2018-05-16 15:29:00

Papa kwa mara nyingine aomba amani katika nchi Takatifu na Mashariki !


Mara baada ya Katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko, mawazo yake yamerudi katika nchi Takatifu na za Mashariki. Kwa namnaya pekee huko Gaza mahali ambapo damu inaendelea kumwagika baada ya maandamano ya wapalestina  kufuatia pia uzinduzi wa Ubalozi wa Marekani mjini Yerusalemu. Ambapo inadaiwa kuwa waathiriki 61 Jumatatu na kati yao mtoto wa miezi nane na wengine wawili wapelestina waliwawa na vikosi vya ulinzi na usalama nchini Israeli.

Baba Mtakatifu Francisko ameonesha masikitiko na wasiwasi mkubwa  wa mivutano hiyo ambayo, amesisitiza kuwa, inafukuzia mbali njia ya amani, michakato ya mazungumzo. Kadhalika uchungu mkubwa wa vifo vya watu wengi na majeruhi na kuonesha ukaribu wake kwa sala na upendo kwa wote wale wanao teseka katika hali hiyo. 
Amerudia kusema kwamba, kamwe vurugu haziwezi kuleta amani. Vita vinaalika vita, vurugu zinaalika vurugu, kwa maana hiyo anawaalika sehemu zote mbili na Jumuiya ya kimataifa kurudia kwa upya wajibu wao ili mazungumzo, haki na amani vipate kutawala. Wakati huo, amesali sala ya Bikira Maria wa amani, kwa kuwalika  waamini wote kuungana katika sala na kumwomba Mungu huruma yake. 

Mwisho amekumbusha ulimwengu wa kiislam kwa kuwatakia  matashi mema ya kuanza mwezi Mtukufu wa Ramadhan ambao ni muhimu katika dini ya kiislam duniani kote, unaoanza 17 Mei 2018. Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa, kipindi hiki, kiwe ni cha sala na kufunga na kuwasaidia watembee katika njia ya Mungu ambayo ndiyo njia ya amani.


Sr Angela Rwezaula

Vatican News!
All the contents on this site are copyrighted ©.