2018-03-09 15:24:00

Askofu Nunzio Galantino:Jirani ni mtu ninaye kutana naye na kuwa na ukaribu!


Jirani ni mtu ninaye kutana naye, ni mtu yoyote ambaye anapitia mchakato wa historia ya maisha yangu ya kila siku, na zaidi siyo jambo muhimu kutambua yeye ni nani, bali jambo msingi ni lile la kuwa na mtazamo wa macho ya ukaribu.Huo ni uthibitisho wa meneno katika mahubiri yake Askofu Mkuu Nunzio Galantino, Katibu Mkuu wa Baraza la Maskofu Italia (CEI) tarehe 9 Machi 2018, wakati wa misa ya kufungua siku ya pili na ya mwisho ya Mkutano wa Kitaifa kuhusu Kazi ya kuchungaji katika vyuo vikuu, iliyokuwa na kauli mbiu Kanisa na Vyuo vikuu ni kambi za matumaini”. 

Ni katika  mkutano uliotayarishwa na Ofisi ya Kutaifa ya Baraza la Maaskifu wa Italia  kwa ajili ya mafundisho, shule na Vyuo vikuu vya hilo, kwa ushirikiano na Huduma ya taifa kichungaji kwa vijana. Askofu Galantino akiendelea na mahubiri yake juu ya mahitaji ya jirani kutokana na Injili ya siku kutoka Mtakatifu Luka 12:28-34), ambayo ilikuwa na kitovu juu ya  amri kuu ya upendo wa Mungu na jirani,anathibitisha kuwa, ni rahisi kuangukia zaidi katika  shughuli ya utoaji wa huduma  kama ilivyo kawaida, wakati huo huo  lakini bila kuwa na mtazamo wa macho ya kindugu na ukaribu wa dhati.  Aidha utoaji wa huduma wakati huo huo kusahau jinsi gani mtu anayehudumia ameumbwa namna gani. Binadamu anahitaji kwanza mshikamano, ukaribu,kushirikishwa na upendo. Siyo mtu wa kuhudumiwa kwa kutazama sura tu, bali hata kutambua hata  mahitaji yake msingi. Binadamu ahitaji sahani ya chakula tu, bali hata huduma ya kupewa meza apate kukaa na kula chakula hicho. 

Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Galantino amesisitiza  kuwa  iwapo katika jumuiya yoyote haikai na kusikiliza  Neno la Mungu, ipo hatari kubwa ya kutotambua jirani huyo ni nani na kugeuzwa dharura na kusahau umakini, ukaribu, ushirikiano, ushikishwaji na upendo wa dhati. Akitoa mifano zaidi anasema hiyo ndiyo hatari inaojitokeza katika baadhi ya  jumuiya  ambazo utakuta wanaanzisha mambo mengi kwa ajili ya wahitaji, wakati huo huo hawana uhusiano wa karibu na upendo kwa wale wanao wahudumia,jambo ambalo lingekuwa ni jema katika kukuza ukaribu na urafiki

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.