2018-02-28 16:16:00

Barua ya Kard. Parolin kwa Askofu Paglia katika Mkutano wa Tiba mbadala!


Barua ya Kardinali Pietro Parolin kwa Askofu Mkuu Vincenzo Paglia Askofu wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Maisha katika  tukio ya mkutano kimataifa  wa afya juu ya tiba mbadala ya wagonjwa ambao hupata tiba mbadala hadi kusindikizwa kufikia mauti, kwa njia hiyo, tiba mbadala ni ile ya kusaidia kuendeleza na kusindikiza ubora wa maisha ya wagonjwa, na kwa kufanya hivyo yahitaji upendo na uvumilivu mkubwa.
 
Mkutano huo umeandaliwa  na Baraza la Kipapa kwa ajilio ya  Maisha. Katika barua hiyo Kardinali Pietro Parolin anasema kwa niaba ya Baba Mtakatifu na yeye binafsi wanatoa salam kwake yeye, wandaaji na washiriki wa Mkutano huo wa Tiba mbadala.

Kardinali Pietro Parolin anasema, Mkutano wao unatazama masuala ya kipindi cha mwisho wa maisha yetu hapa duniani kwa kila kiumbe, ili kukabiliana na kikwazo ambavyo wakati mwingine uonekana kisichoweza kupitika kwa uhuru na wakati mwingine kuonekana hata kiburi na uchungu. Kwa namna hiyo katika jamii za sasa inatafuta njia nyingi za kuzuia na kuondoa, wakisahau kusikiliza ushauri wa zaburi : Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu, ili tujipatie moyo wa hekima (Zab 89,12). Tunapata ujajiri ambao unaficha ndani yake na kuwa fursa ya ukomavu kwa namana ya kusihi katika ngazi binafsi na kijamii.

Matibabu mbadala, badala yake haifichi hekima hiyo na ndiyo sababu msingi na umuhimu wa dhana hiyo. Wao wanaendelea kutafuta namna ya kugundua wito wa kina hata katika  madawa, ambayo hawali ya yote ni kuwasaidia katika shughuli ya kuwatibu daima  hata kama si kupona lakini kuwasindikiza. Matibabu mbadala yanaendelea kufanyika kwa kawaida andani ya mahospitali  na vituo vya afya kwa utambuzi wa mipaka yake ambayo pamoja na kutetea kwa sasa inajulikana na kukubaliwa. 

Mantiki ya kutibu inahitaji msingi mkuu ambao ni upendo  hasa kwa wagonjwa wakati wa mateso na pale wanapofikia  mwsiho wao, lakini pia  ni hali halisi ya mahusiano yote ya binadabu ambayo si rahisi kuwa kinyume na tabia hiyo. Kama Mtakatifu Paulo asemavyo “Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria”(13,8).

Upendo wa karibu ni njia ambayo inaweza kuwasha cheche katika uzoefu wa upendo wa kushirikisha na maisha ya binadamu kufikia fumbo la mwisho ambalo ni kuaga dunia, kwa njia lakini ya kutanza neno la kiinjili ambalo linawatzaama watoto wote wa Baba mmoja mwenye kutambua kila mmoja kuwa ni mfano na sura yake isiyokiukwa.

Mpango wa mkutano wao kwa siku hizi unaweka bayana mambo makuu msingi ambayo yanajikita katika matendo ya  matiababu mbadala. Kazi ambayo inahitaji utaalam, sayansi na mipangilio mizuri  , uhusano na kuwasiliano  ikiwa ni pamoja na kusindikizwa kiroho na sala.

Pamoja na sura tofauti za wataalam, Kardinali Parolin anasisitiza umuhimu wa familia katika mchakato huo . Familia inachukua nafasi msingi, kama sehemu ya mshikamano kati ya kizazi kinachowakilishwa; kama kiunganishi cha mawasiliano ya maisha na upamoja wa kusaidina wakati wa mateso au ugonjwa.

Ugumu na unyeti wa mada ya sasa ya tiba mdala inahitaji tafakari endelevu  na kuisambaza kwa njia ya matendo.Ni shughuli ambayo waamini wanaweza kujikita kama mwenza katika safarii ya watu wengi wenye mapenzi mema. Hiyo ina maana ya kuwa na mzatamo hasa zaidi sasa katika mkutano wao kwa washiriki wangi wa dini na utamaduni ili kujikita kwa kina katika shughuli hiyo.
 
Hata mafunzo ya wahudumu wa afya , wahusika wa umma,kwa jumuiya nzima ni mhimu kuongeza nguvu hizi na kuzipeleka mbele. Aidha amesisitiza kuwa katika shuhuli za Baba Mtakatifu anawatumia salam kuwapa Baraka ya kitume.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.