2018-01-22 15:01:00

Mungu anatoa zawadi nyingi za karama zinazoonekana ndani ya Kanisa!


Zawadi ambazo Mungu ametoa katika Vyama vya Kitume na jumuiya za Kanisa  zinaonekana jinsi zilivyo kutokana na kutambuliwa na Kanisa, katika Kanisa na kwa ajili ya Kanisa na kusambaza manukato yao mazuri  kwa njia ya huduma yao. Ni maneno kutoka katika hotuba ya Maria Voce, Mwenyekiti wa Chama cha Kitume Cha Wafokolari wakati wa Mkutano kuhusu mada ya “Karama na mwenendo wa Taasisi  na jumuya za Kitume  za Kanisa”. Ni mkutano ulioandaliwa na Taasisi ya Chuo Kikuu cha Sofia mjini Roma kwa ushirikiano na  Chama cha Kanuni ya Sheria Katoliki Italia (Ascai) hivi karibuni.

Katika hotuba yake anasisitiza kuwa, moja ya shauku kubwa uliyopo katika taasisi mbalimbali na vyama vya kitume ni ile ya kujibu wito wa Mungu, ambao amewaitiwa yaani kuwa wapo katika huduma ya Kanisa na upendo na shauku;kuwa na upeo ulio mpana katika matarajio yake na mahitaji yake hasa katika nyakati hizi ya mageuzi ya Kanisa linalotaka kutoka nje kwa matashi na wito wa Baba Mtakatifu Francisko.

Katika hotuba yake, Mwenyekiti wa Wafokolari anasisitiza tena  wajibu pia ambao unajikita kila siku katika kila aina ya karama yaani ya kuwa mchango nyeti wa umoja wa Kanisa ili kuweza kuponyesha majeraha yatokanayo na kasumba za sasa za utandawazi,ambao hawali ya yote unataka kuwa kiini cha ufujaji na utumiaji hovyo tu kwa kumsahau Mungu.  Hivyo anakumbusha kuwa, wajibu wa karama zote licha ya utandawazi na hali ya sasa ya maisha ni kuendeleza kujenga madaraja ya kindugu kwa wote na kwa ngazi zote. 

Akimalizia hotuba yake kuhusu umoja wa Kanisa, anatumia maneno ya Baba Mtakatifu Francisko katika moja ya hotuba zake kuhusiana na umoja ya kwamba, “Tunatambua ya kuwa umoja wa kweli hauwezi kuwapo katika vyama vya kitume au ndani ya jumuiya, iwapo hakuna ushirikishwaji wa umoja ulio mkubwa utokao kwa wa Mama yetu Mtakatifu ambaye ni Kanisa”, na kwa njia hiyo Maria Voce anaongeza kusema, hiyo ndiyo shauku kubwa waliyo nayo ambayo inawezekana kupata muungano kamili na ambao unaonekana!

Sr Angela Rwezaula
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.