2018-05-03 16:09:00

Shauku ya kimisionari ya Balozi mpya wa Kitume nchini Korea na Mongolia


 “Ninataka kujua Kanisa la Korea na Mongolia haraka iwezekanavyo ili niweze kulipenda na kulitumikia. Nimekuwa daima na mshangao na shauku ya wamisionari wote kike na kiume, hivyo ni matumaini yangu ya kuweza kuwa kama wao kwa kupeleka mbele matendo ya uinjilishaji; kwa kutangaza neno la Yesu na kupokea wakristo wapya wa Kanisa”. Ndiyo maneno ya Balozi wa Kitume wa Papa nchini Korea  na Mongolia Askofu Mkuu Alfred Xuereb, yaliyotangazwa na Gazeti Katoliki la AsiaNews, wiki chache kabla ya kuwasili kwake Barani Asia mwezi Mei 2018 katika utume wake kama Balozi mpya  nchini Korea na Mongolia.
 
Katika Gazeti Katoliki la AsiaNews limemkariri akisema kuwa, anataka kuendeleza zile nyayo za watangulizi wake na kufanya za  kwake  ndogo za ujenzi wa madaraja. Balozi Mpya wa kitume nchini Korea na Mongolia, alikuwa tayari amesha shika madaraka ya   ukatibu Mkuu wa Uchumi na Katibu maalumu wa Papa Mstaafu Benedikito XVI ambapo Papa Francisko, manmo tarehe 26 Februari 2018 alikuwa amemtangaza kushika  nafasi Jimboni  Amantea Kisiwani Malta, akiwa na hadhi ya Uaskofu Mkuu.
 
Askofu Mkuu Alfred Xuereb,mwenye umri wa miaka 59 kutoka Kisiwa cha Malta anasema kuwa, kipindi hiki ni muhimu kwasababu ya maadalizi ya kuhama kuelekea nchi ya Cora ya Kusini. Nafasi ya kuteuliwa kwake na Baba Mtakafifu kweli ni ya uwajibikaji mkubwa na hivyo anamshukuru sana kwa matumaini na hadhi hiyo aliyomkabidhi. Aidha amemshukuru Askofu Mkuu Hyginus Kim Hee-joong, Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu  nchini Corea (Cbck), akiwa Roma katika shughuli za Kichungaji hivi karibuni amepata hata fursa ya kumtembelea. Na wakati wa kuzungumza juu ya kuwasili kwake katika nchi hiyo amesema kuwa, wao watakuwa chini ya maongozi yake. Na kwa maana hiyo Balozi mpya amejibu: hapana mheshimiwa! kwasababu watajifunza kwa pamoja kutambuana ili waweze kwa pamoja kusaidiana kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa na jamii.

Na hili kuthibitisha zaidi ameongeza kwamba, maelekezo kamili wanapewa na Baba Mtakatifu, lakini kwa upande wake anasema, anayo shauku ya  kutambua Kanisa la Korea na Mongolia kwa kina na mapema iwezekanavyo ili aweze kuipenda na kuitumikia kwa dhati na kwa kufanya hivyo ni matumaini yake ya kujitakatifuza pamoja nao! Vile vile upendeleo wake ni ule wa  kuendeleza nyayo zile za wafuasi wake akitengeneza zake ndogo kwa ajili ya kujenga madaraja. Lakini ili kufanikiwa ni suala linahitaji mshikamano wa maaskofu  wote na wahudumu wao  wote, ili pamoja na mahusiano mema na Kharifa wa mtume Petro wanaweza kuwa thabiti daima. Hata hivyo si tu peke yao bali hata Kanisa na dini nyingine. 

Akifafanua zaidi anasema, ngao yake ya kiaskofu  imeandikwa ‘Ut unum sint’, maana yake ili wawe na umoa wamoja, ambayo  ni sala ya Yesu wakati anamwomba baba yake, na ili dunia ipate kuamini kwamba katumwa na yeye! Kwa njia hiyo Balozi mpya nchini Korea na Mongolia  anaamini sentensi hiyo katika urithi wa Yesu, itamwongoza na kutokana na ngao hiyo, anatarajia kujikita kwa dhati kujenga madaraja, hata kwa ngazi ya utamaduni. Hata hivyo utashi wake kwenda kushi katika jumuiya ya kikristo iliyo ndogo ndiyo upendeleo wake hasa kwa wakatoliki 1,300 nchini Mongolia. Kutokana na hiyo anathibitisha ya kuwa atatoa umakini zaidi na kuwaunganisaha pamha na jimbo la Gozo kisiwani Malta ili weweze kujenga umoja wa kuwa kama mapacha wa kuwasaida hata kwa upande wa msaada wa kifedha, dharura za kichungaji na uinjilishaji . 

Pamoja na hayo pia ameshawasiliana na Padre George Marengo mmisionari wa wakonsolata ambaye yuko nchini Mongolia karibia miaka 15, ambaye amempa taarifa nzuri kuhusu  wabatizwa nane katika usiku wa Pasaka. Aidha akisimulia juu ya upendo wake wa kimisonari anasema, tangu akiwa katika mafunzo  seminarini, alipendelea sana na kushangazwa na wamisionari. Na kwa namna hiyo lengo lake sasa ni kutaka kuwa kama wao, ili kupeleka mbele kazi ya umisionari hasa kwa kutangaza Neno la Yesu Gesu na kupokea wakristo wapya katika Kanisa!

Sr Angela Rwezaula 
Vatican news!








All the contents on this site are copyrighted ©.