2018-02-17 17:05:00

Papa Francisko amekutana na Jumuiya ya Seminari ya Kipapa Kanda ya Sardegna


Ninawakaribisheni mkiwa katika maadhimisho ya kumbukumbu  ya miaka 90 tangu kuanzishwa kwa Seminari ya Kipapa ya Kanda ya Sardegna. Ni kwa matashi i ya Papa Pio XI, kusikiliza mapendekezo ya Maaskofu wa Italia, kwa namana ya pekee wa Kusini  na katika Visiwa, kukubaliana juu ya kuweka Seminari, na mwisho wake kuwasadia mafunzo maaspiranti katika mchakato mzima wa kuwa makuhani. Katika Kanda yenu Seminari ya kwanza ilikuwa huko Guglieri, ikiwa pamoja ni Chuo cha Kitaalimungu;  baadaye ikahamishwa katika makao makuu. Nawasalimieni nyote kuanzia na Askofu Mkuu  Arrigo Miglio wa Jimbo Kuu la Cagliari na kumshukuru kwa hotuba yake. Ni maelezo ya utanguliz wa Hotuba ya Baba Mtakatifu ya tarehe 17 Februari 2018 alipokuwatana na waseminari na walimu wao  na maaskofu kutoka Sardegna kisiwani kusini mwa Italia mjini Vatican wakiwa wanafanya kukumbukumbu ya miaka 90 Tangu kuanzishwa kwa seminari ya kipapa hiyo.

Katika tukio hilo, Baba Mtakatifu anapenda kumshukuru Bwana kwa miaka yote hiyo aliyoweza kuwasindikiza maisha ya makuhani  walimu katika taasisi muhimu ya elimu, katika seminari hiyo unayo julikana kwa jina la Moyo Mtakatifu wa Yesu. Seminari hiyo imetoa makuhani wengi katika Kanisa ambao wanajikita kutoa huduma ya  Kanisa mahalia , utumae wa watu ( ad gentes) na katika kutoa  huduma mbalimbali za Kanisa la Ulimwengu. Tukio hili linaweza kuwa ni kumbukumba ya kuweza kutoa chachu hasa katika uchungaji wa miito mipya. Na kwa  mafunzo mapaya ya kuweza  kuwasaidia makandidati wanaoomba  daraja Takatifu kwa ajili ya wema wa watu.

Baba Mtakatifu akiwalenga hasa wasemaninari amesema wapo wanajiandaa ili waweze kuwa wafanyakazi katika shamba la Bwana , padre anaye tambua kifanya kazi kwa umoja na kati ya majimbo tofauti. Hiyo ni aina ya tunu na sababu msingi kama kisiwa cha Sardenga ambacho kina utajiri mkubwa wa imani na utamanduni wa dini kikristo ambayo kwa namna ya pekee ni sababu ya kuhitaji uchungaji wa mahusiano kati ya jumuiya tofauti za majimbo. Umaskini wa vitu na kiroho leo hii ni muhimu na ambalo daima limekuwa kikitiliwa mkazo ili  wachungaii wawe makini kuwajali maskini; wawe wenye uwezo wa kukaa nao , kwa mtindo rahisi ili maskini waonje kuwa makanisa yetu ndiyo  nyumba yao ya kwanza. Baba Mtakatifu anawatia moyo ili wajiandae,tangu sasa kuwa mapadre wa watu na kwa ajili ya watu, “wala si kama wajifanyao mabwana juu ya mitaa yao, bali kwa kujifanya vielelezo kwa lile kundi,(taz 1Pt 5,3) kama Mtakatifu Petro katika barua yake asemavyo.

 Katika kipindi hiki cha kujiandaa na daraja takatifu ni kuishi kipindi maalumu na ambacho hakitarudia katika maisha yao. Wanaweza kuwa daima na utambuzi wa neema ya Bwana aliyewajalia katika wito huo wa kuacha kila kitu kumfuata na kuishi naye na ili  kuweza kutumwa kutangaza Neno (taz Mt 4,19-20; Mc 3,14). Waseminari ni majibu ya matumaini ya Kanisa hata la Sardegan! Maaskofu wao wanawafuatilia kwa upendo na shauku, wakiwategemea sana hata katika  mapendekezo ya mafunzo ya Yesu mchungaji mwema kwa ajili ya wema na utakatifu wa jumuiya ya kikristo katika kanda yao. Watembee kwa furaha na shauku , wawe makini katika mchakato mzima wa mafunzo yote, ili baadaye wapate kuwajibika katika maisha ya kitume na kutambua kujibu dharura za leo hii za uinjilishaji.

Seminari kabla na zaidi ya kuwa taasisi ya shughuli ya kupata ujuzi wa kitaalimungu, kichungaji na mahali ambapo maisha ya pamoja na mafunzo, ni mahali pa uzoefu wa kweli wa Kanisa,ni jumuiya moja ya mitume wamisionari, wanaoitwa kufuata kwa karibu Bwana Yesu , kukaa naye usiku na mchana, kushirikiana katika fumbo la msalaba na ufufuko wake, kujikita katika Neno na Roho kukua na kujifunza  mambo maalum yanayohusu nini maana ya kuwa mfuasi wa kitume. Tangu sasa maandalizi yao makini yanachukua nafasi kuu ya uchaguzi huru;  ambayo inahitaji uamaninfu kabisa wa Kristo, katika Kanisa, wito wao na utume.

Katika njia ya safari ya Seminari yapo mang’amuzi katika nafasi ya walimu: Baba Mtakatifu akiendelea na ufafanuzia anasisitiza kuwa,ubora wa mapadre unategemea sehemu kubwa na juhudi za wahusika katika mafunzo. Wao wanaalikwa kuwa  makini, kuongozwa na hekima kwa ajili ya maendeleo ya mtu  hasa mwenedendo na tabia njema yenye uwezo wa kuchukua majukumu msingi  binafsi ambayo itawasadia  baadaye waweze kuchukua  wajibu na utekelezaji  wa utume kikuhani. Katika kazi hiyo nyeti ya mafunzo, Baba Mtakatifu anabainsiha kuwa  hata seminari yao inajikita katika huduma muhimu ya Majimbo kwa kuwasaidia kutoa mafunzo bora kwa ajili ya makleri na umoja  kati ya Makanisa. 

Amemalizia Baba Mtakatifu akiwawakabidhi kwa ulinzi wa Mama Yetu wa Bonaria. Kwa hakika anasema kipindi cha seminari ni wakati mwafaka, mahali ambapo uzoefu huuo wa upendo wa Mama Maria katika maisha yao upo.Yeye anakesha kwa upendo wa umama kwa kila mmoja wao , na hivyo kwake yeye daima wamkimbilie kwa matumaini. Amewahakikishia maombi yake na kuwabariki wote!

Na Sr Angela Rwezaula
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.