2018-05-24 16:03:00

Balozi Julio Anibal Rianò awasilisha hati za utambulisho kwa Papa!


Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi, tarehe 24 Mei 2018 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Bwana Julio Aníbal RIAÑO VELANDIA, Balozi wa Colombia mjini Vatican. Alizaliwa kunako tarehe 3 Marchi 1949. Ameoa na kubahatika kupata watoto wawili. Ana shahada ya uzamivu katika Sheria za Kimataif na Diplomasia aliyoipata kutoka Chuo Kikuu Jorge Tado Lozano, kilichoko mjini Bogotà.

Katika maisha na utume wake, amewahi kuwa: Mhariri; Mhadhini na Mkurugenzi wa Kitengo cha Tafiti; Mfanyakazi katika Wizara ya Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa; Waziri na Mshauri wa Ubalozi wa Colombia nchini Argentina. Amewahi kuwa Mkurugenzi mtendaji wa masuala ya Colombia: Asia, Afrika na Oceania kwenye Wizara ya Mambo ya Nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa. Kati ya mwaka 1999 – 2006 aliteuliwa kuwa ni Balozi wa Colombia nchini Costa Rica; Mwaka 2006-2011 Mkurugenzi mtendaji wa Protokali, Wizara ya Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Mwaka 2011 hadi mwaka 203 aliteuliwa kuwa Balozi Mexico na Mwaka 2013 aliteuliwa kuwa Balozi wa Colombia nchini Salvador.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.