2018-03-30 16:20:00

Matashi mema ya Pasaka kati ya Mkuu wa Wayahudi Roma na Papa!


Katika fursa ya Sikukuu ya Pasaka, Mkuu wa Wayahudi mjini Roma, Bwana Riccardo Di Segni ametuma matashi mema kwa Papa Francisko ya kwamba sikukuu hizi zinakwenda sambamba na kalenda yao ya Sikukuu ya kiyahudi ya Pasaka kwa mwaka huu, hivyo hana budi kumtakia matashi mema ya utulivu na amani na wakati huo huo,  hata Papa Francisko naye  amemtumia salam za matashi ya Pasaka katika matarajio ya sikukuu yao (Pesach) yeye binafsi na jumuiya nzima ya Kiyahudi mjini Roma.

Papa anasema kuwa " Mungu mwenyezi kwa neema zake, awabariki na kuwasindikiza katika safari ya wapendwa, watu wa kiyahudi". Anawahakikishia sala zake,lakini pia akiomba nao wasali kwa ajili ya Papa. Na "Mungu Mkuu awajalie wakue daima katika urafiki na  upamoja wa kuwa mashuhuda wa amani na mapatano.

Sr Angela Rwezaula 
Vativcan News!

 

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.