2018-05-29 16:09:00

Papa ataadhimisha Sikukuu ya Mwili na Damu ya Yesu huko Ostia, Roma


Waamini wa Ostia, Roma wanamsubiri Baba Mtakatifu Francisko kwa shauku kubwa Domenika tarehe 3 Juni 2018 katika fursa ya kuadhimisha Siku Kuu ya Mwili na  Damu ya Yesu. Ni miaka 50 ya kihistoria tangu Mwenye heri Papa Paulo VI alipotembelea katika eneo la Ostiense Roma. Misa ya sikukuu  hiyo itaadhimishwa na Domenika ,saa 12.00 jioni maasa ya Ulaya katika Parokia ya Mtakatifu Monica  na baada ye kufuatia maandamano hadi Kanisa la Mama Yetu wa Bonaria na mwisho baraka ya Ekaristi Takatifu.

Katika siku hiyo Papa kwa mara nyingine atarudi kuadhimisha Sikukuu ya Mwili na Damu ya Yesu katika maeneo  ya Roma, ambayo yako karibu na bahari. Eneo ambao kwa miaka ya hivi karibuni imekumbwa na majaribu ya uhalifu mkuu wa kupangwa, lakini wakati huo bado hawajazimika jamii ya raia na Jumuiya za kikristo Ostia. Kwa namna ya pekee katika Kanisa la Mtakatifu Monica mahali ambapo waamini wote watakusanyika kuadhimisha na Baba Mtakatifu Misa Takatifu!

Paroko wa Mtakatifu Monika Monsinyo Giovanni Falbo amesema ziara ya Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Misa Takatifu katika Kanisa la Ostiense la Regina Pacis 2015 anataka kuonesha ushuhuda wa Papa na ukaribu zaidi na upendo kwa ajili ya Ostia ambaya kwa sasa imekuwa na ishara za kihalifu. Anasisitiza ni ushuhuda hasa kwa matendo hai ya Ostia kwa namna ya pekee katika shughuli za jumuia za kiparokia ambazo zinakabiliana na hali halisi kwa upande wa familia. Jumuiya imeanza kuandaa uwanja wa parokia mahali ambapo aliadhimishwa misa Mtakatifu Yohane Paulo II mnamo tarehe 9 Mei 1983.

Pamoja na hayo pia ni kumbukumbu ya kihistoria ya ziara ya Papa Paulo VI aliyoifanya tarehe  13 Juni 1968. Katika fursa hiyo pia likuwa ni sikukuu ya Mwili na  Damu ya Yesu,ambapo Padre Giovanni alikuwa ni  Padre kijana kwa sasa ana miaka 74, na baada ya kubarikiwa Parokia hiyo akawa Paroko hadi sasa. Kwa upande wa walio wengi wanasema ziara hiyo ni ishara ya dhati ya uwezekano wa kujipyaisha hasa baada ya matukio ya kihalifu ambayo yamejitokeza katika miezi hii ya mwisho.

Ziara hiyo ni kutaka kuwa na utambuzi kwamba wote ni watoto wa Mungu katika kila mtaa na kijamii ,kwa pamoja wanaweza  kuendelea mbele japokuwa na matukio hayo ya kiahalifu ya nyakati hizi za mwisho kwa mujibu wa katekista wa parokia ya Mtakatifu Monica. Hata hivyo katika kukaribisha na kwa heshima ya ziara ya Baba Mtakatifu huko Ostia, watapamba maua mazuri sana katika njia ya kuelekea kwenye soko la Appagliatore karibu na Kanisa la mama Yetu wa Bonaria. Ni kikundi cha utamaduni wa sanaa  kitwacho sarda Quattro Mori cha  Ostia,  kilichotaka kuandaa  maua hayo kwa heshima ya Baba Mtakatifu.


Sr Angela Rwezaula 
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.