2018-01-19 09:24:00

Kard.Filoni ameadhimisha Misa ya Sikukuu ya mwenyeheri Pd.Paulo Manna!


Shukrani kwa  Baraza la Kipapa kwa ajili ya utume wa kimisionari katika shughuli za uinjilishaji barani Asia na mahali pengine mwaliko kwa wote kushirikiana kusadia utume wa uinjilishaji wa watu (ad gentes ) kwa wale wasio kuwa wakristo ambao wakati mwingine wako hatari ya kusahuliwa kwa kuwekwa  kwa kile kiitwacho kwa ujumla “yote ni utume”. Umisionari bila kutangaza Neno la Mungu unapunguza thamani na wajibu wa Kanisa, matokeo yake  kuishia kugeuka  kama Shirika lolote  lisilo la kiserikali (NGO); kuna haja ya  uamsho wa utume wa uinjilishiji wa watu  (Ad gentes) katika  mwezi maalum  wa kimisionari kwa mwaka 2019! Ni baadhi ya mada alizozitaja Kardinali Fernando Filoni, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu tarehe 16 Januari 2018 wakati wa maadhimisho ya Misa Takatifu kwa wamisionari wa Pime na Watawa wamisionari wa Shirika la Mkingwa dhambi ya asili mjini Roma. 

Habari zilizoandikwa na AsiaNews linasema kuwa, fursa ya misa hiyo  imetokana na kufanya  kumbukumbu ya sikukuu ya Mwenye heri Paulo Manna (1872-1952), mmisionari wa Pime aliyetangazwa kuwa mwenye heri na Mtakatifu Yohane Paulo II , ambaye pia  ni mwanzilishi  na Mwenyekiti wa Kitengo cha Baraza la Kipapa la Umoja wa wamisionari. Moja ya Baraza la kitume chini ya Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu, hicho ni kitengo kinachojihusisha na uhamasishaji wa kitume kati ya mapadre, watawa wote na walei katoliki.

Katika mahubiri ya Kardinali Filoni anamtaja mwenye heri Paulo Manna kwamba, alikuwa mmisionari wa watu kama vile Mtakatifu Paulo; asiyechoka katika kutangaza Neno la Mungu, kuhimiza daima kwa kipindi mwafaka na kisicho mwafaka, kushauri na  kukemea (2Tim 4,2), lakini pia kutunza imani yake (2 Tim 4,7). Amebainisha pia kwamba, utume wa kimisionari unazingatia hawali ya yote kutangaza Neno la Mungu kwa dhati, kwani bila kutangaza Neno, kila aina ya kazi ya kimisionari inaweza kugeuka kuwa kama aina ya chama chochote kisicho cha kiserikali (NGO).

Mwenye heri Manna anajulikama pia  kuwa na roho ya moto, alikuwa mmoja kati ya wafuasi wa mchakato wazi kwa miaka kadhaa wa  Mtaguso wa II wa Vatican. Yeye alitoa msukumo wa Kanisa kutambua kuwa, wote tunalazimika kuwa na shauku ya utume na kujikita barabara katika matendo ya kweli ya uinjilishaji.  Alikuwa akipinga  vikali kila aina yoyote ya utume unaosimamia  kujionesha au majivuno katika matendo mengi ya huruma na kijamii. Alifanya kazi bila kuchoka ili wakristo watambue nini maana ya utume; wasishindane wao kwa wao bali waoneshe umoja kati yao, kuwa ndiyo kiini msingi na ushuhuda wa imani katika utume wa uinjilishaji mahali popote.

Wakati wa mazungumzo yake na wamisionari wote, hawali ya yote amewaeleza kuwa, utume wa uinjilishaji wa watu kwa sasa unabadilika. Wasio wakristo kwa njia ya kuhahama, wamejikuta wanaingia katika nchi ambazo ni zenye mzizi wa kizamani wa dini; wengine wamejikuta katika nchi za kimisionari, hivyo jumuiya zenye mizizi ya kizamani ya dini, zimewapokea wote, na zinahisi kweli kufanya umisionari kwa njia ya matendo mema. Lakini pamoja na hali hiyo, Kardinali Filoni amebainisha kuwa,  wakati mwingine shughuli za uinjilishaji wa watu, hasa katika kutangaza Neno kwa watu wasio kuwa  wakristo, inasahaulika au kuachwa pembezoni, hali hiyo ipo katika makanisa za kizamani ya uinjilishi, hata makanisa mapya ya uinjiishaji. 

Na kwa njia hiyo anasisitiza kwamba kuna umuhimu, na dharura ya kuweza kutunza uhai wa karama ya taasisi za kimisionari za ujinjilishaji, bila kufurahishwa na maelezo kama vile “utume kichugaji wa kijimbo au matendo ya huruma na uinjilishaji mpya”, badala yake, Neno na matendo viambatane. Kutokana na misingi hiyo, Kardinali Filoni amekumbusha kuwa, mwezi maalumu wa Kimisionari mwaka 2019 utaweza kusaidia kuamsha kidogo Kanisa juu ya  dharura ya utume wa uinjilishji wa watu!

Sr Angela Rwezaula
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.