2018-04-24 14:48:00

Papa anazidi kuomba sala ili maombi ya wazazi wa Alfie yakubaliwe !


“Mshangao kwa sala na mshikamano mkubwa kwa ajili ya mtoto Alfie Evans, ninarudia wito wangu ili mateso ya wazazi wake yaweze kusikilizwa na kukubaliwa mapenzi yao ya kujaribu uwezekano mpya wa matibabu”. Ndiyo maneno ya Baba Mtakatifu Francisko katika Tweet yake tarehe 24 Aprili 2018 kufuatia suala la mtoto Alfie Evans nchini Uingereza. Suala hili la mtoto Alfie Evans, Mtakatifu Francisko aliligusia tarehe 15 Aprili mara baada ya Sala ya Malkia wa mbingu katika kiwanja cha Mtakatifu Petro na kusema: “ ninatoa umakini  mpya juu ya Vincent Lambert na juu ya mdogo Alfie Evans , ninataka kusema kwa nguvu na kuthibitisha kuwa mkuu wa maisha tangu  kutungwa kwake hadi mwisho wa uhai ni Mungu. Wajibu wetu ni kufanya kila iwezekanavyo ili  kutunza  maisha. Na tusali kwa ukimya ili maisha ya kila mtu  yaweze kuheshemiwa kwa  na zaidi kwa ndugu hawa  wawili”.

Vilevile Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya katekesi ya  Jumatano tarehe 18 Aprili 2018 alitoa wito wa aina mbili, kwanza kuhusu mkutano wa wahusika wa kifedha duniani kwa ajili ya maskini na wito wa pili  kwaajili ya kufanya kila iwezekanavyo kutunza maisha  hasa wa  mtoto Alfie Evans na Vincent Lambert. 

“Ninawakabidhi sala zenu kwa watu kama Vincent Lambert huko Ufaransa na mdogo Alfie Evans wa Uingereza na nchi nyingine wanaoishi wakati mwingine kwa kipindi kirefu cha magonjwa na kuhudumiwa na madawa kwa ajili ya  mahitaji msingi. Ni hali ambazo ni nyeti wakati huo za uchungu. Tusali ili kila mgonjwa daima aweze kuheshimiwa hadhi yake na kupata matibabu yanayostahili kulingana na hali yake , kwa kuafikiana na familia, madakatari na wahudumu wa afya kwa heshima kubwa ya maisha”.

Hata hivyo, Thomas Evans, baba yake na Alfie anashukuru Mawakili wa Diamond kusimamisha kwa muda mfupi mchakato,lakini mchakato unandelea japokuwa wanaomba iwe kama dharura ya kuendelea kusali ili Mungu aweze kuelekeza njia na kufika hatima ya janga hili, kwa namna ambayo ni njema ya kumwezesha Alfie aweze kusafirishwa! Mipira ya kumwezesha kupumua madawa ya uhai wa Alfie Evans ulisitishwa. Pamoja na hayo suala hili limejitokeza  kwa njia ya Mahakama Kuu ya Ulaya kuataa haki za binadamu ambayo na kutuèilia mbali maombi y wazazi hao bila kukubaliwa.

Mahakama iliwapokea wazazi wa Alfie ambao walikuwa wanaomba madaraka ya Uingereza wakubali mtoto wao aendelee na matibabu ya mtoto wao kuhamishwa katika hospitali nyingine. Hata hivyo Waziri wa Mambo ya nchi za nje  na ya ndani nchini Italia Bwana Alfano na Minniti wamekubali uraia wa mtoto Alfie kwa namna ya Serikali ya Italia kumwezesha urai ambapo unamruhusu mtoto kuhamishiwa Nchini Italia. 

Mariella Enoc,rais wa Hospitali ya Bambino Gesu Vatican,  alifika Liverpool kwa ajili ya suala hilo ambapo amepata kuzungumza na wazazi wa mtoto Alfie  na kuwa karibu nao, lakini  hakuweza kuongea na yoyote, pamoja na kwamba baba yake Alfie alikuwa ameomba wamwache aingie katika chumba cha mtoto; japokuwa isingesaidia kitu kwa maana,   saa 2.30  usiku wa Jumatatu ya 22 Aprili 2018, masaa ya Uingereza, madaktari waliondoa mashine ya mipira ya kupumua mtoto. Lakini kwa masaa 9 mtoto ameweza kuendelea kuishi  kabla ya kuwekewa hewa ya Oksijeni ya kawaida!

Baba yake  Alfie, Thomas Evans ameandika katika tweet yake asubuhi ya tarehe 24 Aprili 2018 kuwa: “Nimepambana kwa nguvu katika mahakama kwa ajili ya mtoto na kwasababu ninatambua kuwa siyo haki! Lakini tazama mahali nilipo mtoto wangu bado anaishi baada ya masaa 9 ya kutisha!

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!

 








All the contents on this site are copyrighted ©.