2018-03-05 13:34:00

Kuna umuhimu wa kukuza Injili ya uhai na tunu msingi za kifamilia!


Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu, tarehe 5 Machi 2018 amekutana na kuzungumza na Chancellor Sebastian Kurz wa Austria, ambaye baadaye, alibahatika kukutana na kuzungumza pia na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Monsinyo Antoine Camilleri, Katibu mkuu msaidizi wa Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko pamoja na mgeni wake, wamegusia kuhusu uhusiano mwema wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili pamoja na kukazia umuhimu wa kujizatiti kulinda na kudumisha Injili ya uhai dhidi ya utamaduni wa kifo; tunu msingi za maisha ya familia pamoja na kuendeleza mafao ya wengi ndani ya jamii, kipaumbele cha kwanza kikiwa ni maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii! Katika mazungumzo haya, viongozi hao, wamegusia pia mchango wa Austria katika Umoja wa Ulaya kwa kutaka umoja na mshikamano kati ya watu, kupewa msukumo wa pekee. Mwishoni mwa mazungumzo yao, Baba Mtakatifu Francisko na Bwana Sebastian Kurz wamepembua kwa mapana kidogo masuala ya kimataifa, ikiwemo changamoto ya kulinda na kudumisha amani, wahamiaji na wakimbizi pamoja na rufuku ya kutengeneza, kuhifadhi na kutymia silaha za kinyuklia.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.