2018-03-31 12:04:00

Papa amemteua Askofu J.P. Kwambamba Masi kwa jimbo la Kenge (DRC)!


Baba Mtakatifu Francisko amekubali maombi ya kung’atuka katoka shughuli za Kichungaji kwa Jimbo la Kenge, nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Askofu Jean Gaspard Mudiso Mund’la, S.V.D., Wakati huo huo amemteua Askofu Jean-Pierre Kwambamba Masi, S.V.D., ambaye hadi uteuzi wake alikuwa Askofu msaidizi wa Jimbo Kuu la Kinshasa. Askofu Jean-Pierre Kwambamba Masi, alizaliwa mnamo tarehe 19 Agosti 1960 huko Ngi, Wilaya ya Bandundu (DRC). Mara baada ya mafunzo wa hawali huko Bandundu na  Bulungu (1967-1973), alijiunga na seminari ndogo ya Mtakatifu Karoli Lwanga huko Kalonda, mahali ambapo alweza kuhitimisha masomo ya sekondari (1973-1979). Aliendelea na masomo ya Falsafa katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Augostino, huko Kalonda (1979-1982), Taalimungu katika Seminari Kuu ya  Mtakatifu Yohane wa XXIII mjini Kishasa (1990-1992). Na kupewa daraja Takatifu la Upadre mnamo tarehe 17 Agosti 1986.

Baada ya kupewa daraja ya Upadre, aliweza kushika  nyadhifa  mbalimbali kama ifuatavyo:1987-1992: Masomo ya uzamivu  wa shahada ya Liturujia katika Chuo cha Mkatifu Anselm mjini Roma;  1992-1994: Profesa katika Seminari ndogo ya Mtakatifu Karoli  Lwanga, huko  Kalonda; 1994-1998: Vika wa Askofu Jimboni Kenge; 1998-2003: Gombera wa Seminari Kuu ya Taalimungu ya Mtakatifu Cyprien wa  Kikwit; na  tangu 2003, alichaguliwa katika ofisi za  Baraza la Kipapa la Nidhamu na Sakramenti za Kanisa, pamoja na maadhimisho ya liturujia za Papa. Wakati huo, mnamo tarehe 31 Machi 2015, akateuliwa kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo Kuu la Kishasha (DRC).

Na Sr. Angela Rwezaula 
Vatican News!

 








All the contents on this site are copyrighted ©.