2018-03-26 16:02:00

Papa akutana na wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama wa raia Vatican


Tarehe 26 Machi 2018 Papa Francisko amekutana na Wakuu wa Vikosi vya  Polisi na viongozi wengine wa Vikosi vya  Ulinzi na Usalama mjini Vatican. Wakati wa hotuba yake amewashukuru kwa fursa hiyo ambayo ni ya utamaduni na kwamba inampatia fursa ya kuweza kutoa shukrani zake kwao  juu ya huduma yao  wanayo itoa katika Makao Makuu ya Kitume na mjini Vatican. Kwa namna ya pekee ameshukuru hotuba ya Mkuu wa Polisi aliyosoma kwa niaba ya wote. Amewashukuru kila mmoja na kuwapa matashi mema ya Pasaka ambayo inaangazwa na imani thabiti na kuimarishwa kwa upendo na thamani nzuri zaidi na kweli zaidi!

Usimamizi wao wa umma kwa kutoa usalama ni unatoa thamani ya kushirikiana katika utume wa kichungaji wa Askofu wa Roma. Anawasifu kwa shughuli za ulinzi wanazojikita wakati wa maadhimisho yote ya Liturujia na idai kubwa za maadhimisho katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na mikutano mingi itolewayo katika mji wa Vatican kwa ujumla; anaongeza: Papa na wahudumu wake wanatambua vema ya kwamba wanaweza kutegemea sana msaada wao wa ushirikiano katika mchakato mzima  wa ziara zake za  kichungaji katika Parokia, Taasisi za raia na Kanisa la Roma, kama ilivyo hata  katika fursa za ziara zake za  kichungaji nchini Italia.

Shukrani nyingi kwa kazi nyeti ya ulinzi wa mahujaji kutoka pande zote za dunia ambao wanakuja kutembelea Kaburi la Mtakatifu Petro, ili waweze kuishi kwa utulivu wakati wa kufanya uzoefu muhimu wa imani. Papa Anathibitisha kuwa wao wana jukumu  kila siku la kuimarisha na kukuza mawazo ya raia ambayo ni ya kibinadamu, hasa zaidi kama wanachama wa Polisi ya Taifa la Italia.

Tendo la kukutana na matukio mbalimbali ya Kidini, utamaduni, na mapadre watawa, walei ambao wanashirikiana kwa pamoja kupeleka mbele utume wa mtume  Pietro katika  dunia, ni matumaini yake kwamba, wanapata mwamko na  juhudi kwa kazi yao.  Hali ya kazi wanayokutana nayo inawawezesha kila mmoja kuongeza hata juhudi katika taaluma yao ili kuweza kutoa kirutubisho na nguvu zaidi ya ukweli wa Injili. Katika kushuhudia kwa namna ya kazi yao, thamani ya kibinadamu na tasaufi ya kikristo, wao wanaweza kutoa mchango hata kwa utume wa Kanisa.

Vatican ni kilele ambacho si kwa ajili ya wakristo tu kutoka pande zote za dunia bali hata wawakilishi wa madhehebu mengi ya kidini, wahusika wa Mataifa na watu wengine wa kanisa na raia ambao wanakuja Roma kukutana na Papa au wahudumu wa Mabaraza ya Kipapa. Shukrani nyingi kwa kazi yao, katika mikutano ya mazungumzo na matembezi yao wa ushuhuda wa utamaduni na imani ili  waendelee kulinda mji wa Vatican. Kufanya kila tukio liweze kufanyika katika hali ya utulivu na utaratibu mzuri.

Akirudia kwa mara nyingine tena kusifu mshikamano wao wa kazi, amewakabidhi kila mmoja kwa ulinzi wa Mama wa Mungu. Awalinde na kupokea nia zao ili azifikishe kwa mwanae Yesu Kristo.  Kwa namna ya pekee wazo limewaendea kwa familia wao zaid  watoto wao ambao amesema kuwa ni muhimu sana kwao, hivyo ameomba hata wao wasali kwa ajili yake na kuwatakia Pasaka njema!
 
Sr Angela Rwezaula
Vatican News! .

 








All the contents on this site are copyrighted ©.