2018-03-03 13:28:00

Papa Francisko atakutana na Jumuiya ya Mt.Egidio tarehe 11 Machi 2018!


Msemaji mkuu wa Vatican Bw. Grek Burke anathibitisha kuwa tarehe  11 Mach 2018 saa 10.30 jioni  masaa ya Ulaya  katika Uwanja wa Mtakatifu Maria Trastevere, Baba Mtakatifu Francesko atakutana na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, kufuatia tukio la maadhimisho ya Jubilei ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.

Katika uwanja huo wataadhimisha liturujia ya Neno na kukutana na watu wa jumuiya hiyo ambao ni vijana, watoto wa shule ya amani, watu wenye ulemavu, watu wa maabara ya sanaa wasio kuwa na mahali pa kukaa, na ambao kwa siku hizi za baridi wamekaribishwa katika jumuiya hiyo, wazee na maskini, rafiki wa Jumuiya,kati yao hata wahamiaji waliofika nchini Italiwa kwa njia  halali “iitwayo   mkondo wa kibinadamu”.

Jumuiya ya Mtakatifu Egidio imepokea kwa furaha habari hiyo ya  ziara yake katika makao makuu ya Jumuiya ya Mtakatifu Egidio  Trastevere, tarehe 11 Machi, mahali ambapo jioni ya siku hiyo Baba Mtakatifu atashiriki nao na kutoa hotuba yake wakati wa maadhimisho ya liturujia ya Neno. 

Baba Mtakatifu atakutana na jumuiya hiyo katika tukio hilo, kuanzia na mwanzilishi, Andrea Riccardi ambaye kwa miaka 50 iliyopita alianzisha safari hiyo ya jumuiya ndani ya umbu la mji wa Roma wakiwepo wawakilishi kutoka miji mbalimbali ya Italia na duniani.

Kwa waandishi wanaotaka kuudhuria siku hiyo wanaweza kupta maelezo zaidi kupitia: http://press.vatican.va/content/salastampa/it/accrediti/pubblico/accredito.html

Na Jumuiya nzima ya Mtakatifu Egidio inashukuru na kusubiri kwa shauku na upendo kukutana na Baba Mtakatifu Francisko!

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.