2018-05-03 16:48:00

Kitabu kipya cha kufikiria maendeleo endelevu na mahusiano Ulaya kuchapishwa!


Kufikiria kwa upya maendeleo endelevu ya mahusiano, hotuba za Papa juu ya Ulaya, ndiyo kitabu kilicho andikwa na ambacho kitatolewa na Duka la vitabu Vatican. Kitabu kinakusanya tafakari msingi za hotuba zake ambazo Baba Mtakatifu Francisko amejikita kuelezea maana ya Ulaya kwa lengo kuu la kutaka  kurudisha uzalendo wake na kukabiliana na changamoto mpya ya wakati  ili kuweza kung’amua njia mpya za matumaini.

Kitabu hicho kitawasilishwa katika ukumbi wa kimataifa wa vitabu huko Torino nchini Italia, tarehe 11 Mei 2018 saa 10:30 za jioni masaa ya Ulaya, ambapo tukio hilo linatazamiwa kati ya washiki, uwepo wa Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, Katibu wa Mawasiliano Vatican Monsinyo Lucio Adrian Ruiz na wengineo watakao toa hutuba zao ikiwa ni pamoja na Frateli Giulio Cesareo mhusika wa uandisi wa vitabu katika duka la Vitabu Vatican  na ambaye ataongoza  mjadala.

Hotuba za Papa Francisko katika kitabu ni kama vile alizotoa kwa: wawakilishi wa sera za kisiasa, Mabaraza ya maaskofu na katika jamii ya raia wa Ulaya; tangu ziara yake katika  Bunge la Ulaya na Baraza la Ushauri huko Salzburg mnamo tarehe 25 Novemba 2014. Inafuatia hotuba wakati wa fursa ya kupokea Tuzo ya Karol Magno mnamo 6 Mei 2016; hotuba katika maadhimisho ya miaka 60 ya mikitaba ya Roma mjini Vatican tarehe 24 Machi 2017 na hotuba kwa wawakilishi wa Mkutano wa “(Re)thinking Europe”) mnamo tarehe  28 Oktoba  2017.

Na katika utangulizi wa kitabu hicho, Kardinali Pietro Parolin anakumbusha jinsi gani Papa Francikos amekuwa Papa wa kwanza kuzaliwa nje  ya Ulaya tangu karne VIII hadi siku zetu, lakini ameonesha tangu mwanzo umakini kwa namna ya pekee kwa bara la zamani,  Bara ambalo kwa miaka ya mwisho umeonesha ugumu na kulazimika  kukabiliana na changamoto mpya za kipeo.

Changamoto hizo zinahusiana  kipepo cha maono tofauti ambayo hakuna ambaye angetegemea bara la kizamani kuwapo! Kwa maana hiyo Kardinali Pietro Parolin anasema katika utungulizi wa kitabu hicho kwamba, Papa Francisko anafundisha kuwa, kipindi cha kipeo kisiwe ni kizingiti kisichopitika badala yake kiwe ni kipindi chenye fursa. Kardinali akirudi katika ziara ya Papa Francisko huko Lampedusa, mahali ambapo wanafikia wahamiaji na wakimbizi kupitia baharini, anasema ni ishara ya ugumu wa Ulaya, lakini wakati huo huo ni matumaini kwa watu walio wengi ambao wanaikimbilia na kutazama Bara la Kizamani!

Katika picha hiyo kipeo mshikamano kinachokosekana ndiyo kinachohitajika, ambapo Baba Mtakatifu hatoi maneno ambayo ni kinadharia tu bali ni kuonesha wasiwasi hasa ule wa kujikita katika matendo ya dhati kukabiliana na  hali halisi, katika matatizo ya kweli ambayo yeye binafsi anakutana nayo katika mikutano mbalimbali yak ila siku. Pamoja na hayo tafakari zake zote daima zinajikita katika kiini cha binadamu na mahitaji yake, uhusiano na hadhi yake. Na kwa maana hiyo Kardinali Parolin anasema, hatuwezi kufikiria kuwa Papa anatazama kupendekeza suluhisho katika  matatizo yanayo endelea kukusanyika baada ya jingine, badala yake yake, anatoa mchango mkubwa wa kuweza kusaidia kuondokana na kipeo hicho hasa kuwa na ule upeo wa hali ya juu ili angalau uwepo uwezekano na kiini cha chach ya kukabiliana na changamoto za wakati.

Katika utangulizi wa kitabu hicho pia Kardinali Parolin anaonesha moyo wa ujumbe kwa watu wa Ulaya: Papa Francisko kwa watu wa Ulaya anawaalika  kujitafuta wao wenyewe, roho yake, yaani tasaufi ya kibinadamu ambayo pamoja na kupenda, lakini pia  inalinda na kutetea. Ili kufanya hivyo Papa anatoa ushauri wa kushinda mantiki za binadamu anayetaka kujiondoa kabisa na dhana za kijamii na kimaadili. Kwa maana hiyo anazidi kupendekeza njia ya kuwa na maono ya mahusiano mema ya mtu ambaye yumo mstati wa mbele katika jumuiya na jamii.

Halikadhalika akielezea juu ya madhala ambayo yamejitokeza katika bara la kizamani anasema mantiki ya kujibagua ndiyo hasa ambayo imesambaratika katika nchi za Ulaya na kusababisha kuishi kiupweke. Katika maono hayo ndipo yanafungua kile kiitwacho utandawazi wa utofauti ambao unazaa ubinafsi. 
Kwa maana hiyo, Papa Francisko anatoa wito wa kuwajibika ambao umesimika mizizi yake katika ukweli na uwezo wa kutoa maisha katika mshikamano wa dhati.

Kadhalika Kardinali Parolin anasimamia juu ya mwaliko wa Papa Francisko wa kufanya kumbu kumbu ya wakati uliopita, kama kiini cha maisha ambayo ni ya wakati huu,  vilevile kufanya kumbukumbu ya asili ili kuweza kukabiliana na changamoto za leo na kesho, kwa maana hatari ya wakati huu, ni ile ya kupoteza maana ya mizizi binafsi, na  hivyo inahitajika kile ambacho Papa anakiita usambazaji wa kumbukumbu ili kutoa maisha na ubinadamu mpya anasisitiza Kardinali Parolin.

Hatimaye katika utangulizi wa kitabu hicho Kardinali Parolin anamalizia akiwatia moyo wa kuweza kurudisha kwa upya urithi wa mawazo na tasaufi ambayo inaelezea Ulaya na kuifanya iwe ya kipekee kwa namna ya utambuzi wa mtu kuanzia hadhi yake tangu kuzaliwa. Na katika dhana hiyo ni lazima uwepo wa  mchango wa wakristo ambao wanaalikwa kuwa roho ya Ulaya!

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!
All the contents on this site are copyrighted ©.