2018-01-26 09:40:00

Ujumbe wa Papa Francisko kwa Tukio la Uzinduzi wa Kitengo kipya


Asubuhi ya tarehe 25 Januari 2018 katika Taasisi ya Kipapa ya Taalimungu ya ndoa na Familia ya Yohane Paulo II, imezinduliwa Fani mpya ya Gaudium et Spes. Katika tukio hilo, Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe wake kwa Askofu Vincenzo Paglia ambaye tangu tarehe 15 Agosti 2016, ametuliwa kuwa Mwenyikiti wa Chuo cha Kipapa cha Taaluma ya Maisha na Kansela Mkuu wa Taasisi ya Kipapa ya Yohane Paulo wa II, inayojikita katika mafunzo ya Taalimungu na Sayansi ya Ndoa na Familia. Lakini, licha ya shughuli hizo pia ni msimamizi wa kiroho wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio na Mwenyekiti wa Shirikisho la Biblia nchini Italia.

Katika ujumbe wa Baba Mtakatifu anawapa salama washiriki wote  katika uzinduzi wa Fani ya Gaudium et Spes  Hati ya  kichungaji inayohusu Kanisa katika ulimwengu.  Baba Mtakatifu anasema,tarehe iliyochaguliwa kufanya tukio hilo katika taasisi hiyo inawarudisha katika kumbukumbu ya tarehe 25 Januari 1959, mahali ambapo Mtakatifu Yohane  XXIII alishangaza Kanisa na ulimwengu mzima kwa kuhitisha tukio kubwa la Kanisa Karne ya XX ambalo lilikuwa ni mtaguso wa II wa Vatican. Kwa hakika wakati wa hitimisho la kazi ya Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican, mababa walikubali kuwa na  Hati ya kichungaji “Gaudium et spes” yaani “Kanisa katika ulimwengu. Huo ulikuwa na uwezo wa kujieleza  na kutoa muundo kwa malengo ya kina ambayo yangeongoza  na kuelekeza shughuli za Mtaguso, kwa maana hiyo ulikuwa ni mkutano halisi.

Ulikuwa ni mkutano wa kweli kati ya Kanisa na watu wa nyakati zetu. Mkutano ambao ulitokana na nguvu ya Roho anayesukuma Kanisa lake kutoka katika unyaukaji kwa miaka mingi, kwa kujifungua yenyewe na ili kuanza mwamko  mpya na kujikita kwa shauku kubwa ya safari ya kimisionari. Mkutano huo ulikuwa ni hatu ya mchakato wa kukutana na kila binadamu, mahali ambapo anaishi kama vile katika mji, nyumbani, mahali pa kazi, kwa maana hiyo kukutana na mtu halisi. Kanisa  linaalikwa kumfikishia kila mmoja furaha ya Injili na kupeleka huruma na msamaha wa Mungu .Ni msukumo wa kimisionari baada ya mamia ya miaka na ili kuanza upya kwa nguvu zote na  shauku zilezile. ( Mahubiri Papa Francisko ufunguzi wa Jubilei ya Huruma 8 dicembre 2015).

Baba Mtakatifu anaonesha furaha yake kuwa Taasisi hiyo ya Taalimungu ya Yohane Paulo II kuchukua wajibu kwa namna ya pekee katika kujikita kuendeleza uhai na lengo la kutazama kwa upya hati ya Mtaguso katika mafunzo ya kina kutafakari ili hati hiyo iweze kuendelea kuwa na matunda na thamani ya kurithisha. Siyo rahisi kusahau jinsi gani Hati ya Gaudium et Spes imependwa na mwanzilishi wa Taasisi hiyo, Mtakatifu Yohane Paulo II nasema Baba Mtakatifu Francisko na kuongeza kuwa : Yeye alikuwa ni mmoja wa watu walio mstari mbele kuendeleza na kwa maana  utume wake kama kharifa wa mtume Petro ulijikita  mizizi yake katika Hati hiyo.

Baba Mtakatifu Francisko anakumbusha maneno yake Mtakatifu Yohane Paulo II anaposema kuwa: ninataka kuugama  kuwa Gaudium et Spes , kwa namna ya pekee ni msada na wema kwangu, si kwa ajili ya mantiki za kuweza kuendelea, bali kwa ajili ya ushiriki wake wa moja kwa moja ambao nimepewa kufanyia kazi”. Hiyo ni kwasababu anaongeza Baba Mtakatifu Francisko kuwa, Akiwa kijana kotoka Poland alikuwa mjumbe wa Kamati ya kusoma na kuchunguza ishara za nyakati katika Mtaguso, na kuanzia Novemba 1964 aliitwa kuwa sehemu katika kitengo cha  kamati msingi, na kupewa shughuli ya kuhakiki maandiko ya Hati ya Gaudium et Spes. Anaendelea kueleza kuwa, ”kwa kina utambuzi wa mwanzo wa Gaudium et Spes umeniwezesha kutoa sifa kwa kina na thamani ya kinabii na kuichukulia kwa mapana mafundisho yake katika utume wangu hadi kufikia kuandika  waraka wangu wa kwanza wa Redemptor hominis”. Ndani yake yanakusanya urithi wa Hati ya Mtaguso, ambayo inataka kusitisiza kuwa, asili na mwisho wa binadamu na ulimwengu hauwezi kuonekana iwapo si kwa njia ya mwanga wa Kristo msulibiwa na mfufuka.» (taz. kumbukumbu ya Cost. Gaudium et spes, 8 Movemba 1995: Mafundisho, XVIII, 2 [1995], p. 1053).

Fani mpya, iliyoanzishwa leo, inafaa vizuri ndani ya upeo wa utume wao wa kutaaluma kwa ndoa na familia” Baba Mtakatifu anathibitisha na  kusema kuwa anatambua  kuwa misingi hiyo ni hali halisi ya maisha ya binadamu iliyowekwa na Mababa wa mtaguso katika nafasi ya kwanza kati ya matatizo ya leo kwa namna ya pekee  ndiyo yenye dharura (GS, 46). Kwa njia hiyo tunaweza kusema kuwa anasisitiza, katika Gaudium et Spes, Kanisa lilitambua kueleza  uelewa wa kina wa mageuzi ya Injili katika familia kwa hatua mbalimbali , ambazo zimetufikisha kipindi cha Sinodi na kutoa Waraka wa kitume wa Amoris laetitia, ambao ni ” Furaha ya Upendo ndani ya Familia”.

Ni matumaini ya Baba Mtakatifu kuwa Fani hiyo inaweza kutoa mchango mkubwa, ili kwamba taasaufi hiyoiweze kuwa mstari wa mbele dhidi  ya changamoto moja za kichungaji ambazo jumuiya ya kikristo zinaalikwa kutoa jibu. Mafundisho ya maadili na kijamii leo hii yanachukua mshikamano wa binadamu wote katika mipango wa ufunguzi wa upeo mpya kwa ajili ya binadamu kuishi pamoja na ugumu wake , ambapo uonesha  uasili wa wito wake ambao unabainsiha na Mungu kwa ajili ya kazi nzima ya uumbaji. Juhudi za tafakari na mafunzo yanayojikita katika mafunzo ya taalumya hio yanawakilisha ushidi na ahahdi kwa ajili ya taasisi ambayo inaweza kuenza mafao ya Kanisa zina na hata jamii ya raia. Ni kwa namna ya pekee  leo kuna haja ya kuunda maeneo ya makufano na mazungumzo hata ya taaluma ya hali ya juu ambapo inawezakana kufanya uzoefu wa jumuiya ya Kanisa mtazamo wake kwa watu wa nyakati zake.Kama Mababa wasemavyo katika hati ya mtaguso “ furaha na matumaini, hzuzni na uchungu wa watu wa leo  masni na hasa zaidi wale ambao wanteseka, ni sawa na furha na matumaini, husuni na uchungu wa mitume wa Kristo, …(Gs) 

Katika siku ambayo Mama Kanisa anaadhimisha sikukuu ya uongofu wa Mtume Paulo , ambapo Bwana Yesu alimkabidhi kwa namna ya pekee utume wa kutangaza wokovu wa ukristo  katika mataifa , Baba Mtakatifu anawataki matashi mema ya kuanzisha fani mpya ili daima iweze kuonekana “ uzuri wa upendo wa wokovu wa Mungu ulioneshwa ndani ya Yesu Kristo aliyekufa na kufufuka (Taz EG, 36). Anahitimisha akiwashukuru wote waliojikita kuandaa kazi hiyo kwa njia nyingi wanaendelea kusaidia, na kwa wote, Bwana awabariki na Mama Maria awalinde.

Sr.Angela Rwezaula
Vatican News!

 








All the contents on this site are copyrighted ©.