2018-02-15 08:51:00

Monsinyo Dario Vigano kuhutubia katika Chuo Kikuu cha Monterrey Mexco!


Tarehe 13 februari 2018 Monsinyo Dario Vigano  Mwenyekiti wa Sekreterieti ya Mawasilino Vatican, ametoa hotuba yake katika Chuo Kikuu cha Sanaa Takatifu huko Monterrey nchini Mexico, hotuba  hio ilikuwa na  mada ya  “ Uso wa Yesu katika sinema: historia na namna ya mitindo ya kuelezea. Katika mada hiyo amepata kutafakari kwa kina kuhus mwanga na giza, vitu viwili ambavyo vinakwenda daima pamoja japokuwa katika njia tofauti, na hasa katika kuelezea aina na mitindo ya sinema.

Ni kwa mara yake ya kwanza kuhutubia katika Chuo Kikuu cha Sanaa Takatifu huko Monterrey Mexco na hivyo hotuba yake imelenga hasa kuelezea kwa ufasaha mtindo wa sanaa ya sinema kama sehemu mwafaka kwa ajili ya kusaidia wengi ambao wanaanza njia ya kumtafuta Mungu hasa kuanzia kitovu cha sura ya Yesu Kristo. Katika kuelezea kwa ufasaha, ameweza kuwataja watu maalufu katika kutengneza picha kama vile Auguste na Louis Lumière ambao walitengeneza sinema inayowakilisha picha ya Pasaka Takatifu kwa mwaka 1897 ; Padre  Georges Méliès aliyetengeneza picha ya kolossal “ mfalme wa wafalme” na Cecil B. De Mille, mtazamo wa watu  ambayo ni ilikuwa ni “ historia kubwa ambayo haijawahi kusimuliwa” ya George Stevens, na nyingine picha ya Jesus Super Star na wengine wengi.

Monsinyo Vigano anasema, ina maana ya kwamba historia ya picha za Kristo imekuwa inaunda maswali na wasiwasi katika utamaduni, taaluma mbalimbali kwa kila nyakati katika historia. Kwa maana hiyo amesititiza zaidi kwa namna ya pekee katika picha kutoka katika Injili ya Mtakatifu Matayo, iliyotengenezwa na Paulo Pasolini mwaka 1964  ambayo inakwenda sambamba na picha ya Yesu wa Nazareti picha iliyotengenezwa na Franco Zeffirelli mwaka 1976  ambayo kwa hakika inafuata barabara na kulelezea  historia ya Yesu kutoka katika maandishi matakatifu. Kwa mujibu wa Injili ya Matayo, Pasolini alimetaka kuigiza wafuasi wa Yesu kwa namna ya pekee Mtakatifu Yohane.

Na kwa maana hiyo katika machakato mzima wa safari ya mateso ya Yesu, wote tunahusika na kuchanganyikana katika umati mkubwa , kwa wote wanaotazama na kusiliza lakini hawatambui, na pia kutokuwa na uwezo wa kuokea pamoja na kutaka jibu la tukio hilo. Na katika Picha ya Pasolini, Monsinyo Vignao anafafanua, kuwa  Pasolini alichagua  jambo lakutoonyesha kifo cha Kristo. Pamoja na kwamba alionesha vema kila aina ya andiko la kitaalimungu, na kwamba kifo cha Yesu na utii kwa Baba yeke,  upendo upeo kwa kila binadamu ni kiini cha historia ya binadamu , ambaye hawezi  kukubali kutazama mateso makali hayo; hasa kifo cha msalabani, na hiivyo tukio sehemu ya kuonesha utukufu wa Mungu unahitaji usikivu , na ndiyo maana katika picha , ikifikia saa ya kufa, inaonesha giza tu.

Pamoja na hayo hayo picha ya Yesu wa Nazareti kwa mujbu wa Franco Zefferelli,amejitahidi na namna ya pekee kuoanesha uasili wa maandiko mataaktifu ya Injili , na zaidi anaonesha juu ya nguvu zinazotumiwa na wenye madaraka, kutokana na sehemu za mateso ya Yesu kuoigwa mijeredi, mazungumzo ya Pilato, wasaidizi wake masawali ya Pilato yenye kiburi, maaskari wanavyo buruza Yesu . Lakini kwa upande wa Yesu anaonesha unyenyekevu ambao ni mwanga wa mwana kondoo aliyetolewa sadaka , lakini ambaye tayari ni mfufuka.

Mosinyo Vigano amemalizia akisema kuwa ,uwezo wa kusoma vurugu za kutumia nguvu katika mateso, imekuwa ni ufunguo wa kusoma matukio mengi kwa kila eneo ambapo vurugu za utawala zimekuwa zikijirudia mara kwa mara na kuwa vigumu hata kukabiliana nazo!

Sr Angela Rwezaula
Vatican News

 
All the contents on this site are copyrighted ©.