2018-02-15 16:43:00

Misa katika Kanisa Kuu la Mt. Petro kwa wanajeshi 7000 wa Italia !


Tarehe 15 Februari 2018 Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican, ameadhimisha misa kwa Wanajeshi 7000 kutoka Italia katika Kaburi la Mtakatifu Yohane XXIII ambaye ni msimamzi wa Jeshi la Italia asubuhi saa 3 kamili masaa ya Ulaya Katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.
 
Katika mahubiri yake, Kardinali parolin anasema wamekuja kama mahujaji katika Kaburi la Mtakatifu Yohane XXIII, wakitaka kuomba kwa ajili ya Kanisa la Italia, kujiombe wenyewe na  kwa ajili ya ulimwengu zawadi ya amani, ambayo moyo wa mtakatifu huyo alikuwa kwa shauku kubwa  akipenda na ambaye hata leo hii angependa kuwakabidhi kazi hiyo  wanajeshi wa Italia.

Ni ndani ya kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mahali ambapo wanaweza kusema ndiyo ilikuwa nyumba ya Angelo Giusseppe Roncalli, yaani jina la ubatizo la Papa Yohane XXIII. Ni katika eneo hilo kwa dhati alikuwa akipaza sauti kwa nguvu juu ya amani, ili iweze kuwafikia watu wote duniani wenye mapenzi mema, kila kiumbe na kila imani.

Amani ndiyo ilikuwa inawakilisha sehemu kubwa ya hotuba zake, mahubiri yake na ndiyo ulikuwa ujumbe wake kwa kila tendo na ishara aliyo ichagua ya kichungaji, katika uwezo wake wa ufanya mahusiano na mtindo wa kutengeneza urafiki kati ya watu.
Amani imebaki katika maandiko yake ya mwisho wakati wa maisha yake kwa Waraka wa Pacem in Terris yaani amani kwa mataifa, waraka ambao hadi sasa haupotezi thamani yake na unaendelea kuwa muhimu katika hali halisi ya sasa.

Kwa mtazamo wa Mafunzo jamii ya Kanisa, amani siyo jambo rahisi na kusema bila kuwa na vita, hata usawa kati ya nguvu na mpizani, bali amani inajikita katika kutafuta ukweli wa mantiki ya binadamu na kutaka kuweka sawa mambo kwa mujibu wa kazi ya haki ambayo ni amani; na mazao ya haki yawe ni utulivu na matumaini daima. (Taz Gaudium et spes, 78; Centesimus annus, 51; Is 32,17).

Akielezea juu ya utume wao kama wanajeshi, amesema wao wanalinda kwa namna  nyingi na njia mbalimbali wakimbizi ambao kwa sababu ya vita na ukosefu wa maendeleo, watu hao wanazidi kufika wengi kutoka katika mataifa mbalimbali ya dunia. Kama wanajeshi wanajikitia katika kuokoa maisha mengi ya binadamu ambaye anazidi kukataliwa haki msingi na wakati mwingine vizingiti vya ukiritimba wa ruhusa na mikataba mbalimbali za kimataifa.

Wao wanajikita katika nafsi nyeti ambayo inatazama kati ya utume wa kimataifa , mahali ambao wao wanawakilisha wanajeshi wenzao katika mataifa mengi chini ushirikiano wa kimataifa na kupeleka mbele huduma kwa namna ya pekee , huduma hiyo ni ngumu ya hatari ambayo wakati mwingine ni kutoa sadaka ya maisha.

Kwa njia hiyo katika altrare ya Bwana  wawakumbuke hata ndugu wengi wanajeshi waliopoteza maisha yao  wakiwa katika utume na kwa ajili ya wao wenyewe. Kardinali Parolini anasema, jumuiya nzima inatambua kwa dhati  hali halisi ya uwajibikaji wao na huduma yao kwa ujasiri wakitoa ushuhuda halisi. Huduma yao ni yenye thamani kubwa katika kukabiliana kila siku matatizo na kutazama kwa matumaini na imani wakati ujao.

Katika Injili ya siku, Yesu anasema “kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha. (Lc 9,24)” Hivyo  Kardinali anathibitisha kuwa, kuchagua maisha maana yake ni kulinda maisha ya kila binadamu kama jinsi walivyoitwa kutenda, hasa kisaidia mahali palipo na vurugu na nguvu, chuki unyanyasaji, vita, njaa, ubaguzi na sintofahamu. Kuchagua maisha maana yake ni kutimiza  wajibu kwa ajili ya wema wa haki na kwa ajili ya amani ili kuwafanya wadhaifu wakwezwe juu kutoka mikononi mwa wenye nguvu na  hata kama ni lazima kutoa sadaka binafsi kwa ajili ya kuwalinda na kuwatetea wengine! Siyo kazi rahisi maana inahitaji ujasiri na zaidi shauku ya kukua kila siku kiroho katika mantiki ya kujitoa binafsi, na ili mantiki hiyo iweze kutambuliwa na yenye  thamani katika ulimwengu ambao unazidi kumilikiwa na ubinafsi, kwa bahati nzuri lakini kitovu ni ujumbe wa Injili amesema Kardinali Parolin.

Katika hatua hiyo, basi Kardinali anawashauri wazidi  kweli kuongozwa na Injili na kwa njia ya ulinzi wa msimamizi  wao Mtakatifu Yohane XXIII ambaye ni mfano hai. Yeye alitambua kuunganisha upendo wa kibaba na upendo wa amani, alitambua kutetea kwa njia ya mzizi ya imani, kupanda ile sanaa ya mshikamano kati ya tamaduni na dini, alitambua kuwa matumaini na kutunza kila aina ya udogo wa mtu wakati huo huo kuwasikiliza hata wakubwa  na wakuu wa mataifa.

Sr Angela Rwezula 
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.