2018-04-21 15:02:00

Papa Francisko akutana na Wanajimbo wa Bologna na Cesena Vatican !


Ninawasalimia kwa furaha kubwa,  asante kwa uwepo wenu na matembezi yenu katika kaburi la Mtakatifu Petro, pia  ninyi kubadilishana na mimi ziara yangu katika Jumuiya ya majimbo yenu mnamo Mosi Oktoba mwaka jana, kwa hakika ninayo furaha kubwa! Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi 21 Aprili 2018  akitoa hotuba yake katika uwanja wa  Mtakatifu Petro mjini Vatican alipokuta na wawakilishi wa majimbo ya Bologna na Cesena. Wakisindikizwa na  Askofu Mkuu Matteo Zuppi wa jimbo la Bologna na Askofu Douglas Regattieri wa Jimbo la Cesena-Sarsina; Baba Mtakatifu anawashukuru kwa hotuba yao ambayo anakumbuka ukarimu na siku ile ya ziara yake katika majimbo yao. Bila kuwasahau hata viongozi wa umma,  mapadre, watawa, waamini walei  na zaidi hata wale ambao wanaungana pamoja katika hija hiyo kiroho kwa kwa namna ya pekee wagonjwa na wanaoteseka.

Baba Mtakatifu anakumbuka mapokezi mema aliyo pokelewa wakati wa ziara yake, imani na maombi waliyoshirikishana kwa pamoja na  ambapo waliweza kukusanyika waamini wengi toka pande zote za majimbo mengi. Kwake yeye ilikuwa ni zawadi kutoka kwa Mungu ambayo iliweza kumwimarisha na pia  kuwatia miyo na nguvu kwa maana ya imani ili kuhusika katika matendo hai, ndani ya Kanisa ambalo linataka kwa dhati kujikita kwa namna ya matendo na ishara hai za upendo, hasa kwa wale walio wadhaifu.

 Pamoja na hayo anakumbuka kuwa maaskofu wao wamesisitiza jinsi gani ziara ya kichungaji imekuwa sababu ya kupyaisha shughuli zao kwa upande wa jumuiya zao. Anawashukuru sana na kuwashauri waendelee kwa ujasiri katika safari waliyo anza.  Akikumbuka ziara aliyofanya katika jimbo la Cesena amekumbusha juu ya kumbukumbu ya miaka 300 tangu  kuzaliwa Papa Pio VI, hata wazo la Papa Pio VII. Kumbukumbu ya maaskofu wawili wa Roma lakini  wote wakiwa ni wazaliwa wa Cesena, imaimarisha wanajumuiya wa jimbo  kuwa na fursa kubwa ya kutafakari hatua za uinjilishji wao hadi sasa na mitazamo yake mipya ya kimisonatri ambayo inawasubiri.  Urithi wa watu hawa, hata ule wa wachungaji wengine na wainjilishaji. unawaalika kuendelea katika njia hiyo hiyo , kuwa na  ukarimu  wa kutangaza Injili kwa wazalendo wao, kushuhudia matendo  na ulazima ikibibidi pia kuwa chachu ya upendo, ya kindugu , ya matumaini ya ishara ndogo za kila siku. Baba Mtakatifu amehimiza wapende ishara ndogo ndogo za kila siku, kwa maana hata kama ni chachu ndogo, lakini wakati huo inatengeneza mambo mengi.

Na fursa ya ziara ya  kutembelea Bologna, Baba Mtakatifu amekumbusha kuwa: ilikuwa ni tukio la kuhitimisha Kongamano la Ekaristi Takatifu kijimbo.  Chachu  ya tukio la Kanisa, lililokusanya watu wengi kuzungukia Yesu wa Ekaristi,linaweza kuelendelea kwa muda mrefu bila kusita na kusinyaa ili liweze  kutoa matunda na kuacha ishala ambazo hazifutiki katika hatua ya imani ndani ya jumuiya ya kikristo.

Na kama alivyokumbusha katika Wosia wake wa Kitume  wa hivi karibuni  Gaudete et exsultate, “ kushirikishana Neno na kuadhimisha pamoja Ekaristi, wote tunakuwa ndugu na kugeuka taratibu jumuiya Takatifu na ya kimisionari” (Gaudete et exsultate n. 142). Kwa manaa hiyo Baba Mtakatifu anaongeza, Ekaristi inafanya Kanisa, inakusanya, inaunganisha katika kifungu cha upendo na matumaini. Bwana Yesu alianzisha ili sisi tuweza kukaa na yeye na kuwa mwili mmoja na kufutilia mbali tofauti ili kuweze kuwa wamoja na ndugu.

Baba Mtakatifu amesema, katika nyakati hizi, wana haja ya kukutana na Yesu Kristo, Yeye ni njia ambayo inalekea kwa Baba; Yeye ni Injili ya matumaini na upendo wenye uwezo wa kutusukuma kujitoa zawadi binafsi kwake. Na huo ndiyo utume ambao kwa kipindi cha uwajikabkaji na furaha, urithi wa wokovu na zawadi ya kushirikishana.Lakini inahitaji ukarimu wa kuwajibika na kujitoa, katika kujikabidhi binafsi kwa matumaini ya mapenzi ya Mungu. Ndiyo kutumiza mchakato wa utakatifu ambao unajibu wa ujasiri wa wito wa Yesu, kila mmoja kwa mujibu wa karama yake. Kwa upande wa Mkristo inawezekana kufikia utume wake binafsi katika ardhi bila kujua namna gani ya safari ya utakatifu itakuwa kwasababu ya mapenzi ya Mungu na utakatifu watu( taz” (1 Ts 4,3). Kila mtakatifu ni utume: ni mpango wa Baba ili kutafakari na kujikita kwa undani wakati wa historia ya maisha katika mantiki ya Injili (taz Gaudete et exsultate, 19).

Baba Mtakatifu amewatia moyo katika jumuiya za ona kualikwa katika utakatifu ambao unatazama kila mtatizwa na kila hali ya maisha. Katika utakatifu m, dimo unakamilishwa kila aina na tarajio ya moyo wa kibinadamu. Ni safari ambayo inaanzia katika kisima cha ubatizo na kuendelea hadi mbinguni: wakati huo huo ni kuishi kila siku kwa kupokea Injili katika maisha ya dhati.  Kwa shauku hiyo na matarajio ya kimisionari ambayo inataka kutoa upyaisho wa injilishaji katika majimbo yao, wataweza kujikita kwa dhati kwa kutafakari ushauri alio wapatia wakati wa ziara yake.

Wasichoke kumtafuta Mungu na Ufalme wake, wakijikita katika huduma kwa ndugu na kila mtindo rahisi wa kuishi kindugu. Na mama Maria Mtakatifu, kati ya watakatifu aliyebarikiw na ambaye anatuonesha njia ya utakatifu awasindikize aliye tayari  pia  kusikiliza na kusindikiza katika hatua zao zote  za uchungaji kimisionari.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.