2018-05-25 13:23:00

Cuamm:Siku ya Afrika, kufanya kazi na... kwa ajili ya maendeleo endelevu!


Tarehe 25 Mei ya kila mwaka ni siku ya Afrika Dunia, ambapo maadhimisho hayo kwa mwaka 2018 yanaongozwa na kauli mbiu,“ kufanya kazi “na” kwa ajili ya wakati endelevu ulio bora” kwa mujibu wa madaktari na Afrika Cuamm! Kwa kutazama siku hiyo ushuhuda wa kambi za kufanyia kazi za madaktari na Afrika (Cuamm) unajieleza zaidi kutokana na uzoefu wa miaka mingi ambayo imewawezesha kusaidia watu wengi wanaoteseka katika sekta ya Afya barani Afrika. 

Kutokana na fursa ya siku hiyo, madaktari na Afrika(Cuamm) wanathibitisha kuwa, tarehe 25 Mei ni Siku ya Afrika ambayo inataka kuadhimisha hatua madhubuti ya Afrika katika kuelekea uhuru kamili,hasa ule  uwajibikaji wa watu wake, waweze kuona upeo wa wakati endelevu na ulio bora! Kwa mtazamo wa upeo huo,Madaktari na Afrika, (Cuamm) wanataka kwa kina, kutoa umakini juu ya mahitaji ya bara zima, lakini pia hata  kusisitiza kwamba, ili kuweza kutazama upeo wa  maendeleo endelevu, inatakiwa kuwashirikisha watu na  jumuiya mahalia, ili waweze kuwa mstari wa mbele katika ubunifu, mipango, mbinu za maendeleo ya kweli katika maisha yao ya kila siku!

Na hiyo ndiyo  hatua ya mstari wa mbele ambayo Madaktari na Afrika (Cuamm) wamekuwa wakijikita kila siku kufanya kazi katika kambi za afya karibia  watu 1660, sehemu kubwa ya wahudumu wa wafya wakiwa ni  asili ya kiafrika.  Katika nchi saba wanazo shughulikia, wapo madaktari 260 kutoka Ulaya, kati yao 250 ni kutoka Italia, wakifanya kazi pamoja na wahudumu 1400, asili ya Afrika, ambamo kati yao ni madaktari, wauguzi,viongozi tawala na mipango!

Kwa ushuhuda zaidi, yupo Steven Ngoma, daktari wa Cuamm, mzaliwa wa nchi ya  Demokrasia ya Congo na  ambaye ametoka  Ulaya na kurudi Afrika na familia yake ili kufanya kazi katika nchi ya Sierra Leone, akiwa karibu na watu wenye kuhitaji. Daktari  Ngoma ambaye kwa sasa yuko  Kisiwani  Bonthe, anashuhudia umuhimu wa kufanya kazi barani Afrika, hasa mara baada ya kufanya uzoefu wake kama daktari Ulaya na muuguzi Afrika katika nchi yake.
Yeye ni mzaliwa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, lakini wakati anafanya kazi katika hospitali ya Serikali kama muuguzi alikutana na na muuguzi mwenzake, Celine kutoka nchi ya Uswiss na  ambaye sasa ni mke wake kwasababu walifunga ndoa mwaka 2016.

Mara baada  ya ndoa walihamia Ulaya, lakini si kwa ajili ya kukaa  bali kujiendeleza na masomo ya juu zaidi. Kwa hakika wamepata shahada katika utaalamu wa magonjwa ya kitoripiki, wakati huo  Celina mkewe Steven, amefapata master ya magonjwa kwa ujumla. Lengo lao tangu mwanzo lilikuwa ni lile la kurudi Afrika, wakiwa  tayari na utaalam mkubwa ili waweze kukabiliana na changamoto ya hali halisi Barani Afrika, mahali amabpo wanathibitisha kuwa wanalipenda sana.

Akiendelea na ushuhuda wake amesema kuwa, wakati wa masomo yao, kwa bahati nzuri wakakutana na kufahamiana na madkatari na Afrika  Cuamm na ndiyo maana kwa sasa wameishia  huko Bonthe katika kisiwa kimoja  Kaskazini ya nchi ya Sierra Leone.  Ushuhuda wake, Daktari Steven anaongeza kusema, wako kule kwasababu wote  pamoja wanaamini pia kuwa na  uwezekano wa kuchangia kuleta mabadiliko. Kuna kazi nyingi za kufanya anasema, lakini jambo la kwanza ni kutazama mahitaji na wagonjwa wao, pia wanajiuliza je ingekuwaje iwapo pasingekuwapo msaada kutoka nje hasa katika masuala ya matukio ya upasuaji ?

Na hili kuweza kufanya hivyo, anathibitisha, kwa dhati inahitaji kuwa na moyo na ukarimu na kwa  kila mmoja kukunja mikono yake ili  kuweza kusaidia na  hasa kama waafrika, ni lazima kuachilia mbali tabiana mitindo ya kujiona au  kujitosheleza wakati huna uwezo wowote, badala yake ni liele suala la kupenda mabadiliko ambayo kwa pamoja inawezekana. Katika ufafanuzi wa mipango na miradi itokayo nje ili kuwafikia watu, anathibitisha kuwa, mipango haitoshi na mbinu kuletwa kutoka nje, badala yake, ni kuwahusisha wenyeji mahalia kupanga pamoja naili kuweza kuendeleza mipango kwa ajili ya wakati endelevu, kwasababu, katika uzoefu wake, wakati anafanya kazi hospitali ya Serikali huko Congo aliona kwa macho yake, mipango mingi kuharibika bila  kuleta mafanikio yoyote. Kwa njia hiyo: kuwashirikisha wanajumuiya mahalia, ndiyo ufunguo wa mafanikio ya maisha endelevu!

Kwa kuhitimisha ametoa mfano kwamba, katika jumuiya yao, walianzisha mipango ya pamoja ya kuwashirikisha wahudumu 900 wa afya, na mpango huo kwa sasa unaendelea vizuri kwa sababu watu wamekuwa  na mahusiano mema kati ya vituo vya afya na vijiji ambavyo vinahamasishwa na wahudumu hao wakizunguka ili kuhakikisha mahitaji na afya za watu. Huo ndiyo mfumo wa afya unavyokua  namna hiyo ukiwa na msingi thabiti wa kushirikishana na jumuiya nzima mahalia!

Na Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!
All the contents on this site are copyrighted ©.