2018-05-10 15:13:00

Mkutano wa XIV wa Sinodi ya Maaskofu waikubali Hati ya kutendea kazi!


Tarehe 7 na 8 Mei , umefanyika mkutano wa nne mjini Vatican wa Baraza la XIV la Sekretarieti Kuu ya Sinodi ya Maakofu, iliyo ongozwa na Baba Mtakatifu Francisko. Na katika mkutano huo,Instrumentum Laboris yaani, Hati ya kutendea kazi, ya Sinodi ya Maaskofu kuhusu vijana imekubaliwa!  Shughuli ya Mkutano huo ilianza na hotuba ya Kardinali Lorenzo Baldisseri, Katibu  Mkuu wa Sinodi ya Maakofu, na wakati wa kutoa salam zake, amemshukuru Baba  Mtakatifu Francisko uwepo wake na kuendelea kuelezea hatua za mchakato mzima unaotazamiwa kufanyika katika Sinodi ya XV ijayo mwezi Oktoba mwaka huu.

Kwa namna ya pekee Katibu Mkuu amesimama zaidi kujikita katika mandalizi ya Instrumentum Laboris  yaani , Hati ya kutendea kazi, ya Sinodi ya Maaskofu, iliyofanyiwa kazi na kikundi cha wataalam ambao walikusanya zana mbalimbali msingi kutoka katika vyanzo vikuu vitano ambavyo amevitaja ya kuwa ni:maswali ya mwisho wakati wa maandalizi kwa upande wa wajumbe wakuu wa matukio yote; majibu ya maswali kutoka kwa vijana yaliyokusanywa kutoka katika mtandao wa kijamii; Hati ya mwisho ya Semina ya Kimataifa kuhusu hali ya vijana iliyofanyika mwezi Septemba 2017; maoni tofauti huru kutoka kwa kila kikundi; na hatimaye hati ya mwisho ya Mkutano kabla ya Sinodi ya maaskofu uliofanyika kuanzia tarehe 19-24 Machi 2018.

Katika tukio hilo la mwisho wa mkutano uliofanyika machi 2018, Kardinali Baldisseri ameonesha kwa shauku kubwa kuhusu ushiriki wa vijana kutoka pande zote za dunia na ambao walikuwa ni wawakilishi wa mantiki tofauti za Kanisa na zisizo za Kanisa! Baada ya hotuba hiyo, Kardinali Baldisseri, amewakilisha mpango wa Instrumentum Laboris yaani, Hati ya kutendea kazi, ambayo ndiyo ilikuwa mada msingi ya mkutano huo. Hati hiyo imetoa mwamko mkuu na kuwapa mawazo mengi ya kubadishana maoni, kiasi cha  kutoa ushauri na maoni juu yake  kulingana na jinsi hati  ilivyo kuwa na ambayo itawawezesha mababa wa sinodi kuwa kweli zana ya kitendea kazi katika majadiliano; kwa njia hiyo Hati hiyo ya kitendea kazi imekubaliwa rasimi na washiriki wote.

Aidha Wajumbe wote wa Baraza la kawaida la Maskofu walikabiliana hata  baadhi ya mantiki na dhana mbalimbali za maandalizi ya Sinodi ya Maaskofu ijayo kutokana na kuwakilishwa na Hotuba ya  Monsinyo  Fabio Fabene Katibu Mkuu Msaidizi wa Sinodi ya Maaskofu, na baadaye  ilifuatiwa mjadala juu yake na kubadilisha maoni msingi. Mwisho wa  mkutano huo, Baba Mtakatifu aliwashukuru wajumbe wa Baraza na washiriki wote  kwa mchango wao na roho ya umoja  kindugu ambao uliongoza mkutano huo!

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!

 








All the contents on this site are copyrighted ©.