2018-05-20 12:59:00

Papa ametangaza Makardinali wapya kusimikwa tarehe 29 Juni 2018!


Mara baada ya sala ya malkia wa mbingu Baba Mtakatifu ametoa tangazo kuwa tarehe 29 Juni atawasimika rasmi makardinali wapya14. Baba Mtakatifu anathibitisha kuwa, uwepo wao unawakilisha Kanisa la Mungu duniani, ambalo linaendelea kutangaza upendo wa huruma ya Mungu kwa watu wote katika Ardhi hii. Miongoni mwa makardinali wapo kutoka  Roma  na zaidi ili kuoinesha uhusiano uliopo kati ya Vatican na  Kiti cha Petro na Kanisa Mahalia duniani kote. 

Baba Mtakatifu ametaja makardinali wapya kuwa ni Patriaki Louis Raphaël I Sako wa  Babilonia ya Wakaldei; Askofu Mkuu Luis Ladaria, Rais wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa; Askofu Mkuu Angelo De Donatis, Makamu Askofu Jimbo kuu la Roma; Askofu Mkuu Giovanni Angelo Becciu,  Katibu msaidizi wa Vatican na mahusiano ya nje na Mwakilishi Maalumu wa Kikosi cha Kijeshi cha Malta; Askofu Mkuu Konrad Krajewski  Msimamizi wa Sadaka za Kitume Vatican; Askofu Mkuu  Joseph Coutts  wa Jimbo Kuu la Karachi.

Akofu António dos Santos Marto wa Jimbo la Leiria-Fátima Ureno; Askofu Mkuu Pedro Barreto  wa Jimbo Kuu la Huancayo; Askofu Mkuu Desiré Tsarahazana wa Jimbo Kuu la Toamasina Madagascar; Askofu Mkuu  Giuseppe Petrocchi  wa Jimbo Kuu la  Aquila Italia; Askofu Mkuu  Thomas Aquinas Manyo wa Jimbo Kuu la Osaka. 


Pamoja na maaskofu wakuu, pia maaskofu wa mashirika ambao  wanamajukumu ya kutoa huduma tofauti katika Kanisa; Askofu Mkuu mstaafu Sergio Obeso Rivera wa Jimbo Kuu la  Xalapa. Askofu Mkuu Mstaafu Toribio Ticona Porco wa  Corocoro na mwisho Padre R.P. Aquilino Bocos Merino  wa Shirika la Waclareti. Baba Mtakatifu anaomba kuwaombea sala hawa makardinali wateule ili waweze kujikita kwa kina katika nyayo za  Kristo wakiongozwa na ukuu wa huruma na imani (taz  Eb 2,17), na ili pia waweze kumsaidia katika utume wake kama Askofu wa Roma kwa ajili ya wema wa watu watakatifu, waaminifu wa Mungu!

Sr Angela Rwezaula 
Vaticsn News!








All the contents on this site are copyrighted ©.