2018-04-04 14:48:00

Katekesi:Papa anashukuru Mungu kugundua nini maana ya Misa!


"Ndugu wapendwa tazama leo hii kuna maua: Maua yanayoeleza furaha, shangwa, hata katika sehemu nyingine Pasaka inaitwa“ Pasaka iliyochanua. Kwasababu anachanua Yesu Mfufuka: Ni maua mapya: haki yetu inachanua, Utakatifu wa Kanisa unachangua. Kwa namna hiyo maua mengi ni furaha yetu. Juma zima sisi tunasheherekea Pasaka. Na ndiyo maana tunarudia kwa pamoja, kutakiana heri za Pasaka. Pasaka Njema!. “Tunaweza kumtakia Pasaka njema, hata aliyekuwa Askofu wa Roma, mpendwa wetu Papa Benedikto anayefuatilia kwa njia ya televisheni. Kwa Papa Benedikto tumpe heri ya Pasaka: Heri ya Pasaka”; “Tazama ni makofi ya nguvu”.  Huo ni utangulizi wa maneno ya Baba Mtakatifu Francisko aliyo anza nayo wakati wa kuanza Katekesi yake siku ya  Jumatano tarehe 4 Aprili 2018 katika viwanja vya Mtakatifu Petro mjini Vatican, kwa waamini wote na mahujaji kutoka pande  zote za Dunia.

Baba Mtakatifu anasema: Na katika katekesi hii tunahitimisha mzunguko mzima kuhusu Misa Takatifu ambayo ndiyo kumbukumbu lakini si tu kumbukumbu bali ni kuishi kwa upya mateso na fufuko wa Yesu: mara ya mwisho tulikuwa tumefikia mwisho wa komunio na maombi ya baada ya kumunio. Misa inahitimishwa na Baraka inayotolewa na Padre na kuwaaga waamini.  Kama ilivyokuwa mwanzo wa kuanza Misa na ishara ya msalaba, kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu,na ndiyo tena, kwa jina la Utatu Mtakatifu unahitimisha katika tendo la kiliturujia.

Licha ya hayo Baba Mtakatifu anaendelea kufafanua kuwa; tunatambua vema ya kwamba, wakati Misa inamalizika, inafunguliwa hatua mpya ya kuweka jitihada ya ushuhuda wa kikristo. Akristo hawendi katuka Misa ili kufanya mazoezi ya wiki na baadaye kusahau, hapana . Wakristo wanakwenda Misa ili kushiriki mateso na ufufuko wa Bwana na baadaye kuishi zaidi kama wakristo. 

Na tunatoka ndani ya Kanisa na kwenda kwa amani, ili kupeleka baraka ya Mungu katika shughuli zetu za kila siku, katika nyumba zetu, katika maeneo yetu ya kazini, kati ya mahangaiko ya maisha ya dunia hii, kwa kutumkuza Bwana katika maisha yetu. Lakini tunapotoka ndani ya Misa tukaanza  masengenyo, kwa kutazama huyo na yule, nakuwa na ulimi mrefu, misa hiyo haikupata nafasi ndani ya moyo wakko, kwasabu gani? Ni kwasababu ya kukoksa ule uwezo wa kuishi kwa ushuhuda wa kikristo. Kila mara unapotoka katika Misa lazima utoke vema zaidi ya ulivyoingia ndani ya Kanisa, yaani ukiwa na maisha zaidi, nguvu zaidi na shauku  zaidi ya kutoa ushuhuda kikristo. Kwa njia ya Ekaristi, Bwana Yesu anaingia ndani mwetu, katika moyo na katika mwili ili sisi tuweze kujieleza katika maisha ya Sakramenti tuliyo ipokea kwa imani (taz Misala ya Roma, sala ya maombi Jumatatu ya Pasaka).

Kutoka katika maadhimisho ya Misa hadi kufikia maadhimisho ya maisha ya kila siku, kwa utambuzi kwamba Misa inapata ukamilifu na uchaguzi wa dhati kwa yule anayejikita hawali ya yote binafsi katika fumbo la Kristo. Baba Mtakatifu anaongeza kusema:Tusisahau kwamba tunadhimisha Ekaristi Takatifu ili  kujifunza kugeuka kuwa wanaume na wanawake wa Ekaristi. Lakini je ina maana gani ?Maana yake ni kuacha Yesu aweze kutenda kazi yake ndani ya shughuli zetu; , mawazo yake yawe mawazo yetu, hisia zake, ziwe hisia zetu, uchaguzi wake uwe uchaguzi wetu. Na huo ndiyo utakatifu kufanya kama alivyofanya Kristo utakatifu wa kikrsto.

Hayo yanafafanuliwa vema na Mtakatifu Paulo, lipokuwa akielezea kufananishwa na Yesu kwamba: “Mimi nimeuawa na pamoja na Kristo msalabani na sasa naishi, lakini si mimi tena, bali Kristo anaishi ndani yangu, Maisha haya ninayo ishi sasa naishi kwa amani, imani katika Mwana wa Mungu aliyenipenda hata akatoa maisha yake kwa ajili yangu” (Gal 2,19-20). Baba Mtakatifu anaongeza kusema: “Huo ndiyo ushuhuda wa kikristo”. Uzoefu wa Mtakatifu  Paulo unatuangazia hata sisi kwani iwapo kipimo hicho ni  kujaribu kupunguza ubinafsi, kuacha Injili itawale maisha yetu na kuwa karibu na Yesu katika Upendo wake na ambao unaunda ndani mwetu nafasi kubwa kwa ajili ya nguvu ya Roho wake.

Wakristo ni wanaume na wanawake wanaoacha nafasi yao mioyo yao ipanuliwe na nguvu ya Roho Mtakatifu, mara baada ya kupokea Mwili na Damu ya Kristo. Baba Mtakatifu anahimiza kuwa; “panueni roho na kuachana na roho zilizo finyu na kufungwa kwa mambo madogo madogo ya ubinafsi. Kuweni na roho pana, zenye kuwa na upeo mkubwa. Mwachie  roho hizo zipanuliwe na nguvu ya Roho, baada ya kupokea Mwili na Damu ya Kristo, amesisitiza Baba Mtakatifu Francisko!

Kwa kawaida uwepo wa hai wa Kristo katika Mkate uliobarikiwa haiushii katika Misa tu (KKK 1374), Ekaristi unatunzwa katika Taberkulo kwa ajili ya kumunio ya wagonjwa na kwa ajili ya kuabudu kwa ukimya kwa Bwana katika Sakramenti Takatifu: Ibada ya Ekaristi nje ya Misa, ikiwa ni faragha, hata katika jumuia, inasaidia kwa namna ya pokee kubaki na Kristo ( Taz KKK 1378-1380).

Matunda ya Misa Takatifu kwa dhati yanakomaa katika maisha ya kila siku. Tunaweza kukazia kwa nguvu kwamba Misa ni kama ngano ambayo inakuwa katika maisha ya  kila siku na kukomaa hadi kufikia katika matendo na tabi njema ambazo zinafanana na za Yesu. Matunda ya Misa kwa hakika lazima yakomae katika maisha ya kila siku. Kwa hakika, kukua katika umoja na Kristo, Ekaristi inapyaisha  neema ambayo Roho ametupatia kwa njia ya Ubatizo na Kipaimara, ili iweze kuaminika katika ushuhuda wa kikristo ( KKK 1391-1392).

Zaidi ikiwasha katika mioyo yetu, ule upendo wa Mungu, Ekaristi inatutengenisha na dhambi: Na  kadiri tunavyoshiriki maisha ya Kristo ndivyo tunazidisha kuwa na urafiki wake na vigumu kutengenishwa kwa dhambi ya kifo ( KKK 1395). Kujongea kawaida katika meza ya Ekaristi, inapyaisha, inaimarisha na kujikita kwa udnani ule uhusiano wa jumuiya ya kikristo ambamo tunashiriki kwa mujibu wa misingi ambaye Ekaristi inafanya Kanisa (KKK 1396).

Hatimaye, kwa kushiriki Ekaristi, tunajikita katika kukabiliana na maskini kwa maana mi kuleimika kupitia katika mwili wa Kristo na kwenda katika mwili wa ndugu, ambao wanasubiri  waweze kutambuliwa, kuhudumiwa, kuheshimiwa na kupendwa(KKK1397).  Kwa kubeba hazina ya umoja na Kristo katika vyombo vya udongo (taz 2 Kor 4,7) tunahitaji kurudi katika Altare Takatifu hadi mbinguni na kuonja ule utimilifu wa Heri za wale walioalikwa kwenye Karamu ya harusi ya Mwanakondoo (taz Uf 19,9).

Baba Mtakatifu Francisko amemalizia kwa kumshukuru Mungu kwa safari ya ugunduzi wa Misa Takatifu: kwayo tumezawadia naye ili kutimiza pamoja na kuacha kuvutiwa na imani iliyo pyaishwa katika kukutana na  Yesu wa kweli, aliyekufa na kufufuka kwa kwa ajili yetu na kwa wakati wetu! Na maisha yetu daima yaweze kuchanua kama ya Pasaka, kwa maua ya matumaini, imani na matendo mema. Na sisi tuweze kupata nguvu daima katika Ekaristi, umoja na Yesu. Pasaka njema kwa wote!

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.