2018-05-28 16:08:00

Papa amesali Salam Maria wa Mama Yetu wa Afrika kwa tukio la Sr Leonella


Mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana Domenika 27 Mei 2017 Baba Mtakatifu amesali kwa ajili ya amani Afrika. Lakini hiyo imetokana na  kukumbuka kutangazwa kwake Sr. Leonella Sgorbati  kuwa mwenye heri, ambapo ameomba waumini wote waliokuwa wamkusanyika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro kusali salam Maria kwa Mama Yetu wa Afrika  ili Bara liweze kuwa na Amani. Sr Leonella Sgorbati aliuwawa nchini Somalia mnamo mwaka 2006 mjini Mogadishu kwa sababu ya kutetea imani yake. kwa maana hiyo  Baba Mtakatifu amesema, maisha yake yote yalishuhudia Injili na huduma kwa ajili ya maskini, kama vile kifodini, kuwakilisha kiini cha  juhudi ya matumaini ya Afrika na kwa ajili ya amani dunia nzima.

Zaidi ya mapambano dhidi ya ugaidi wa kiislam Kaskazini ya Afrika na  katika nchi ya Nigeria na Mali na nchi mbalimbali zilizoko kwenye migogoro barani Afrika, Baba Mtakatifu ametoa wito wa amani huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jamhuri ya Afrika ya Kati na huko Sudan. Halikadhalika katika fursa ya Siku ya husaidizi wa Wagonjwa, Baba Mtakatifu amewasalimia wote waliounganika katika Hospitali Katoliki ya Policlinico Gemelli, Roma kwa ajili ya kuhamasisha mshikamano wa watu wenye magonjwa mwakubwa. Amewaomba wote wawe na utambuzi zaidi lakini pia   hata yale ya kiroho ya watu wagonjwa na kuwa karibu nao kwa huruma.

Kuhusiana na mwenye heri mpya wa Kanisa, Kardinali Angelo Amato, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza waamini kuwa wenyeheri na watakatifu, Jumamosi, tarehe 26 Mei 2018 kwa niaba ya Baba Mtakatifu Francisko amemtangaza Mtumishi wa Mungu Sr. Leonella Sgorbati kuwa Mwenyeheri. Ibada Takatifu imeadhimishwa huko Piacenza, Kaskazini mwa Italia. Jina la ubatizo alikuwa Rosa Sgorbati aliyezaliwa tarehe 9 Desemba 1940 huko Piacenza na baadaye, akajiunga na Watawa Wamisionari wa Consolata akapewa jina la Leonella.

Naye Kardinali Angelo Amato wakati wa Misa Takatifu amepita maisha ya mtawa huyo, katika maisha ya Mwenyeheri Sr Leonella Sgorbati alikuwa ni mwenye kupenda sana, kupenda wote na kuhurumia daima, ndiyo ilikuwa msimamo wa maisha yake ya kila siku jambo ambalo kwetu sisi inakuwa vigumu, kwa mfano wa kutoa tabasamu, kupokea tabasamu na kumfanya mwingine ahisi furaha ya kweli. Kardinali Amato amesema ni mambo mazuri na madogo ambayo watawa wenzake wanakumbuka katika maisha ya mtumishi aliyependa Mungu Baba, Yesu Kristo wa Ekaristi na Mama Maria.

Alikuwa ni mtawa wa Roho, mwamanamke wa imani hai, iliyo mwongoza katika hatua zake na uchaguzi wake. Mwanamke wa matumaini, daima mwenye furaha, jasiri na heshima. Alikuwa ni mwanamke wa upendo, mwenye uwezo wa kujitoa mwenyewe kwa ajili ya wengine hadi kufikia sadaka yake binafsi; mwanamke wa utii; mwanamke aliyejifunza kutoka kwa Bikira Maria unyenyekevu na kujitoa moja kwa moja katika ukimya. Kardinali Amato, amesisitiza pia, Sr Leonella aliishi kwa ukamilifu katika upendo kwa ajili ya Kristo na moyo wa kitume , mwenye kutafuta Mungu na na mapenzi,mwenye kujisahau binafsi bila kushikilia mambo ya kidunia bali daima kutafuta na kufanya mapenzi ya Mungu.

Akiendelea na mahubiri yake Kardinali Angelo Amato anasema, kuuwawa kwa Sr Leonella , ni kuoneash sumu ambayo inajificha ndani ya moyo wa binadamu.Kuwawa namna hiyo bila kuwa na hatia ni mhuri wa ubaya. Mkristo halisi  siyo mhalifu bali  bali ni mtetezi wa maisha na na anaye wajibika katika upendo  na msamaha. Sr. Leonella alifunikwa na damu takatifu katika ardhi ya Somalia, nchi ambayo alikuwa anaipenda na ambayo kwasasa inahisi upweke na nchini Somalia Kanisa Katoliki linaendelea kuteseka. Kwa maana hiyo mwenye heri  Sr. Leonella Sgorbati ni mmoja wa mlolongo  wa wafadhili walio uwawa kwa ajili ya chuki ya Imani nchini Somalia, kama vile Salvatore Colombo, askofu wa kwanza wa Mogadishu, mmisionari wa kifransiskani Pietro Turati, mmisionari Mlei Annalena Tonelli, na Dakrati Graziella Fumagalli.

Maneno ya mwisho ya Sr Leonella kabla ya kufa ili kuwa ni msamaha, msamaha msamaha, kama vile maneno yaliyotamkwa na Yesu  msalabani kwa wale wote walimsulibisha. Huo ndiyo utambulisho wa shaidi wa kikiristo. Kuwa shiidi ni zawadi inayozaa amani na undugu, ushaidi unaalika kusalimisha kila aina ya silaha na kugeuka kuwa chombo cha amani. Kardinali Amato ameongeza kutoa mfano wa historia ya Mkristo wa kianglikani kutoka uingereza Nigel Baldwin, kwamiezi kadhaa baada ya kifo cha Sr. Leonella. Yeye pamoja na nguvu zake hakuweza kusamehe mtu aliye mfanyia vibaya pamoja na kwamba alikuwa ameshakufa na zamani. Lakini aliposika mauaji ya sr  Leonella siku hiyo, yaliwasha tena mshumaha ndani ya moyo wake na kufikiria maneno ya msamhaa ambayo yaliweza kumsaidia na kutupilia mbali hisia za  uchungu ndani ya moyo wake hadi kusamehe huyo mtu aliye kuwa amemtendea vibaya.Kardinali Amato amemalizia mahubiri yake akisali kwa maombezi ya Mwenye heri mpya Sr  Leonella ili wote wanaweza katika familia na jamii kufungua upya njia za mazungumzo, maopkezi na msamaha.

Wakati huo huo “Leo hii tumeadhimisha uzuri na matunda:matunda na mzizi ya wito wetu wa kikristo”. Haya ndiyo maneno ya Sr Simona Brambilla, Mkuu wa Shirika la wamisinonari wakonsolata  mara baada ya maadhimisho ya misa Takatifu  ya kutangazwa mwenyeheri Sr Leonella Sgorbat ikatika Kanisa Kuu la Piacenza nchini Italia. Sr Simona ameonesha shauku kubwa ya kumshukuru Mungu kwa moyo wote kuwapatia zawadi ya kuadhimisha pamoja  wito wao na kuwa na utambuzi wa ushuhuda hai wa Sr Leonella kama yeye binafsi, maisha yake, mzizi,na kufanya kumbukumbu ya Kristo.
Kadhalika amependa kumshukuru Mama Maria mwenye upole na mtoa faraja ambaye ndiyo msingi wa Shirika lao la kimisionari, kama mama anaye wasindikiza na kuwasaidia kila moja katika safari yao ya utakatifu na ambayo ni mwongozo wa mwanzilishi wao  Mwenye heri Giuseppe Allamano.

Na Sr Angela Rwezaula

Vatican News

 

 

 
All the contents on this site are copyrighted ©.