2018-02-23 15:32:00

Tarehe 21 Februari 2001 Askofu Jorge Mario Bergoglia aliteuliwa kuwa Kardinali!


Ni miaka 17 iliyopita ambapo tarehe 21 Februari 2001, Mtakatifu Yohane Paulo II alimteua Karidinali wa Jimbo Kuu la Buenos Aires nchini Argentina,  Askofu Mkuu Mario Bergoglio  akiwa na umri wa miaka 64. Wakati wa uteuzi huo Askofu Mkuu alikuwa tayari ameongoza hata shirika la Wajesuit huko Argentina na zaidi ni mtoto wa wahamiaj kutoka mkoa wa Piemonte nchini  Italia mahali ambapo wazazi wake walihamia  Argentina.

Mario Bergoglio,alizaliwa katika mji wa Argentina tarehe 17 Desemba 1936, na wakati wa kuchaguliwa kwake  kuwa papa akachukua jina la Francisco, tarehe 13 Machi 2013. Kuchaguliwa kwake ulichukua nafasi ya 266 ya papa wa Kanisa Katoliki tangu Mtume wa kwanza wa Kanisa Mtakatifu Petro. Ni papa wa kwanza kutoka katika Shirika la Yesu liitwalo Jesuit na papa wa kwanza kutoka bara la Marekani, na kama alivyojielezea kati ya maneno yake ya kwanza mara baada ya kuchaguliwa kuwa “ametoka mwisho wa dunia”! 

Ili kuweza kupta ufahamu zaidi hasa wasomaji wetu katika mitandao ya kijamii: utume wa papa Francisko katika mji mkuu wa Aregentina, kabla ya kuanza uchaguzi ambao baada ye akachaguliwa kuwa Papa kwa jina la Francisko, na  kuagana na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedkito XVI, picha zinapatikana katika video kwenye mtandao wa :

http://www.lastampa.it/2018/02/21/multimedia/vaticaninsider/ita/il-febbraio-jorge-mario-bergoglio-diventava-cardinale-RCKpmAbrf3Tg5JqVRyT99M/pagina.html

Sr Angela Rwezaula

Vatican News

 








All the contents on this site are copyrighted ©.