2018-05-18 16:09:00

Kupenda,kuchunga na kujiandaa kubeba msalaba ndiyo dira ya mfuasi wa Yesu!


Kupenda, kuchunga na kujiandaa katika msalaba, zaidi ili kutoangukia katika vishawishi hasa vya kuweka pua katika maisha ya wengine. Ndiyo ushauri wa Baba Mtakatifu alio wapatia wakati wa mahubiri yake tarehe 18 Mei 2018 katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatacan, akitafakari Injili ya siku ya Mtakatifu Yohane inayoeleza mazungumzo ya mwisho kati ya Bwana Yesu na Mtakatifu Petro. Katika mahubiri ametafsiri mtindo wa dhati, ambao mitume wanapaswa kuwa nao katika kumfuasa Yesu.

Kutokana na maelezo ya hatua ya kwanza ya Mazungumzo, ambayo Yesu anamuuliza Simoni Mwana wa Yohane kama anampenda, ndiyo inathibitisha na kuonesha jinsi gani  Yesu anabadili jina na kurudi kumkumbusha kipindi cha udhaifu wake hawa wakati wa wimbo wa jogoo!  Na huo ni mchakato wa kiakili ambao Bwana anautaka kwa kila mmoja ili kuweza kufanya kumbu kumbu ya hatua zilizo kwisha tendeka na yeye anabainisha Baba Mtakatifu! 

Katika hatua hiyo, Baba Mtakatifu anajaribu kutoa ufafanuzi katika sehemu tatu kama ulivyojitokeza katika mazungumzo ya Bwana na Petro: “nipende, chunga na jiandae”. Hawali yayote upendo ni mpango madhubuti wa kuweza kukufanya kuwa mfuasi wa Mwana wa Mungu na baadaye kuchunga maanaye ni kulinda na ndiyo utambulisho wa kichungaji unao jionesha wazi  katika kuchunga na kama   utambulisho wa askofu na padre kuwa mchungaji.
Nipende, chunga na jiendae: Nipende maana yake, nipende zaidi ya wangine, nipende kila  uwezavyo, lakini nipende tu. Baba Mtakatifuanasema, hiyo ndiyo hali ambayo Bwana anawataka wachungaji, hata waamini wote kuwa nayo kwa maana upendo ndiyo hatua ya kwanza ya mazungumzo na Bwana. Akitoa mfano amesema, ni wangapi ambao wanamkumbatia Bwana wakati wanaelekea katika kifodini; wanabeba  msalaba na kupelekwa mahali ambapo walikuwa hawataki au kutegemea. Lakini hiyo ndiyo dira ambayo inaelekeza hatua za kila  mchungaji.

Jiandae katika majaribu: jiandae kuacha kila kitu kwa maana yanakuja mambo mengine na kufanya tofauti kabisa na kile ulichokitarajia; jiandae na tenguo la maisha; Utapelekwa katika njia za unyenyekevu, labda katika barabara ya mashahidi. Siyo hajabu na wanao kupeleka ni wale ambao,  wakati ulikuwa mchungaji walikusifu na kuzungumza  vema juu yako, lakini leo hii wanakugeuka na siyo wema tena kwako. Jiandae kwa ajili ya msalaba na upelekwa mahali ambapo hutaki. Nipende, chunga na jiandae ndiyo karatasi ya mwongozo wa  kichungaji yenye kuchanika!

Katika sehemu ya mwisho wa mazungumzo, Baba Mtakatifu anasisitiza zaidi kuonesha vishawaishi vilivyosambaa leo hii, hasa shauku ya kuweka pua katika maisha ya wangine, bila kufurahia mambo y binafsi, badala yake kutazama ya wengine. Kwa maana hiyo ameshauri kujitazama binafsi, badala ya kwenda kuingiza pua katika maisha ya watu wengine. Hiyo ni kutokana na kwamba mchungaji anapenda, anachunga na kujiandalia msalaba, kujivua utu wake binafsi, lakini siyo kutia pua  katika maisha ya wengine, kwa kupoteza wakati katika msululu wa mambo yasiyo na maana, badala yake ni  kupenda, kuchunga na kujiandaa ili kuweza kuepuka kuangukia katika vishawishi!

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.