2018-02-21 08:55:00

Barua ya Askofu D.Battaglia kwa Vijana! Mapambazuko mapya!


"Ndugu vijana, Barua hii ni kwa ajili ya jumuiya nzima lakini kwa namna ya pekee ninawalekeza ninyi ambao ni moyo na uwepo wenu leo na kesho. Baba Mtakatifu Francisko wakati wa hotuba yake katika mkutano wa Kanisa huko  Firenze aliwambia vijana wenye nguvu na ujasiri kuwa “ msitazame maisha mkiwa juu ya baraza, bali fanyeni  jitihada na kujikita kwa mapana katika masuala ya maisha ya kijamii na kisisa. Mikono yenu  yenye imani  iamshwe juu mbinguni”. Uwepo wenu ni wa thamani na unabii wa safari ambayo inawasubiri kila siku, lakini kwa pamoja”. Huo ni utangulizi wa Barua ya kichungaji ya kwaresima mwaka 2018 ya Askofu Domenico Battaglia wa Jimbo la Cerreto Sannita-Telese-Sant'Agata de' Goti nchini Italia wenye kauli mbiu “ni kujifunika usiku wakati ukisubiri  machweo ya jua” barua ambayo amejikita kuwazama  vijana kwa karibu sana  ili kuwapa mwelekeo wa maisha hasa katika kipindi hiki cha kwaresima na daima. 

Akiendelea na tafakari hiyo ujumbe wake  unasema,upendo unaoishi kwetu na  katika jumuiya zetu, uwe kama upendo wenye uwezo wa kutazama mwingine, kumpokea maskini, kuita jina kwa jambo lolote lisilo la haki, kuwa na huruma, lakini pia kijana anahitaji kutafuta njia ya wakati uliopo, katika matatizo yake, hata  kama yapo masuala ya kuchelewa na sintofahamu za kijamii. Upendo ambao unatumaini ni upendo  unao amini katika uwezo wa mabadiliko, uongofu wa mioyo na safari ambayo inawahusisha wote kwa mantiki ya kuishi binafsi hata kushirikisha wengine.

Vijana ambao wanatafuta na kuomba wanahitaji kujua maana ya kuwajibika:Ni shauku kwa watu wazima kuona wanataka kujenga wakati endelevu na kuwa wajasiri daima wa kwenda zaidi ya; kuamini katika mwanadamu ambaye amependwa na Mungu na ametaka kumjenga na kumpatia wokovu; kuwa na matumaini kwa mwanadamu na katika umoja wa kindugu; kumpokea Mungu katika ukaribu na yule anayeishi katika hali ya umaskini,pia wa mwisho katika ardhi yetu. Kutumaini maana yake si kuachana na hali halisi inayokukabili ya  wakati uliopo bali ni kuwepo na kusimama kidete katika ardhi hii; kuwajibika kwa jitihada zote na  ujasiri; si kuamini katika mantiki za wenye kutaka madaraka na ubaguzi; si kuamini utofauti au kutaka kujiachia bali ni kuwa na akili na busara ya kutaka  kujenga kwa njia ya zana tulizo nazo, tuliozokabidhiwa japokuwa zinabadilika kila wakati!

Vijana,sura zenu na majeraha mliyo nayo yanakumbusha mengi zaidi! Ni mengi zaidi kwa yule anayetambua kwenda zaidi ya upeo, anayetambua kukaa kimya na  kuacha masengenyo yenye kuleta utupu ndani ya mioyo,majivuno na kujionesha. Kwa njia hiyo ni muhimu kuwa na utambuzi zaidi ya kwamba mbele ya mambo hayo kuna jambo kuu msingi lipitalo yote ! Katika dunia ambayo utafikiri ni ndoto za utaalam wa teknolojia isiyo na  uwezo wa kuendeleza maendeleo ya kweli ya binadamu, bali kuamini katika dunia inayotaka kuendelea kuwa na kiu ndani ya mioyo yetu, kiu ya uhuru, kiu ya mahitaji  ya mahusiano ya kweli. Vijana mnayo thamani kubwa zaidi ya kile ukipendacho  kupokea. Muda wenu ni wenye thamani zaidi ya kubadilisha tabasamu na macho yanayo kutana yana thamani zaidi ya maneno mengi. Vijana wawe na ujasiri wa kuamini kama alivyo fanya Yesu; wa kutumaini na kupenda kama alivyo fanya yeye!

Askofu Domeniko akitazama juu ya  Injili ya Jumapili ya kwanza ya Kwaresima anasema; Injili ya  Mtakatifu Marko, anaonesha mwanzo kuwa, Yesu akisukumwa  na Roho Mtakatifu katika jangwa, kwa siku 40 na ambaye baadaye alijaribiwa; tofauti na Injili nyingine mbili zinazofanana, Matayo na Luka ambao wanaonesha majaribu hayo mwishoni, mara baada ya Yesu kumalizia kipindi chake cha kusali na kufunga  na mwisho anaona njaa. Askofu Domenico anafafanua kuwa,kishawishi ni kile cha kusema, iwapo unao uwezo, kwanini usifanya mawe yawe mkate, ikiwa na maana ya kwamba majaribu hayo  yanamtokea hata mwanadamu kama ifiatavyo: kama una uwezo, kama unayo nafasi nzuri ya uwajibikaji unaweza kupata fursa, fanya haraka kwa ajili yako na kwa ajili ya wengine, marafiki, hata wale ambao labda wanakudai. Kama unayo kazi, fikiria kuikumbatia na  kuwashibisha ndugu zako tu na kujali vema kazi yako hata kwa gharama ya kunyonya ngozi ya watu wengine, hata kwa gharama ya kutumia uwezo wa wengine na kudanganya. Achilia mbali  janga la wasio kuwa na kitu, wahitaji, nyanyasa na hata umaskini! 

Jibu la Yesu  lakini katika  majaribu hayo anaweka bayana  jinsi gani ya kufunga katika jangwa,ikiwa na maana, ni kushirikishana hali halisi ya maisha: kifunga udanyanyifu, ufisadi, kupata vya bure, kuiba nafasi za bure, kupendelea nafasi za kwanza, kutaka kutambuliwa,ukahaba, ubatili, na ubinafsi. Kufunga siyo tu kwa yale mambo yaliyo mengi, bali ni kwa ajili ya kuweza kushirikishana na wengine kile ambacho hao wengine hawana.

Imani aliyoishi Yesu leo hii inatupatia nguvu mpya ya kuishi imani hiyo kwa ujasiri,  hasa wito katika uongofu.Ufalme wa Mungu ukaribu, tubuni na kuamini Injili. Kuamini injili ya ya kuwa, Ufalme wa Mungu hauwezi kamwe kupitia katika mantiki ya kutaka kuwa na uwezo, kupitia kwa wenye ulaghai, utajiri, bali ufalme wa Mungu unao uwezo wa kuamsha dhamiri zetu zenye uvuguvugu. Ukaribu wa Mungu ni kwa njia ya Yesu anayeshikamana na binadamu hadi mwisho, akajifanya mtu katika hali ya mtu kwa ajili ya wote.

Umoja wa Mungu na watu ambao utafuta kulinda wema wa pamoja ni mantiki ya kutambua wema wa kweli ambao unajenga ubinadamu, ukaribu na kupendelea hali halisi ya wadhaifu. Iwapo sisi hatuwezi kugeuza mawe kuwa mkate, halikadhalika  na Yesu mwenyewe hawezi kufanya hivyo.
Katika jangwa Yesu kwa hakika alifanya maamuzi na mtindo wa utume wake kwa  watu ambao wanasubiri masiha mwenye nguvu ambaye anaweza kufanya kile ambacho kila mtu anataka. Alikabidhi maisha yake ili wengine waweze kuishi na kuamini kuwa umoja katika nchi hii unawezakana! Nini maana ya imani kama siyo ujasiri wa kugeuka na kupata uongofu  kwa ajili ya kilio cha binadamu? Na ndiyo maana ya kufunga kwa  maana ya kutambea; ndiyo matumaini ya wito kwa wengi kama ndugu kaka wa baba mmoja.

Askofu Dominco Bataglia katika barua yake ya kichungaji  anaandikia kuwa, vijana wanatambue zaidi mipango isiyo kuwa na kichwa wala kiuno, maneno matupu yasiyo kuwa na msingi na wala ya dhati, wanatambua nafsi  kubwa ya mawasililiano ambayo yamejaa upweke, wakati huo huo kuwa yenye nguvu. Lakini udhaifi huo unawaweza kugeuka kuwa fursa, njaa ya haki inaweza kugueka kuwa nafasi ya kutangaza ufufuko , kwa ajili yao na hata jumuiya kwa ujumla. Kutokana na hili, kipindi cha kwaresima Askofu Domeniko anapenda Vijana wakae kidete na kutafakari kwa pamoja. Kutafuta ukweli, njia za haki kwa wema na kwa ajili ya wema wa dunia. Rasilimali ya kweli ni zile za kujikomboa binafsi  na kukomboa wengine kwa njia ya  uwajibikaji. Vijana ni mashuhuda wa kweli wa maisha yao; kwa maana hiyo  safari si kwa ajili ya kufika ukiwa wa kwanza, bali ni  kutambea na kufika kwa pamoja katika safari hiyo.

Maisha mara nyingi  yanatoa mshangao, anasema askofu, maana daima  kuna haja ya kunyosha mikono na kutoa, kuanguka, kuamka na kutia moyo; ndiyo hali halisi na uzoefu wa maisha . Hili ni kutokana na maskini wa kukithiri ambao wanajua  kufundisha na kufanya tufikiri ndani ya mioyo yetu ,wakati mwingine kwa kujificha pembeni kusubiri au kushirikiana wakati wa kusubiri mabadiliko. Ni lazima kujikita katika kutafakari shauku hiyo kwa lengo mahsusi. Kukutana na mitazamo, kukutanisha mikono, miguu isiyosimama kamwe ya kukimbia ili kushirikishana hatua na kuanza tena kwa pamoja. Siyo mipango mikubwa yenye kuleta ubora wa hatua ya maendeleo anasema Askofu Domenico,bali ni muda kupita taratibu ndiyo unaweza kugundua kuwa upendo tayari upo katika maisha, hasa zaidi kwa maskini na wa mwisho. Kutembea kwa pamoja ndiyo ugeuka kuwa fursa ili kuwapa pumzi wenye kuwa na dhamiri ya kujifungia binafsi. Kujitoa binafasi, urafiki, upendo ushirikiano ni vitu ambavyo vina miguu ya kutembea ili kufika mbele na nguvu ya kukumbusha nini maana ya kuishi katika ardhi hii.

Amewataka vijana kujikita katika wajibu huo katika kipindi cha kwaresima ili kujiandaa vyema kusherehekee sikukuu ya Pasaka ya Yesu, kwani imani inatoa pumzi ya ujasiri wa kukabiliana na changamoto kusimama karibu na mwenzako ili kutembea kwa pamoja hatua kwa hatua bila kumwacha hata mmoja nyuma. Wawe kama walinzi wangojeavyo asubuhi na dipo nuru yao  itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yao itatokea mara; na haki yao itakutangulia; utukufu wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde. (Is 58,8).

Ni wakati wa usiku wa kwenda katika kaburi la kushindwa kwetu na kukata tamaa, lakini ni vizuri wakati wa usiku kwasababu ni vizuri kusubiri mapambazuko ya jua. Ni kujifunika wakati wa usiku ukisubiri machweo ya asubuhi. Hata Mtakatifu Yohane mbatizaji alikuwa amesema mimi siyo nuru. Iwapo sisi ni wakweli binafsi, kwa wengine na kwa Bwana, tutaona mahali penye kuokea mwanga , mahali ambapo machweo ya jua yanachomoza. Na hapo ndipo patakuwapo neema . Kwa matumaini hayo, ni kusubiri pamoja mbele ya kaburi wazi. Maana pale tutaona hata wengine kwa macho yao, tutatazama asili yake, kuona machwo yake yakichomoza kutoka  katika giza, na ndipo palipo matumaini yao ya  leo na daima.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.