2018-02-27 11:31:00

Askofu mkuu Josè Avelino Bettencourt ateuliwa kuwa mkuu wa Itifaki


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Josè Avelino Bettencourt kuwa Mkuu wa Itifaki ya Vatican pamoja na kumteua kuwa ni Balozi wa Vatican. Askofu mkuu Bettencourt alizaliwa tarehe 23 Mei 1962 huko Azzorre, Ureno. Baada ya majiundo na malezi yake ya Kikasisi, kunako tarehe 29 Juni 1993 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre, Jimbo kuu la Ottawa, Canada. Ana shahada ya Uzamivu katika Sheria za Kanisa.

Alianza utume wake katika masuala ya kidiplomasia mjini Vatican kunako tarehe 1 Julai 1999. Katika maisha na utume wake tangu wakati huo, ametoa huduma kwenye Ubalozi wa Vatican nchini DRC na baadaye kwenye Idara ya mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa.  Baadaye aliteuliwa kuwa mkuu wa Itifaki ya Vatican, hapo tarehe 14 Novemba 2012.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Vatican News.








All the contents on this site are copyrighted ©.