2018-05-28 14:13:00

Pumzi ya Kikristo ni furaha itokanayo na tunda la Roho Mtakatifu!


Furaha ni pumzi ya kikristo ni furaha ambayo inatokana na amani ya moyo na siyo unafiki kama vile utolewavyo  na utamaduni wa kisasa, kwa kuunda mambo mengi ya kujifurahisha na anasa, katika mambo yasiyo na idadi utafikiri ni vipande vidogo vidogo vya keki ya maisha lakini ambavyo havitoshelezi hamu ya maisha. Ni tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko aliyoanza nayo Jumatatu tarehe 28 Mei 2018 katika maadhimisho ya Misa Takatifu katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta Mjini Vatican.

Baba Mtakatifu akitafakari somo la  kwanza la Mtakatifu Petro na Injili ya Mtakatifu Marko ambayo inasimulia kisa cha kijana tajiri asiyekubali kuacha mambo yake binafsi, amethibitisha kwamba, mkristo wa kweli hawezi kubaki gizani au kuhuzunika. Kuwa mwanaume na mwanamke wa furaha, maana yake ni kuwa na amani, na ndiyo maana ya mme na mke wa faraja. Baba Mtakatifu ameendelea kueleza: mwamba wa kujiegemeza wa mkristo ni kufanya kumbukumbu, kwa maana huwezi kusahau kile ambacho Bwana ametenda kwa ajili yetu na kufanya maisha mapya;  ndiyo  matumaini ya yule anayetarajia kukutana na Mwana wa Mungu. Kumbukumbu na matumaini ni mambo mawili yanayoruhusu wakristo kuishi na furaha,  lakini si katikafuraha iliyo na utupu, badala yake ni  ni yenye msingi wa amani ndani yake.

Kadhalika anatoa mfano kwamba, furaha siyo kuishi na vicheko kwa vicheko; Furaha siyo jambo la kufurahisha tu, kwa maana ni jambo jingine. Furaha ya mkristo ni amani. Amani ambayo ina mzizi; ni  amani ya moyo ambayo Mungu peke yake anaweza kutoa; hiyo ndiyo furaha ya mkristo na  Siyo rahisi kuhifadhi furaha hiyo binafsi. Katika dunia ya sasa, Baba Mtakatifu anaendelea, kwa bahati mbaya walio wengi wanafurahishwa na utamaduni usio na furaha, utamaduni ambao unaunda mambo mengi ya anasa, idadi ya mambo mengi kama vile  vipende vipande vya keki ya maisha lakini ambayo haitoshelezi kwa dhati haja ya moyo wa mtu. Furaha ya kweli hainunuliwi katika masoko, kwa maana ni zawadi ya Roho Mtakatifu na ambayo inatingisha hata wakati wa dukuduku na wakati wa majaribu.

Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anathibitisha kwamba, kuna wasiwasi mwema, lakini pia kuna jambo ambalo siyo jema lile la kutafuta uhakika kila mahali na kutafuta anasa kila sehemu. Kijana wa Injili alipata dukuduku ya kuacha utajiri wake lakini ambao haumkumpa furaha ya moyo, kwa maana hiyo furaha, na faraja ni pumzi ya kikristo amehitimisha.

Na Sr Angela Rwezaula
Vatican News
All the contents on this site are copyrighted ©.