2018-05-28 15:40:00

Papa amekutana na wawakilishi wa Shirikisho Kimataifa la Madaktari Katoliki


Tarehe 28 Mei 2018, Baba Mtakatifu Francisko, amekutana na Wawakilishi wa Shirikisho la Kimataifa la vyama vya Madaktari Katoliki (FIAMI) mjini Vatican. Akianza na hotuba yake, kwanza amemshukuru Mwenyekiti wa Shirikisho hilo, Daktari John Lee, kwa hotuba yake na taaluma yao kama madaktari katoliki ambao wanajibidisha katika mafunzo ya kudumu ya kiroho, kimaadili na kibayolijia na ili hatimaye waweze kujikita katika matendo hai ya kiinjili, kuanzia  hawali ya yote katika uhusiano wa dakrari na mgonjwa hadi kufikia, shughuli za kimisionari, kwa kuboresha hali halisi  ya afya ya watu wanaoishi pembezoni mwa dunia. Shughuli yao inaundwa na tabia ya mshikamano wa kibinadamu na ushuhuda wa kikristo; kazi yao kwa hakika inatajirishwa na Roho ya imani. Kwa njia hiyo ni muhimu, vyama vyao vikajikita zaidi kuhamasisha misingi hiyo kwa wanafunzi wanaosomea udaktari na vijana ambao ni madkatari kwa kuwahusisha katika shughuli za vyama vyao.
 
Baba Mtakatifu anaendelea kusistiza, utambulisho katoliki kwamba hautoa ahadi ya ushirikiano katika mantiki tofauti na  dini, au  imani maalum. Wao wanatambua hadhi na utu wa binadamu kwa dhana ya shughuli zake. Kanisa ni kwa ajili ya maisha na kuwa na wasiwasi wake  juu ya kile kinachopinga maisha katika hali halisi, katika udhaifu au ukosefu wa utetezi au kwamba hakuna njia ya kufanya. Kuwa daktari katoliki maana yake  kujihusiaha kutoa  ya  afya ambayo ina amani na muungano na Kanisa, kwa kupokea ile chachu kuhudumia na kukomaa katika mafunzo ya kikristo, taaluma na kujikita bila kuchoka ili kupenya na kutambua sheria za asili kwa ajili ya kuhudumia maisha ( Taz Waraka wa  Human Vitae, 24 wa  Papa Paulo  VI ) 

Ndiyo uaminifu na udhati ambao kama vyama vya Shirikisko lao kwa miaka kadhaa wameweza kuwa na imani  na uhalisia wa ukatoliki na kuendeleza mafundishao ya kanisa kwa kuongozwa na nyaraka mbalimbali katika kambi za madaktai kimaadili. Mantiki hiyo ya utambuzi na matendo hayo Baba Mtakatifu anaongeza kusema kuwa, yamesaidia shughuli yao ya kushirikiana katika utume wa Kanisa kuhamasisha na kutetea maisha ya binadamu tangu kutungwa kwake hadi mwisho wake wa asili, ikiwa pamoja na kuhudumia , kuheshimu wadhaifu zaidi na ubinadamu katika maisha na ukamilifu katika jamii nzima.

Baba Mtakatifu Francisko akitazama hali halisi ya sasa, amewaalika kuwa na msimamo katika kiini  mgonjwa kama mtu na hadhi yake, pamoja na haki ikiwa ndiyo jambo la kwanza la haki ya maisha. Ni lazima kupinga tabia ambayo inafikiria binadamu mgonjwa kama chombo cha kukarabati, bila kuheshimu kwanza msingi ya kimaadili, kunyanyasa walio wadhaifu na kuwabagua wengine  kutokana na kwamba wanakataa baadhi ya itikadi ambazo hazifai au zenye kutaka kujinufaisha. Kutetea mtu aliye mgonjwa ni shughuli muhimu kwa ubinadamu katika sekta ya madawa kwa maana hata hiyo ni ekolojia ya binadamu!  Kwa maana hiyo Shirikisho la Madaktari Katoliki wanaalikwa kujikita kwa dhati katika shuguli yao katika nchi mahali, hata kwa ngazi ya kimataifa, huduma katika mazingira ya kitaalam, hata majadiliano hayo ya kutazama sheria juu ya maadili nyeti kwa mfano wa utoaji wa mimba, mwisho wa maisha  na madawa.

Baba Mtakatifu anawasihi wawe mstari wa mbele katika kulinda na kutetea huru wa dhamiri, madaktari na kila mhudumu wa afya. Haikubaliki kwamba nafasi yao kupunguzwa kwa kile kinachoitwa utashi wa mgonjwa au mahitaji ya mfumo wa afya mahali wanapofanya kazi. Aidha Baba Mtakatifu amesema katika Mkutano wao utakao fanyika huko Zagabria siku chache zijazo wanatafakari mada kuhusu Utakatifu wa maisha na taaluma ya daktari, kutoka Waraka wa “Maisha ya binadamu” (Humanae Viatae), hadi “Sifa kwa Bwana” (Laudato Si). Kwa maana hiyo anathibitisha kwamba, kutokana na mada hiyo ni ishara ya ushiriki wa dhati katika maisha na utume wa Kanisa. Katika ushiriki huo ni kama inavyosisitiza Mtaguso wa Vatican II kwamba: ni lazima kwani bila kufanya hivyo hata shughuli za kitume za Mchungaji haziweia kufikia ukamilifu wake (Decr. Apostolicam actuositatem, 10). Baba Mtakatifu  amewahimiza wawe daima na utambuzi kuwa, leo hii ni lazima na dharura ya matendo hai ya Daktari katoliki ambaye yupo na mwenye tabia inayoonekana wazi kushuhudia binafsi na hata kama mwanachama!

Amewaomba katika shughuli zao za chama cha madkatari katoliki waweze kushirikiana vema na hali halisi za Kanisa kwa namna ya pekee katika juhudi za pamoja na mapadre, watawa na pia wahudumu wa kichungaji katika afya na ili kwa pamoja  wawe karibu na yule anayeteseka: wawe na uhusiano mkubwa na mahitaji ya wale wanahusika. Wawe watumishi zaidi ya kutibu, wakiongozwa na upendo kindugu na kuonesha ule ukaribu wa kweli katika mahusiano yao ya dhamiri na utajiri wa kibindamu ambao unaongozwa na  huruma ya kiinjili.

Amehitimisha kwa kuhimiza tena juu ya kazi yao na kwamba, maneno, ishara ushauri, uchaguzi wao ambao una mwangwi katika uchungu kwenye kambi yao ya kitaalam, iwe kwa dhati ushuhuda wa imani ya kuishi. Anawatia moyo waendelee katika shughuli yao kwa furaha na ukarimu kama hatua madhubuti ya chama na kushirikiana na watu wote,na taasisi nyingine kwa upendo katika maisha na kuhdumia watu ili wakimbilie katika utakatifu. Mama Maria kimbilio la  Wagonjwa awasaidie na kuwasindikiza!

 Na Sr gela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.