2018-01-30 14:34:00

Toleo jipya la Misale ya waumini itatolewa ikiwa na tafsiri ya Baba Yetu!


Toleo la Misale ya waumini ya Baraza la Maaskofu wa Italia ya  mwaka 2008 , itafanyiwa marekebisho kwa mara nyingine tena. Hayo ni maelezo kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Italia, Askofu Mkuu Nunzio Galantino wakati kuhitimisha Mkutano Mkuu wa Baraza hilo (Cei) na kusema kuwa, hata hivyo marekebisha katika kipengele cha sala ya Baba Yetu uliye mbinguni yalikuwa tayari yapo kwa toleo la 2008.

Katika Biblia  iliyokuwa imefanyiwa marekebisho mwaka 2008,  hasa katika misale ya waumini, wataongeza kipengele kipya cha Baba yetu. Ni kwa mujibu wa maelezo ya katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Italia, Askofu Mkuu Nunzio Galantino wakati wa hitimisho la Mkutano Mkuu wa kudumu wa Baraza la Masskofu wa Italia. Mkutano Mkuu wa Cei uliioanza mapema mwezi huu kuanzia tarehe 22 Januari na ambao umekijita katika mada nyingi za Kanisa na jamii kwa ujumla, lakini pamoja na  mada nyingine kuhusu mchakato na makubaliano ya kutoa toleo jipya la tatu la Misale ya waumini, ili  kuweka tafsiri mpya kwa lugha ya kiitalia kuhusu sala ya “Baba yetu”.

Uamuzi huo umefikia mara baada ya ufafanuzi wa ufasaha wa Baba Mtakatifu Francisko wakati wa kutafakari ya Baba yetu kwa kina. Ni katika tukio la kipindi cha televisheni ya Baraza la Masskofu wa Italia (TV2000), kipindi ambacho kiliendeshwa na Padre Marco Pozza, Msimamizi wa Kanisa dogo la wafungwa huko Padua nchini Italia, akiwa na Baba Mtakatifu Francisko kwa vipindi 9 vilivyooneshwa kila siku ya Jumatano usiku.

Kipindi hicho kilikuwa ni “Baba yetu” iliyofundishwa na Yesu mwenyewe, na hivyo Baba Mtakatifu Francisko wakati wa maelezo ya tafakari yake katika kipingele cha kichawishi, alikuwa amefafanua kwamba,“si Mungu anayetutia katika kishawishi, bali ni shetani”. Ufafanuzi huo pia ulikuwa tayari umeshaonekana katika Baraza la Maaskofu wa Ufaransa na Hispania. Kwa mfano, Baba Mtakatifu Francisko alisema: “wafaransa wameisha badili tafsiri hiyo na kuweka “usianiache nianguke katika kishawishi”, na hiyo ni kwasababu anaongeza, “ni mimi mwenyewe ninayeanguka, wala si Yeye, Mungu Baba anayeniangusha katika kishawishi na baadaye aone jinsi gani ninaanguka; baba yoyote yule hawezi kufanya jambo hilo, badala yake baba anamsaidia mtoto wake kuamka haraka”. 

Hata hivyo Askofu Mkuu Galantino anasema kuwa, tangu mwaka 2008, tafsiri ya “usiniache nianguke katika kishawishi ilikuwa tayari katika Biblia ya 2008 ya Baraza la maaskofu wa Italia japokuwa haikuwa imeweka katika misale ya kiliturujia na kuitilia mkazo, lakini kwa sasa itaanza kutumika rasmi mara tu itakapokuwa tayari imerekebishwa katika toleo la tatu la misale ya waumini.

Sr Angela Rwezaula

Vatican News!

 








All the contents on this site are copyrighted ©.