2018-05-04 16:42:00

Askofu ni mchungaji mwema anayekaa karibu na watu wake na kukesha!


Kutunza imani na kusimama kidete katika imani pamoja na kukesha kwa mchungaji ndiyo mada muhimu ambayo Baba Mtakatifu amerudia kujikita wakati wa mahubiri yake kwenye Misa Takatifu katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta mjini Vatican tarehe 4 Mei 2018. Tafakari imeanzia katika somo la kwanza la matendo ya mitume ambapo inaelezea kipindi kigumu ndani ya jumuiya ya kikristo  ya Antiokia pia Injili ya siku juu.

Baba Mtakatifu anendelea na ufafanuzi, kutoka katika somo la Matendo ya mitume, “Kwakuwa tumesikia ya kwamba watu waliotoka kwenu wamewasumbua kwa maneno yao wakipotosha roho zenu, ambao sisi hatukuwaagiza”: Haya ni maandishi ua Petro na mitume wakiwaandikia wakristo kwa maamuzi pamoja na Roho Mtakatifu kutenda hivyo ili kuleta amani. Huko Antiokia walikuwa wametumwa Barnaba na Paulo na wengine waaminifu wakiwa na  barua hiyo. Na baada ya kuisoma, watu walifurahi kutiwa moyo, kama inavyoeleza. Na hiyo imetokana na kwamba; wale waliokuwa wamejionesha kulinda watu kama walinzi na watetezi wa kweli wa mafundisho,walikuwa wajifanya ndiyo wanataalimungu wa kikristo, lakini waliwapotosha watu,lakini  mitume, maskofu wa leo wanawaimarisha katika imani.

Baba Mtakatifu anaendelea kusisitiza, askofu leo hii ndiyo anayelinda na kukesha kama mlinzi ambaye anatunza na kutetea zizi lake dhidi ya mbwa mwitu wanaokuja kulishambuliwa. Maisha ya Askofu yanajihusisha na maisha ya zizi. Pamoja na hayo askofu pia anafanya jambo kuu zaidi, kwa maana ni kama mchungaji anaye kesha. Ili kuelezea wito wa askofu kwa neno zuri, Askofu anakesha daima na kutoa maisha yake yote katika zizi. Yesu mwenyewe waliweza kutoa maana ya kweli ya kuwa mchungaji, kumtofautisha na yule aliye ajiliwa, kwasababu ya kutojihusisha zaidi na zizi inapotekea hatari ya mbwa mwitu. Mchungaji mwema ni yule anayekesha na kujihusisha na maisha ya zizi lake, anatetea, si kondoo peke yake walioko katika zizi  bali kila mmoja na hata yule anayepotea, anarudi kumtafuta ili hasiache hata mmoja apotee.

Askofu wa kweli anajua kila jina la kondoo na ndiyo maana Yesu anathibitisha na kumfananisha Askofu kuwa ni karibu. Roho Mtakatifu aliwapatia wakristo uwezo wa kujua mahali ambapo yupo askofu wa kweli. Akifafanua hili anasema, ni mara ngapi tumesikia wanasema kuwa, askofu yule ni mwema lakini hajali watu wake, mara nyingi ana mambo mengi ya kufanya, au mara nyingi analalaimika, au askofu yule anafanya mambo ambayo hayafanani na wito wake, au askofu huyo mara nyingi yupo na sanduku mkononi akizunguka kila mahali, au askofu huyo mara nyingi ni kuwa gitaa mkononi, na kila mmoja anaweza kufikiria, Baba Mtakatifu anathibitisha. Lakini ki ukweli watu wa Mungu watambua mchungaji mwema hasa yule anayekaribia watu wake, mchungaji mwema anayetambua kukesha na kutoa maisha yake kwa ajili yao kwa maana ya ukaribu!

Na ndiyo inapaswa kuwa maisha ya askofu, pia ndiyo kifo chake. Baba Mtakafifu ametaja mfano wa Mtakatifu Turiniode de Mogrovejo, aliyekufa katika kijiji kimoja cha watu wa asili akiwa amezungukwa na wakristo wake, wakipiga chombo kimoja cha muziki ili aweze kufa kwa amani. Amemaliza akiomba Bwana ili atupatie wachungaji wema na wasikose kulinda Kanisa na kuwa wachungaji wao kesha, ili tuweze kuendele mbele nao. Wawe ni watu wafanyakazi, wa sala wa ukatibu na watu wa Mungu kwa neno moja wawe ni watu wanao jua kukesha!

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!
All the contents on this site are copyrighted ©.