2018-02-13 15:44:00

Papa Francisko:inahitaji ujasiri kufichua wanafiki wa biashara ya watumwa!


Tarehe 8 Februari, 2015 iliwekwa kuwa siku ya sala na uhamasishaji kimataifa kuhusu swala la biashara haramu ya watumwa inayokwenda sabamba na sikukuu ya Mtakatifu Bakhita. Baraza la Kipapa la haki na amani kwa wakati ule kwa kushirikiana na umoja wa Wakuu wa mashirika ya kitawa ulimwenguni, wamekuwa daima wakiwaalika waamini na wenye mapenzi mema  ulimwenguni kote kusali na kuhamasisha jamii juu ya tatizo sugu la utumiaji wa watu kama vyombo vya kujipatia mapato. Kutokana na hilo  Baba Mtakatifu anasema, "siku zilizopita niliona katika gazeti kichwa cha habari katika mji ndogo wa Italia: miji hii ni mahali ambapo wabakaji mwaka huu ni  asilimia 40% ya wahamiaji. Hii ni njia ya kuchafua jina la wahamiaji ! Lakini bado asilimia 60% Je, walikuwa ni akina nani ? waitalia! hivyo  kuna aina ya kuwasilisha mambo ambayo hubadili ukweli".

Tarehe 12 Februari Papa Francisko wakati akibadilishana mawazo kwa baadhi wa washiriki wa Mkutano ya Siku ya Dunia ya kutafakari juu ya kudhibiti biashara haramu ya utumwa Mjini Vatican ameyaeleza hayo akiwa na masikitiko makubwa mno!. Wakati akijibu maswali  mengi, mada nyingi amegusia kwa uchungu mkubwa na kwa wazi kuanzia unyanyasaji kijinsia,uonevu,shule za picha mbaya katika mitandao, eutanasia zilizojificha, wazee wanao achwa pweke kwa kusingizia vituo vya kutunzia wazee, unafiki, sintofahamu na mengine.

Papa Francisko hata hivyo anashutumu, "unafiki" unaozunguka wa usafirishaji wa watu ambao hutumiwa kama watumwa, kuwafanyisha kazi ya ukahaba wasichana. Pia amtoa shukrani kubwa kwa parokia nyingi na nyumba za kitawa ambazo ziliitikia wito wake wa kufungua milango kwa wahamiaji. Amendelea jibu maswali mengi kutoka kikundi zaidi ya vijana 100 na washiriki wa vyama mbalimbali vya nchi tofauti vya kitume, kati yao wakiwemo wahamiaji ambao nyakati zilipopita wamekuwa waathirika wa unyanyasaji, ambao kwa sasa wanajikita kushiriki katika juhudi zinazohusiana kuthibiti utumwa mambo leo.

Wiki iliyopitia alikuwa ameshutumu vikali hali hiyo alipokutana na kikundi cha Mtakatif Martha Kimataifa, Taasisi dhidi ya biashara haramu ya binadamu iliyoanzishwa mwaka 2014 na Baraza la Maaskofu wa Uingereza na Galles kutokana na ukweli kwamba jamii nyingi inaonekana wakati mwingine kutia moyo na kuhimiza unyanyasaji wa kijinsia na kwa mjia hiyo shughuli ya Taasisi ni kujikita kikalifu kudhibiti.

Baba Mtakatifu amesema,wakati mwingine, wahamiaji wanachafuliwa na kashfa nyingi. Kwa maana kuna aina ya kuwasilisha mambo ambayo yanabaidilisha ukweli. Na kama Kanisa lazima kuhamasisha na kuunda nafasi za makutano na  hiyo aliomba wafungue maparokia ili kupta kukutana na kukaribisha. Ni lazima kuwa na utambuzi wa kazi yao ambayo ni jibu la wito wake, hivyo anawashukuru wote waliotikia wito wake. Hizo ni pamoja na parokia nyingi, shule nyingi, nyumba za watawa nyingi ambao wamefungua milango hiyo na  anawatakia safri njema!

Amewaomba pia nao kutenda hivyo kwa ajili ya kuwafungulia wengine zaidi hasa wale ambao wamejaruhiwa hadhi yao. Anasisitiza wawe wahamasishaji katika maparokia yao ili parokia zipate kuwa na ukarimu, wasaidie Kanisa kutunza nafasi ya kushirikishana na kufanya uzoefu wa kushirikisha kwa imani na maisha. Kuhusu swala la biashara haramu ya watumwa, Baba Mtakatifu anasema kuna ujinga mkubwa sana. Hio inatokana hali ya kutokuwa na utashi wa kutambua matatizo yake na kutojali. Je ni kwanini, ni suala linalogusa wote kwa karibu katika dhamiri nyingi kwasababu ni ukoma, na sual a hilo linatufanya tuwe na aibu. Katika nchi ambayo inafanya hivyo au kutenda hivyo, haitaki kusikia mambo yanakuja katika mwanga na tatizo la biashara haramu ya watumwa inafichuliwa.

Wakati huo huo wapo watu ambao pamoja na utambuzi hawataki haya yasemwe maana wanapata kipato , wapo wafanya biashara ambao wanakodisha vijana kwa ajili ya kazi ya utumwa na wapo wengine wanatumia wasichana katika biashara ya unyanyasaji kinsia na ukahaba, kwa maana wanaporudi nyumbani kwa matajiri wao, lazima wapeleke faida ya siku. Na ndiyo maana watu wanaopenda kusafirisha,hawataki tatizo liwekwe wazi, hivyo inahitajika ujasiri!

Wapo hata wanafiki ambao utafikiri wanakabiliana kwa ngazi ya juu kuondoa  tatizo wakati huo huo wanashirikana katika kuongoza biashara hiyo ya utumwa na kuruhusu au kushirki katika unyanasaji kijinsia kwa wasichana, baba Mtakatifu kwa masikini anasema inasikitisha kuona hata unafiki ambao umejaa katika jamii. Katika njili inahukumu kwa nguvu zote juu ya unafiki, na hata yeye mara nyingi amekazia kwa viongozi wengi juu ya unafiki. Baba Mtakatifu anaongeza kuwa wapi ambao wanasura mbili. 

watu wambao wanazuia na kupambana wakati huo huo manazuia  matatizo hayo yasijitokeze katika mwanga na yaendelee. 
Ametoa mfano kwamba anamaliza sehemu ya mwisho ya gazeti la Vida Nueva, maana yake maisha mapya unayoeleza juu ya watoto wadogo wanaokuja nchini Hispania wakiwa peke yao na jinsi gani  wanapata mateso makubwa.  Vijana hawa wanafikia ili wawe huru na kufanya kazji japokuwa kulipwa sentí mbili na kama watumwa, wakati huo huo akitokeza mtu wa kuandika hayo, anapigwa vita na ksuhambuliwa badala ya kutazama  tatizo la kweli.

Vijana wana vinywa vilivyo wazi na  ambayo havina mfumo wa utumwa bado. Vijana hawana cha kupoteza kwasababu wanasema kile wanachofikiria na kusema , pamoja na kwamba ukweli wao unawatia katika matatizo makubwa. Kama watoto daima wanasema ukweli hadi kuwafanya wazazi wao waone aibu. Huo ni  uhuru wa vijana na watoto kusema mambo yalivyo.

Halikadalika amegusia matatizo makubwa ya vijana yanayowakumba katika mitandao ya kijamii, kwa utambuzi ya kwamba mitandao ya kijamii ndiyo nawfasi ya mawasiliano ya vijana. Lakini katika mtando ndipo wanakutana na majanga, kama ya picha mbaya, na hivyo amesema, ni uchaguzi wao kujua namna ya kukwepa tabia hiyo , yaani uchagua yaliyo mema au mabaya. Uchaguzi uko ndani ya roho zao, kwasababu bila kufanya hivyo matoke yake yatakuwa mabayasana, ni sawa na kupelekwa na maji au upepo ambao haushikiki, amesisitiza!

Akitazama mada ya wengine kuwekwa pembezon na hasa wazee amesema, wapo wengi waliobaguliwa na umaskini, wenye kuhitaji na wagonjwa. Leo hii watambue kuwa kuna ubaguzi watu kama wabaguavyo karatasi, au kama watoto anavyo chanachana karatasi , ni bora jambo hili lisisike kwasababu upungufu wa watu ni wa hatari sana. Wanabagua wazee, kwa kudai kuwapeleka katika vituo vya kupumzika, hakuna madawa au nusu ya madawa kitu ambacho kinaitwa eutanasia iliyojificha!

 Hakusahau kuwaonya vijana juu ya uonevu na ukatili , kudharau wengine katika mashule. Kwa masikitiko makubwa amesema katika shule zimefunguliwa katika matukio mabaya. Zipo tabia za kuwaonea wengine, kuwadharau wengine, maneno mabaya  na hivyo anasema, ni matatizo makubwa, hayo yanaingia katika sekta ya utumwa mambo leo!

Sr Angela Rwezaula
Vatican News !
All the contents on this site are copyrighted ©.