Kwa mujibu wa mwandaaji mkuu wa Liturujia za Vatican, Monsinyo Guido Marini ametoa
Kalenda ya maadhimisho ya Baba Mtakatifu Francisko kwa mwezi Machi na Aprili 2018.Tarehe
9 Machi saa 11 jioni masaa ya Ulaya Baba Mtakatifu ataadhimisha liturujia ya kitubio
katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Jumamosi 17 Machi, Baba Mtakatifu atafanya ziara
yake fupi ya kichungaji kwenda huko Mtakatifu Giovanni Rotondo.
Jumapili tarehe 25 machi,Baba Mtakatifu ataadhimisha misa katika siku ya Jumapili ya Matawi na mwanzo wa mateso ya Bwana wetu Yesu Kristo katika uwanja wa Mtakatifu Petro saa 4 asubuhi masaa ya Ulaya. Alhamisi Tarehe 29 Machi saa 3.30 ataadhimisha Karamu ya mwisho na kubariki mafuta Matakatifu ya Krisma.
Tarehe 30 Machi Ijumaa Kuu saa 11 jioni, masaa ya Ulaya Baba Mtakatifu anataadhimisha
ibada ya mateso ya Bwana wetu Yesu Kristo , katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro
na usiku saa 3.15 ataongoza maadhimisho ya njia ya msalaba kuzunguka Magofu ya Colosseo.
Jumamosi Kuu tarehe 31 Machi, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro saa 2.30 za usiku
masaa ya Ulaya Baba Mtakatifu ataanza mkesha wa Pasaka na kufuatia misa ya Pasaka
ya Bwana.
Tarehe 1 Aprili ni Jumapili ya Pasaka. Katika uwanja wa Mtakatifu Petro saa 4 kamili
masaa ya Ulaya, Baba Mtakatifu anataongoza misa ya Sikukuu ya pasaka na saa sita
kamili kufuatia Baraka ya “Urbi et Orbi”
Domenika ya Pili ya Pasaka, tarehe 8 Aprili saa 4.30 masaa ya Ulaya, Baba Mtakatifu
ataadhimisha misa Takatifu ikiwa ni sikukuu ya huruma ya Mungu, ambapo itakuwa ni
fursa ya wamisionari wa huruma kukutana na Baba Mtakatifu Francisko.
Sr Angela Rwezaula
Vatican News
All the contents on this site are copyrighted ©. |