2018-05-14 15:33:00

Urafiki wa kuishi na Yesu ndiyo hatma yetu na ndiyo wito wetu!


Tumepokea kwa namna moja hatma  ambayo ni kama mwelekeo wa mwisho na siyo kwa bahati mbaya.Kuwa na urafiki na Yesu ni  wito wetu yaani  hatma ya kubaki ndani ya urafiki na Bwana daima. Ndiyo kiini cha tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 14 Mei 2018, wakati wa mahubiri yake kwenye Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican, Mama Kanisa akiwa anaadhimisha sikukuu ya Makatifu Matia, mmoja wa mitume 12 aliyechaguliwa kuchukua  nafasi ya mtume Yuda baada ya kumsaliti Yesu.

Tumepokea  zawadi ya hatma  kama kweli  mwelekeo thabiti wa mwisho wa kuwa marafiki wa Bwana na huo ndiyo kweli wito wetu. Urafiki huo wa Bwana, ndiyo walio upokea mitume wake kwa nguvu zaidi lakini hata sisi leo hii, tumepokea  sawa sawa kama mwelekeo wa zawadi ya urafiki wake usio kuwa na  kikomo. Na hatma yetu ya kuwa marafiki wake ndiyo zawadi kuu ambayo Bwana anazidi kuitunza kwa ajili yetu daima maana yeye ni mwaminifu wa tunu hiyo msingi.

Lakini mara nyingi, Baba Mtakatifu ameongeza kusema,  sisi siyo waaminifu kwa maana tunakwenda mbali kwa sababu ya  dhambi na utukutu wetu,  pamoja na hayo Bwana anabaki daima mwaminifu kwa  urafiki wake. Na ndiyo maana Yesu anakumbusha katika Injili ya Siku kuwa “siwaiti tena watumwa bali marafiki (Yh 15,9-17), ndiyo maana ya kwamba anazidi kudumisha  neno hilo hadi mwisho maana ni mwaminifu.  Hata mbele ya janga la  Yuda kabla ya kumsaliti, alimwita  “rafiki yangu” na hakumfukuza kwa nguvu aondoke zake. Yesu ni rafiki, na Yuda kama Injili inavyofafanua   alikuwenda zake katika hatma ya mwelekeo  mpya, yaani mwisho wake aliouchagua binafsi na kwa uhuru wake na kwenda mbali na Yesu. Kukufuru ni njia ya kwenda mbali na Yesu, kwa maana, rafiki anageuka kuwa  adui au rafiki anageuka kuwa tofauti au rafiki anageuka kuwa msaliti!

Katika nafasi ya Yuda, kama somo la Matendo ya Mitume (Mdo 1,15-17.20-26) wanavyoeleza, kura ilimwangukia Mattia, ili aweze kuwa shuhuda wa Ufufuko, shuhuda wa zawadi hiyo ya upendo. Baba Mtakatifu anakumbusha kuwa, rafiki ni yule ambaye anashirikisha siri zake binafsi kwa mwingine. Kwa maana Yesu katika Injili anathibitisha:“ nimewaita marafiki, kwasababu kile nilicho sikia kwa Baba yangu nimewafanya hata ninyi kutambua ”. Hii ina maana ya kwamba urafiki ambao tulio upokea hawali ndiyo kama hatma ya mwelekeo wa mwisho, kama walivyo upokea Yuda na Mattia.

Baba Mtakatifu amehitimisha mahubiri yake, kwa kuwaalika waamini wafikirie jinsi gani Yesu hakanushi zawadi hiyo na anatusubiri hadi mwisho. Sisi tunapokuwa wadhaifu na kwenda mbali Yeye , anasubiri tu , na kuendelea kusema, rafiki yangu ninakusubiri, rafiki yangu unafanya nini? rafiki yangu kwa nini unanipa busu la usaliti? Yeye ni mwaminifu katika urafiki na sisi lazima kuomba neema ya kubaki katika upendo na urafiki, yaani urafiki tulio upokea kama zawadi ya hatma yetu.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.