2018-03-22 15:27:00

Kard.Bassetti:Italia kwa sasa inahitaji kuishi undugu na upendo zaidi!


Tarehe 19-21 Baraza la Maaskofu Italia wamefanya mkutano wao Na wakati wa hitimisho la mkutano huo, Kardinali Gualtiero Mwenyekiti wa Baraza hilo na Katibu Askofu Glantino wametoa taarifa yao ya mwisho. Katika hotuba ya kardinali  Bassettti  mada nyingi amegusia na hasa amekumbuka juu ya uchanguzi wa kisiasa uliofanyika tarehe 4 Machi, na kuwakumbusha kuwa vyama vina haki lakini pia  majukumu ya kuongoza na kuelekeza jamii. Kardinali kwa maana  hiyo anasema Bunge linapaswa kujieleza kwa kiasi kikubwa na kutafsiri si katika nguvu za kisiasa lakini zaidi kutafakatri juu ya mahitaji msingi ya watu kuanzia kwa wale wanaohitaji zaidi.

Akiendelea na hotuba hiyo ujumbe wake ulikuwa wazi, hasa wa nguvu kuelekeza katika sera za kisiasa ya kwamba, inawezakana kuongoza mahali hadi kufikia unapoweza, lakini ikiwa ni kwa uvumilivuna umakini wa wazalendo na kutafuta wema kwa ajili ya nchi. Anakumbuka maneno ya kiongozi wa zamani wa nchi Bwana Alcide Del Gasperi aliyoyatamka mwaka mmoja kabla ya kifo chake, wakati wa kufunga kampeni za uchaguzi tarehe 5 Machi 1953 mjini Roma. Maneno hayo yalikuwa:katika kampeni hii ngumu, kuna maneno ya kampeni nyingi zinazo hamasisha chuki, na  maneno ya kubomoa na kulipiza visasi. Lakini raia wa Italia wanahitaji undugu na upendo. Askofu Bassetti anaongeza kusema, ni kweli kwamba wote tunahjitaji huo undugu na upendo. Ni mamilioni ya maskini ambao wanaomboleza kupata ukombozi wa matendo ya kijamii; mamilioni ya watu ambao wanaishi kwa shida ma mahitaji kuzidi kuongezeka, upungufu wa kizazi endelevu; mamilioni ya vijana kukosa ajira na kubaguliwa. 

Inahitajika upendo na undugu zaidi. Kuna jamii inayohitaji kuwa na amani. Kuna matumaini ambayo yanapaswa kujengwa. Kuna nchi ambayo inapaswa kushona mipasuko na hivyo Kardinali anaongeza; aliye na uwezo wa kupima mitazamo hiyo ni lazima kutafuta njia ya kuweza kutambea kwa pamoja.  Katika hotuba hiyo pia anaonesha wasiwasi mkubwa ya wakati endelevu kwa jamii waliyo nayo hasa kwa upande wa ukosefu wa ajira kwa vijana, umaskini wa familia, watu wengi waliobaguliwa pembezoni, vilevile akikimbuka hata wahamiaji, anasema kwamba, kuna hatari inayozidi kuongezeka ya  kufunga milango. 

Kardinali ameita kipindi hiki ni cha vuli kwasababu kinadiriki kuongeza matendo ya  kujisikia, ugonvi, hasira ya kijamii, hata ongezeko la ukosefu wa heshima kati yao  kwa wale ambao wanapatana fursa ya uongozi. Hotuba yake Kardinali pia anamtakia  matashi mema  Baba Mtakatifu Francisko kama makanisa yote walivyo fanya kutokana na kutimiza  miaka mitano tangu achaguliwa na  ili aweze kuendelea vema na hija yake ya kitume. Anaonesha uzoefu wa kushirikishana kwa maelfu ya vijana nchini Italia unaotarajia kufanyika katika maeneo mbalimbali ya Italia na kuhitimisha  hija hiyo ya imani mjini Roma kwa kukutana na Papa Francisko tarehe 11-12 Agosti 2018. 

Kadhalika juu ya Hija ya Sinodi ya Maskofu ijayo  kuhusu Vijana imani na Mang’amuzi ya miito, ambayo anathibitisha kuwa  sasa inaendelea kutoa fursa nyingi katika majimbo yote ya Italia kujiandaa katika tukio hili muhimu la kutaka kuwasikiliza kizazi kipya, aidha anasema ni fursa ya kuweza kujadiliana na taasisi zota mahalia za elimu na kazi. Pamoja na hayo Kardinali anasisitiza juu ya kutoa ushuhuda wa vijana kwasababu ya maisha yao  na kitovu cha mahusiano mema kwa njia ya nguvu ya Injili, ambayo kwa upande wake anasema inaweza bado kuleta mwangaza na kumfungulia nini maana ya maisha ya kweli ya kila binadamu.

Utambuzi wa ukomavu kwa upande wa kizazi kipya ni muhimu kutokana na kwamba unaweza kuwafanya waweze kujituma na kujitoa kwa ajili ya wengine. Na ndipo anajikita kwa mada ya nini maa ya kuwa  baba hasa kwa upade wa makleri, ili wawe makini kujikita katika ujezi wa  mahusiano na mshikamano na kufundisha mambo mengi yanayohusu hata dharura inayoikabilia jumuiya nzima,na ndiyo huduma yao ya kichungaji. Ametoa taarifa juu ya  mkutano mwingine maalumu utakao fanyika kunzia  mjini Roma tarehe 12 – 15, Novemba 2018. Na mwisho kwa mtazamo mzima wa masuala ambayo yanatarajiwa kufanyika mwaka huu kwa ujumla.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.