2018-02-02 15:24:00

Ujumbe wa Pariaki Hirarion kwa Jubilei ya dhahabu ya Jumuiya ya Mt. Egidio


“Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, katika nusu karne imeweza kugeuka  kuwa Jumuiya kubwa ya walei wanaunganisha maelfu na maelfu nchini Italia, katika nchi nyingine za Ulaya na ulimwengu mzima. Ni kama mbegu ndogo ya aradali inayotajwa katika Injili takatifu  na kugeuka kuwa mti mzuri sana;mahali ambapo matawi yake mengi yamezidi kusaidia wahitaji wengi duniani”

Haya ni maelezo ya Patriaki  Hilarion wa Volokolamsk na Mwenyekiti wa kitengo cha mahusiano na nchi za nje, mjini Moscow Urusi katika barua aliyo mtumia Bwana Andrea Riccardi mwanzilishi  wa Jumuiya hiyo na wanajumuiya nzima, katika fursa ya tukio la Jubilei ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwake. Patriaki Hilarion anakumbusha jinsi gani miaka mingi Jumuiya ya Mtakatifu Egidio inazidi kuendelea katika mahusiano mema na mshikamano wa Kanisa la Kiorthodox nchini Urusi,hata ushirikiano huo hawali ya yote unajikita katika matendo ya huduma ya upendo na ulinzi wa kazi za utamaduni katika jamii ya sasa.

Moja ya kipaumbele cha kwanza,anaongeza kusema, jumuiya imejikita katika kutafuta amani, akikumbuka juhudi hizo za kuwezesha hata  kufikia amani katika nchi ya Msumbiji Afrika, nchi ambayo iliteseka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Shughuli nyingine kubwa ya Jumuiya hiyo imekuwa ni mikutano ya  majadiliano  ya kidini na sala kwa ajili ya  amani, ikiwa pia kutazama watu wengi wenye shida, wakimbizi na wagonjwa mbalimbali katika jamii. Patriaki pia anakumbusha kuwa, kila mwaka ameweza kutuma wawakilishi wake katika mikutano na ushirikiano wa jumuiya hiyo na upatriaki wa Moscow umetoa matunda mengi katika mantiki ya majadiliano ya kiorthodox na wakatoliki hata kwa upande wa ushuhuda wa mawazo hasa ya kiinjili na vyama vingi vya kidini.

Ikumbukwe: kutokana na tukio la Sherehe za jubilei ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio,Misa Takatifu itafanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane Laterano Roma, Jumamosi tarehe 10 saa 11.30 jioni  masaa ya Ulaya Februari. Misa hiyo itaongozwa na Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican kwa ushirikiano na  Askofu Mkuu  Angelo De Donatis, Msaidizi wa Papa kwa ajili ya Jimbo la Roma, maaskofo 100  kutoka sehemu mbalimbali za dunia, mapadre  200, wanajumuiya, viongozi wa serikali na wawakilishi kutoka mataifa mbalimbali. 

Sr Angela Rwezaula
Vatican News

 
All the contents on this site are copyrighted ©.