2018-05-20 10:35:00

Telegram ya Papa Francisko kutokana na ajali ya ndege chini Cuba!


Tarehe 19 Mei 2018 Baba Mtakatifu anaonesha  masikitiko makubwa  na uchungu katika ujumbe wa  salama za rambi rambi kwa njia ya Telegram kutokana na ajali ya ndegu iiliyo anguka huko Avan nchini Cuba tarehe 18 Mei 2018 na kusabisha vifo vya watu wengi. Katika Telegram aliyo mwelekeza Askofu Mkuu Dionisio Guillermo García Ibáñez, wa Jimbo Kuu la Santiago ya Cuba, Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Cuba, Baba Mtakatifu anawahakikishia maombi yake kwa Mungu kwa marehemu wote ili wapumzike kwa amani pia kuwaombea faraja ya roho , ndugu jamaa na marafiki wanao omboleza kwa ajili ya wapendwa wao kipindi hiki cha huzuni na uchungu.

Ujumbe wa Telegram uliotiwa sahini na Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican unamalizika ukiwatakia ndugu wa waathirika wote wawe na utulivu wa kiroho katika matumaini ya kikristo. Sababu ya ajali ya ndege, Boeing 737 ya Damojh Aerolineas, Low Cost ya Mexco yenye kuwa na  kituo chake Guadalajara na ambayo ilikuwa inaelekea huko Holguin, bado haijafahamika kwa mujibu wa Kampuni wa Shirika la ndege la Quba ya Aviaciòn.  Pia kwa mujibu wa habari za taifa hilo, waathirika ni 107, kati yao walio nusurika ni wanawake watatu tu. Rais wa Cuba Bwana Miguel Díaz-Canel amesema kuwa, wamefungua tume ya uchunguzi ili kuweza kugundua  sababu ya ajali hiyo.  Na kwa maana hiyo Serikali imetangaza msiba wa Kitaifa kwa siku mbili. Hii ni ajali kubwa iliyo wahi kutokea nchini Cuba kwa miaka mingi!

Sr Angela Rwezaula
Vatican News!

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.