2018-02-01 08:56:00

Ripoti ya Caritas Italia kuhusu njaa ya amani:chakula,ukosefu wa usawa na vita!


Ripoti ya Caritas nchini italia imetolewa mwishono mwa janauri 2018  ikiwa na kaulimbiu “Chakula kilichokataliwa” na kwamba kuna ongezeko kubwa la watu wa utapia mlo  hasa katika bara la Afrika. Kulingana na janga hilo ni wito kwa wote uli  kutazama na kuangalia namna ya kubadili mantiki za masoko, kwa  kuhakikisha haki ya chakula kwa kila mmoja.

Hata hivyo hata ripoti ya Umoja wa mataifa mwaka 2017 imedhihirisha kuwa utapia mlo kwa mara nyingine tena unazidi kuongezeka, kama vile vifo kutokana na njaa; inaonesha kuwa milioni 815 watu wamekumbwa na baa la njaa, kati yao ni watoto milioni 38  kulinganisha na mwaka uliotangulia, kwamba asilimia 23 % ni katika nchi za Afrika chini ya Jangwa la sahara.

Hivyo kutokana na ripoti hiyo , hata  sehemu kubwa ya janga inaoneshwa bayana na Caritas nchini Italia katika ripoti iliyotangaza tarehe 30 Januari 2018 ikiwa na kichwa cha habari “Chakula kilichokataliwa”, wakati wanafanya  kumbukumbu ya mwaka wa 70 tangu kuwawa kwa Ghandi. Mwalimu wa kiroho na maarufu katika utetezi wa  haki, usawa na amani ya watu.

Ripoti ya Caritas ina lengo la kuonyesha tofauti zinazoendelea kuashiria mfumo wa kiuchumi duniani na kufufua yale yaliyoripotiwa na kupendekezwa katika Kampeni “Familia moja ya kibinadamu, chakula kwa wote: ni kazi yetu", inayohamasishwa  na Makanisa duniani kote mnamo mwaka 2015. Kwa hiyo, ni muhimu kutilia mkazo hasa juu ya  sababu za haki yakukosekana kwa chakula na kuchunguza ili kupata ufumbuzi iwezekanavyo kwa mtamzamo kwa Afrika iliyoshambuliwa na migogoro na mvutano kuachangia watu wengi kuwa na njaa.

Ripoti hiyo pia inatazama  juu ya suala la haki ya chakula inayokwenda  sambamba na mada ya vurugu, na aina mpya za uchumi unaojikita katika utamaduni wa kibaguzi, na kusababisha ukosefu wa haki sawa za sayari hii. Na ndiyo maana ya umuhimu wa kuingilia katika hasa hata katika Mkutano wa Viongozi wa Afrika na huko Addis Sababa Ethiopia, ulio andaliwa na Fao.  Baba Mtakatifu katika fursa hiyo, pia ametuma ujumbe wake akitoa wito wa nguvuakiwataka mshikamano na ushirikiano kati ya nchi zota za Afrika na ili kuweza kukomboa watu wa Afrika katika hatari ya njaa, pia kuwapatia hadhi wanaume na wanawake, kuwahimiza hasa katika shughuli za kilimo, uzalishaji wa vyakula na hata kujikita katika mali za asili kwa njia ya mikakati na mipango ya hali ya juu.

Lakini hata hivyo Swali ambalo halijatatuliwa ni juu ya haki ya chakula ripoti inathibitisha, na kwamba inalinganishwa na suala la unyanyasaji na mifumo  ya kiuchumi inayotokanayo na utamaduni kubagua ambao unazidi kukuza uovu ndani ya mataifa na kimataifa. Kwa upande wa Afrika ya Mashariki kuanzia mwanzo wa mwaka 2017, mitandao ya Caritas inaendelea kujikita kusaidia zaidi ya watu milioni 3 na nusu  kwa zaidi ya mipango 120 katika nchi ya Ethiopia, Kenya, Somalia, Sud Sudan e Uganda kwa kiasi cha jumla ya Euro milioni 114 . Lakini pamoja na hatua muhimu za usalama wa chakula na upatikanaji wa maji, njia za kubadili mapambano inaendelea kupitia heshima, mazungumzo, suluhisho na kila aina yoyote ya azimio la amani  kama vile alivyokuwa anafundisha  Gandhi.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.