2018-04-21 15:18:00

Ziara ya Papa Francisko Bologna na Cesena iliwaachia tunu msingi!


“Baba Mtakatifu uliwafundisha familia ya kwamba: kuna maneno matatu ambayo hayatakiwi kukosa kamwe katika maisha ya kila:asante,kubisha hodi na samahani. Maelekezo hayo ya dhati na  rahisi yanayowezekana kwa kila mtu na ni njia ya utakatifu, kama vile mambo mengi yenye uwezakano ambayo unatueleza ya  kushangaza,  ya furaha ya kuwa watakatifu, labda ndiyo yanayohitajika kwa namna ya pekee ndani ya familia ambayo ni Kanisa”.

Ni maneno ya Askofu Mkuu Mateo Zuppi wa Jimbo Kuu la Bologna aliyo anza nayo wakati wa hotuba yake  ya utangulizi kuwakilisha jimbo la Bologna na Cesena waliokutana na Baba Mtakatifu katika viwanja vya Mtakatifu Petro Mjini Vatican tarehe 21 Aprili 2018. Askofu Mkuu Zuppi akitaka kusisitiza juu ya usemi wake anatoa mfano mwingine ya kuwa, mama wote tangu zamani walikuwa wakiwafundisha tangu utotoni jinsi ya kutoa ya kusema asante kila mara unapopewa zwadi kwa watoto wao. Hiyo ilikuwa ni elimu ili kuweza kuepuka aibu kwa watu wengine na kuwasaidia watoto waweze kutambua nini maana ya zawadi wanayoipokea. Kwa maana hiyo wazazi hao walikuwa wanahimiza watoe shukrani ya kusema asante. 

Askofu Mkuu  Zuppi anaongeza kusema kwamba , wazazi hao walikuwa na sababu kuu na msingi. Kwana  Zawadi siyo haki; siyo jambo jema la kupokea na kuunza binafsi ma kusahau kutoa asenta na upendo kwa yule aliyetoa zawadi. Kwa maana hiyo Askofu Mkuu ametumia maneo hayo akitaka kumwambia Baba Mtakatifu kuwa, kwa furaha kubwa wote   wanasema asante kwa ziara yake kutembelea Bologna na Cesena mnamo tarehe 1 Oktoba 2017. Pamoja na hayo tarehe 22 Aprili  inaangukia katika sikukuu ya uhuru wa mji wao Bologna, siku ambayo inawahamasisha kutambua na kukumbuka  wale ambao bado wanaishi chini ya shikashika za udikteta na ambao unazuia ufufuko wa amani. Mji wa Bologna ni huru kama nembo yao na kama mji ambao unatetea binadamu aweze kuondokana na kila aina ya utumwa.

Halikadhalika ameweza kukumbusha Baba Mtakatifu juu ya ziara yake ambayo aliweza kukutana na hali halisi ya Kanisa  ambao walikuwa wanaadhimisha Kongamano la Ekaristi  na  maandalizi ya ziara ya Baba Mtakatifu. Kutokana na hili anathibitisha kuwa, waamini wamebaki na furaha ambayo siyo rahisi watu kusahau, na hata hotuba zake ambazyo aliweza kuunganisha majimbo hayo kwa pamoja ambayo ni muhimu ili kuweza kugundua zaidi mzizi ya kina ya miji yao na kuenga kwa pamoja muungano ambo ni Kanisa.

 Amesisitizia pia juu ya matokeo baada ya ziara yake kwamba, furaha hiyo imegeuka uwajibikaji na utambuzi.  Mji wa Bologna haukusikiliza tu bali kwasasa unajaribu kuweka maneno ya Baba Mtakatifu katika matendo. Katika ziara yake, kwa namna ya pekee katika mazungumzo kati ya taasisi tofauti imewawezesha si katika kujenga kuta mpya, badala yake wanazidi kupyaisha ule utamaduni wa kupokea na kulinda, ili kila mtu binafsi au kikundi ndani yake wawajibike ka kujikita ndani ya   mtandao wa mahusiano.

Amehitisha mara baada ya kuelezea shughuli zote ambazo zimetendeka mara baada ya zaiara yake, akimshukuru kwa sababu ya kuwatia moyo na matumaini, na kwamba aliwasaidia kujitambua waoni akina nani na kuwasaidia watazaea wakati ujao kwa matumaini na ili washinde hofu na ukosefu wa uhakika. Kutokana na hayo wao wanamthibitishia kuwa, watajaribu kufuata ushauri wake kama tunu, kwa maana ziara yake imewahakikishia kutambua hata  mambo gani makubwa waliyo nayo  ambayo wanaweza kuendeleza thamani hiyo ndani ya kanisa na jamii kwa ujumla. Mfano wake, maneno yake na tabasamu yake vinawasaidia.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.