2018-05-28 15:52:00

Katika Utatu Mtakatifu tusifu Fumbo la Mungu, Yesu na Roho Mtakatifu!


“Sikukuu ya Utatu Mtakatifu, inafanya kutafakari kwa kina fumbo la Mungu anaye umba, anaye hurumia na kutakatifuza daima kwa upendo, kwa ajili ya upendo;  na kila kiumbe anayempokea, anampatia mwanga wa uzuri,  wa wema na ukweli. Sikukuu hii ni kutafakari kwa dhati na kusifu fumbo la Mungu na Yesu katika umoja wa nafsi tatu, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Ni katika kuadhimisha mshangao ambao daima ni upendo wa Mungu  ana utoa katika  maisha bure na kuhimiza atangazwe duniani kote”. Ndiyo utangulizi wa tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko aliyoanza nayo Domenika tarehe 27 Mei 2018, kabla ya  Sala ya Malaika wa Bwana, Mama Kanisa akiadhimisha Siku kuu ya Utatu Mtakatifu, mara baada ya Domenika ya Petenkoste ambapo katika tafakari yake ameongozwa na masomo yote ya siku yanayo onesha upendo wa Mungu kwa ajili yetu na nini mapenzi yake kwetu sisi !

Baba Mtakatifu akiendelea na tafakari yake kwa kina katika  maneno ya  Mtakatifu Paulo mtume wa watu kuhusu uwepo wa matendo hai ya Roho Mtakatifu, amesisitiza juu ya upendo wa Mungu alio nao kwetu sisi, kwani  amesema, Mtakati Paulo, binafsi alifanya uzoefu wa mabadiliko aliyotendewa na Mungu upendo na ambao unajieleza zaidi  katika shauku ya kumwita Baba, hata hivyo Baba Mtakatifu anaongeza kusema, kumwita Baba kwa maana  Mungu ni Baba Yetu, kwa uaminifu mkubwa kama vile  mtoto anayejikabidhi moja kwa moja katika mikono ya yule aliye mpatia maisha. Mtakatifu Paulo anakumbusha kwamba, Roho Mtakatifu akiwa ndani mwetu, siyo rahisi Yesu kupunguzwa nafsi yake kama mtu aliyepitwa na wakati, bali tunahisi uwepo wake karibu, kwa nyakati zetu na kufanya uzoefu wa furaha ya kuwa wana wapendwa wa Mungu.

Baba Mtakatifu Francisko aidha amehitimisha akikisisitiza juu ya utume wa kila mkristo na maana ya sikukuu ya Utatu Mtakatifu. Amesema, shukrani kwa uwepo na nguvu za Roho, wote tunaweza kutimiza utume ambao yeye mwenyewe anatupatia. Lakini ni utume gani?  ni kutangaza na kushuhudia kwa wote Injli yake na kupanua muungano na yeye, kuwa na furaha ya kweli itokanayo na kukutana naye! Kwa njia hiyo, Sikukuu ya Utatu Mtakatifu inafanya kutafakari kwa dhati fumbo la Mungu ambaye daima anaumba, anahurumia na kutakatifuza na upendo kwa ajili ya upendo na kwa kila kiumbe anaye mpokea, anampatia mwanga wa uzuri, wa wema na ukweli wake!

Na Sr Angela Rwezaula
Vatican News!
All the contents on this site are copyrighted ©.