2018-05-20 15:00:00

Sikukuu ya Pentekoste inahitimisha Kipindi cha Pasaka, kifo na ufufuko!Siku ya leo ni Sikukuu ya Pentekoste ambayo inahitimisha kipindi cha Pasaka, kipindi kilichokuwa kinajikitia kutafakari juu ya Kifo na ufufuko wa Yesu. Sikukuu hii inakumbisha na kuishi uvuvio wa Roho Mtakatifu juu ya Mitume na wengine walio kuwa wameunganika katika sala na Bikira Maria katika Ukumbi Mkuu (taz Mdo 2,1-11). Siku hiyo ndiyo ilianza historia ya Takatifu kikristo kwasababu Roho Mtakatifu ambaye ndiye  kisima cha utakatifu na ambaye si kwa ajili ya wachache tu bali ni wito kwa wote.

Ni utangulizi wa  Tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko, Jumapili 20 Mei 2018 wakati wa kusali sala ya malkia wa Mbingu,  mama Kanisa akiadhimisha Sikukuu ya Pentekoste. Katika tafakari yake kwa mahujaji na waamini wote walio kusanyika katika Kiwanja cha Mtakatifu Petro, Baba Mtakatifu amesema, katika ubatizo kwa hakika wote tunaalikwa kushiriki maisha yenyewe ya Mungu katika Kristo, katika Kipaimara tunageuka kuwa mashuhuda wake katika dunia. Roho Mtakatifu ananyunyizia utakatifu kila mahali kwa watu waamini watakatifu wa Mungu (Wosia wa Gaudete et exsultate, 6).

Kama Mtaguso wa Pili wa Vatican usemavyo, Mungu anapenda kutakatifuza watu wote kwa kila nafsi na kufanya mahusiano  kati yao na kuwaunganisha  watu hao kwa mujibu wa ukweli na kuhudumia katika utakatifu (taza Lumen gentium, 9). Baba Mtakatifu amesema, hata hivyo katika Agano la kale manabii wa Bwna walikuwa wametoa unabii: “Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.  Nanyi mtakaa katika nchi ile niliyowapa baba zenu, nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu” (Ez 36,27-28). Pia “kila atajaye  jina la Bwana ataokoka” (Joeli 3,1-2.5). Unabii wote huo unatimilizwa kwa njia ya Yesu Kristo ambaye ni daraja na uhakika kwa vuvio wa Roho.

Tangu wakati wa Pentekoste hadi nyakati za mwisho utakatifu na ukamilifu ni Kristo ambaye anajionesha kwa wote ambao wanajifungulia matendo hai ya Roho Mtakatifu na kujibisha kuwa wakarimu. Mantiki msingi ya utakatifu ni ile ya kuwa tunda la takatifu la Roho. Roho Mtakatifu anapoingia ndani ya maisha, anashinda ukavu na kufungulia mioyo matumaini na kuweka chachu, hasa katika kukuza ukomavu wa ndani na mahusiano na Mungu na jirani!

Kwa mujibu wa Mtakatifu Paulo anaonesha matunda ya roho Mtakatifu kuwa ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, (Gal 5,22). Kwa njia hiyo tuombe Mama Bikira Maria tuweze kupokea zawadi hizo na hata upyaisho wa Kanisa kwa njia ya Pentekoste ili kulijalia zawadi ya furaha ya kuishi na kushuhudia Injili n, kuitangaza kwa shauku ya kuwa watakatifu kwa njia ya  utukufu wa Mungu (Gaudete et exsultate, 177).

Na Sr Angela Rwezaula 
Vatican News
All the contents on this site are copyrighted ©.