mbali lengo la kujifikiria binafsi; Umuhimu wa kumtambua mwingine ambaye si tu katika timu ya  mchezo, bali hata wasimamizi, wahusika, wafadhili, familia na wote ambao wanajitahidi kujihusisha kusaidia ili kuweza kufikia kujitoa kikamilifu. Iwapo baba anacheza na mtoto wake,watoto wanacheza pamoja katika uwanja au shuleni, iwapo mchezo unasheherekea ushindi na washabiki wake, katika mazingira yote, inawezekana kutazama thamani ya mchezo kama sehemu ya muungano na makutano kati ya watu na kwa maana hiyo matokeo makubwa, katika mchezo kama vile ilivyo hata  maisha  tunapata umoja katika timu!

Baba Mtakatifu Francisko ameendelea kufafanua zaidi kuwa mchezo ni kama  gari la mafunzo. Kwa kusisitiza amesema, labda leo hii na zaidi mtazamo wetu uelekwezwe kwa vijana katika kipindi ambacho kbala ya kuanza mchakato wa mafunzo kwa maana ni rahisi kupata matokeo  mazuri ya maendeleo endelevu  kamili ya binadamu kwa njia ya mchezo. Inatambulika katika kizazi kipya jinsi gani wanatazama na kupendelea mchezo! Kwa njia hiyo ni lazima ushiriki wa wote katika michezo, kila rika na kwa ngazi zote , ili wale ambao wanashiriki katika dunia ya michezo waweze kuwa mfano wa fadhila kama ile ya ukarimu, unyenyekevu, sadaka, uthabiti na furaha. Kwa namna nyingine mchezo unapaswa utoe mchango mkubwa kwa wale ambao wanashiriki  roho ya timu kuwa na heshima, usafi wa mchezo na mshikamano na wengine. Ni lazima wote tuwe na utambuzi wa umuhimu uliopo katika kushiriki mazoezi ya michezo, kwa maana ndiyo jembe la kulima katika udongo wa rutuba ambayo inasaidia kutoa matunda mema  na daima ni kupalilia na kufanya kazi inayostahili.

Baba Mtakatifu katika bara yake pia anasisitizia juu ya nafasi ya mchezo kama chombo  cha utume na kutakatifuza. Kanisa limeitwa kuwa ishara ya Yesu Krsito duniani na kwa njia ya mchezo na mazoezi katika vituo, maparokia, shule, vyama… Kila fursa ni njema ya kupeleka ujumbe wa Kristo, wakati ukufaao na wakati usiokufaa,  (2 Tm 4,2).  Ni muhimu kupeleka na kutangaza furaha hii itokanayo na mchezo, na ambayo zio zaidi ya kugundua nguvu ya mtu aliyetuita na kuonesha uzuri wa uumbaji kwa binadamu mwenyewe aliye mfano na sura ya Mungu. Mchezo unaweza kufungua njia  ya kuelekea kwakwe Kristo katika maeneo na mazingira ambayo kwa  sababu tofauti , siyo rahisi kutangaza neno mbashala; watu na ushuhuda wao wa furaha katika kufanya mchezo wanaunda jumuiya ambaoi inaweza kuwa wanapashanaji  Habari njema.

Kujitoa kikamilifu  katika mchezo ni wito wa kujikita katika utakatifu. Baba Mtakatifu Francisko akielezea suala hili, ametoa mfano kuwa, wakati wa kukutana na vijana katika maandalizi ya Sinodi ya maaskofu hivi karibuni mjini Vatican, ameweza kukubali kwamba, vijana wote walio kuwapo hapo au kwa njia ya mtandao wa kijamii, walikuwa na  shauku zao na matumaini ya kujitoa kikamilifu. Aidha ameandika kuwa, alitumia maelezo Wosia wa Kitume wa hivi karibuni  akiwakumbusha kwamba, Bwana anao mtindo mmoja na maalum wa kualika katika utakatifu kwa kila mmoja: Kinachotakiwa ni kila mmoja mwaamini kuweza  kung’amua njia yake na kujitoa kikamilifu kadili ya Mungu alivyo muumba (Gaudete et exsultate, 11). 

Kwa namna hiyo inahitaji kujikita kwa kina kuwa na muungano wa mahusiano yaliyopo kati ya mchezo na maisha, ambayo yanaweza kuwaangazia kwa pamoja ili kuweza kupta nguvu ya kujishinda na kuwa na  adabu ya michezo inayosaidia hata kutoa chachu bora daima  binafsi na katika mantiki zote za maisha. Utafiti huo unawezesha kujikita katika njia ambayo kwa msaada wa neema ya Mungu unaweza kufikia katika ukamilifu wa maisha ambayo kila mmoja anaalikwa katika utakatifu. Mchezo ni utajiri wa kisima cha thamani na fadhila ambayo inasaidia kuwa bora kama mtu. Kama mwana michezo wakati wa kufanya mazoezi, yanasaidia kujitoa kikamilifu sisi wenyewe, kujigundua bila hofu ya vizingiti vyetu na kupambana kwa ajili ya  ubora wa kila siku. Kwa namna hiyo “kila mkristo , katika kipimo ambacho najitakatifuza , anatoa matunda duniani, ( Gaudete et Exsultate 33). Baba Mtakatifu ameweka wazi ya kwamba: kwa mwanamichezo mkristo, utakatifu utakuwa ni kuishi mchezo kama chombo cha makutano, mafunzo binafsi, ushuhuda na kutangaza furaha ya kuwa mkristo kwa wale wote wanaomzunguka. 

Amehitimisha katika barua hiyo akiomba Bwana kwa maombezi ya Bikira Maria Mtakatifu, ili Waraka huo wa “kujitoa kkaimalifu”  uweze kutoa matunda mengi na iwe shughuli ya Kanisa kwa ajili ya uchungaji wa mchezo,  hata nje ya Mazingira ya Kanisa. Na kwa wanamichezo wote, wahudumu wa kichungaji ambao wanajitambua kuwa  katika “timu” kubwa ya Bwana Yesu, amewaomba wasali kwa ajili yake na kuwatumia Baraka kwa moyo wote. 

Na Sr Angela Rwezaula
Vatican News
 








All the contents on this site are copyrighted ©.