2018-05-26 14:37:00

Mkakati wa Kimataifa wa afya ya wanawake,watoto na vijana 2016-2030!


Askofu Mkuu Ivan Jurkovick mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika ofisi za Umoja wa Mataifa zilizoko mjini Geneva, tarehe 25 Mei 2018 ametoa hotuba yake katika kikao cha 71 kuhusu mada ya ajenda, kipengele 12.3, kinachohusu mkakati wa kimataifa kwa afya ya wanawake, watoto na vijana waliopevuka. Ni Mkakati kwa Afya ya wanawake, watoto na vijana waliopevuka ambao ulianzishwa mwaka 2016-2030. Lakini uzinduzi wa mkakati wa kimataifa kwa afya ya wanawake, watoto na vijana waliopevuka ulizinduliwa mnamo 26 Septemba 2015 jijini New York, Marekani wakiwa kando ya  mkutano wa kupitishwa kwa malengo ya maendeleo endelevu, (SDGs) na aliyekuwa katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki-moon na  ambaye alitangaza ahadi ya dola Bilioni 25  ziweze kutumika kwa kipindi cha miaka mitano katika kuboresha afya ya wanawake, watoto na vijana waliopevuka.

Kwa maana hiyo katika hotuba yake, Askofu Mkuu Ivan anathibitisha kukubaliana na Ripoti ya Mkurugenzi Mkuu ambayo inajihusisha na nguvu kazi  katika dunia kwa ufanisi wa afya; kuongeza mantiki msingi kuhusiana na suala la afya kwa wanawake,watoto na vijana wanaopevuka; kukubaliana na  mambo kadhaa ya kushirikishana na malengo msingi ya Shirika la Afya Dunia (WHO), kama vile kuhamasisha huduma ya afya ulimwanguni, mapambano dhidi vurugu na manyanyaso dhidi ya wanawake na watoto; sehemu kubwa ya mpango wa afya kuanzia utoto hadi kufikia umri wa miaka 18. Lakini pamoja na hayo yote, Askofu Mkuu Ivan anasema bado kuna wasiwa wasi wa kile kinachoitwa ubaguzi, kwa sababu ya kile kinachoitwa utoaji mimba wa uhakika katika mantiki za mkakati wa kimataifa.

Kutokana na hiyo katika hotuba yake Asofu Mkuu amesema, Vatican inatoa msimamo wake mkali wa kupinga kila aina ya nguvu yoyote ya Umoja wa Mataifa au Mashirika yoyote maalum ambayo yako tayari kuhamasisha sheria inayoiwezesha nchi kuua maisha kabla ya kuzaliwa kwa maana hiyo utoaji mimba. Anathibitisha hayo na kuhitimisha akitoa tafakari ya maswali:,inawezekanaje kuwapo  chombo cha kulinda haki za binadamu, wanawake na watoto wakati  huo huo inakataa watoto kuzaliwa au kukataliwa haki msingi ambayo ni  maisha? ikumbukwe, Baba Mtakatifu,anasititiza :"ipo  haki ya maisha ambayo ni matakatifu yasiyokiukwa na kuwekewa masharti ya hali yoyote"

Hata hivyo katika kujikita kwa mantiki hiyo ya  kutazama thamani kuu ya uhai wa maisha  na hasa wa watoto,  tunaweza kufanya tafakari zaidi juu ya  nani mwenye madaraka na hasa anayetufanya tuisha maisha haya na kutoa kweli thamanai hiyo. Kwa dhati, fundisho la utetezi na kulinda watoto, tunaupata kutoka kwa  Yesu Mwenyewe, anapofundisha katika Injili ya Mtakatifu Marko 10,13-16 , “Basi wakamletea watoto wadogo ili awaguse; wanafunzi wake wakawakemea.  Ila Yesu alipoona alichukizwa sana, akawaambia, Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao.  Amin, nawaambieni, Ye yote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hautaingia kabisa; Akawakumbatia, akaweka mikono yake juu yao, akawabariki”.

Je hii inatokana na nini? Ni ktuzama ni jinsi gani tangu enzi za zamani, watoto hawakufikiriwa kitu kabisa, hawakuwa na sauti, , na ndiyo maana tunaona mitume wanawakaripia bila aibu watoto hao na tunaweza kuthibitisha kuwa, waliokuwa kama kivuli cha kukanyagwa miguuni pa  wazazi au watu wazima kwa ujumla. Kwa upande wa waafrika, ndiyo tabia ambayo kwa  baadhi ya makabila na nchi inaendelea hata leo hii, hata katika mambo msingi kwa upande wa chakula, mavazi, na mambo kadhaa …. Baba anaweza kupata nyama nyingi mtoto akapewa mfupa… Wazazi kama baba anaweza kuvaa suti mama kanga nzuri na mavazi mazuri, lakini watoto wanatembea peku, au na nguo zilizochanika au mbaya sana.

Na mambo kadhaa ambayo siyo rahisi kuyataja yote, japokuwa kwa njia ya Injili na utetezi wa watoto ni wazi  kuonesha umuhimu wa kuhimiza umakini kwa ajili ya watoto kizazi hadi kizazi. Lakini, tufikirie ni watoto wangapi wanateswa, wananyanyaswa na kuwawa. Wangapi wanasahauliwa na wengine hawewezi kuzaliwa,utoaji mimba umekuwa jambo la kawaida kama vile  kwenda haja?  Ukitazama katika watoto yatima ambao hawana hatia kuzaliwa katika ulimwengu huu, lakini unakuta wanateswa na wale ambao wamekubali majukumu ya kuwatunza? Maneno ya Yesu yanafanya moyo wetu udunde kwa makosa makosa mengi tunayotenda dhidi ya watoto wetu, yatima na hata wale ambao tunakutana nao njiani lakini hatujali, au kuwatumia kama bidhaa. Lakini Yesu leo hii anamtukuza, katika hali ya binadamu kamili, na kuthibitisha kwamba,anayempekea mtoto, anapokea ufalme wa Mungu. Anaonesha hata sisi namna ya kuwapokea kwa maana anawachukua, anawabariki na kuwakumbatia. Ndiyo mafundisho ya Yesu katika matendo ya kweli, ili nasi tuweze kuyatenda kwa watoto wetu, hata wote tunaokutana nao njiani tunapokuwa, maana watoto ni baraka ya maisha yetu! 

Watoto ni ishara ya mshangao, huruma, usafi, upole, uzuri, utukutu mzuri, ni watoto ambao wanahitaji  Baba na mama anayewaamini na kuwapa neno lake. Yesu anafundisha kufanya hivyo hivyo na  mwenye masikio  asikie hayo kwamba, hasiye mpokea mdogo, yaani kumlinda, kumtetea, kumpenda na kumpatia haki zake kama inavyotakiwa ina maana hataweza kamwe kuingia na kuwa na mahusiani au kutambua nini maana ya maisha ya Mungu katika ufalme wake. Ufalme wa Mungu unaanzia hapa duaniani, maana yeye ametuumba hapa duniani kwa ajili ya kwamba  umjue, umpende, umtumikie na mwisho wake ili uweze kuungana naye huko duniani,lakini ili kuungana nayo lazima upitie katika matendo ya dhati na siyo ya kinadharia. Kwa njia hiyo wote tunaalikwa kuhisi kama watoto ambao wamemszunguka Yesu, ili kumsikiliza. 

Anatusaidia Mtakatifu Mama Teresa wa Calcutta ambaye katika maisha yake kama mtawa alitambua nini maana ya maisha haya. Mama Teresa anatueleza kwamba:“ kuishi maana yake ni kupenda na kupendwa. Na ndiyo maana wote tunao wajibu wa kupambana ili pasiwepo kamwe hali ile ya kukataa na kudharau maisha kwa manaa kila mtoto ni ishara ya upendo wa Mungu, ambaye anapaswa kutangazwa katika dunia hii. Iwapo mnatambua mwanamke yoyote ambaye hataki kuwa na mtoto aliye naye tumboni mwake na akiwa na nia ya kutaka kutoa mimba hiyo, mtafuteni na kumsihi abaki na mtoto huyo baada ya kujifungua aniletee mimi, kwa maana nitampenda kwa sababu ni ishara ya upendo wa Mungu”. Kwa maana hiyo ni wazi kwamba tendo la utoaji wa mimba ni kosa na uhalifu mkubwa maana ni kuua maisha ya upendo wa Mungu!

Sr Angela Rwezaula  
Vatican News
All the contents on this site are copyrighted ©.