2018-01-18 09:21:00

Bado ni hai kauli ya Martin L.King katika utetezi wa usawa na ubaguzi Marekani!


Kila jumatatu ya tatu ya mwezi wa Januari kwa kila mwaka,ni Siku ya Kukumbukumbu ya Martin Luther King, mtetezi wa haki za raia na usawa wa watu nchini Marekani. Kwa mwaka huu tarehe hiyo imeadhimishwa tarehe 15 Januari 2018. Kutokana na siku hiyo hata Baraza la Maaskofu wa Marekani wameikumbuka siku hiyo kwa namna ya pekee na hai kabisa kutokana na matukio mbalimbali ambayo yanazidi kujionesha katika taifa huru na linalojulikana na mataifa yote.

Ili kuweza kuponyesha majeraha katika jamii inayojigundua kuwa bado kuna ubaguzi wa rangi, maaskofu wa wanahamasisha uwepo wa  sheria njema inayojali  wahamiaji na kubadili mtindo wa mawazo potofu  juu ya hadhi ya binadamu. Kwa upande wa Maaskofu wa Marekani, bado wanaonesha msimamo wao mkali hasa wakilenga kwa rais wa nchi na wawakilishi wa Bunge, lakini hata kwa wananchi wote wenye mapenzi mema ya kuamini usawa na hadhi ya binadamu katika dunia hii. Ni ujumbe unaojikita ndani ya jamii ya Marekani, kutokana na kwamba daima nchi inaendelea kuona cheche za moto wa ubaguzi wa rangi ambao kumbe haujawahi kuzimika kamwe. Ni maneno yanayotaka kuwahamasisha mahusiano hasa ya kuelimisha juu ya mapokezi kwa wale wanaobisha milango katika nchi yenye utajiri mkubwa duniani ili  nao waweze kujikimu hali zao za  maisha na kupata mshikamano wote walio wadhaifu.

Kwa mantiki hiyo bado ujumbe wao unazingatia matukio yote yaliyotokea hivi karibuni, kuanzia mazungumzo juu ya sheria ya wahamiaji ambayo wanataka kusitisha kinga ya muda, kufikia hali halisi  ambayo inatazama sheria ya Daca. Maaskofu wa marekani wanaonesha wasiwasi mkubwa wakiomba masuala hayo yatafutiwe suluhisho la haraka.  Kwa mfano kuhusu vijana, wamasema, hawa wanaishi na kutajirisha nchi ya Marekani kwa namna nyingi, wakichangia uchumi wa nchi, ni wanajeshi, wana matokeo mazuri katika taaluma za vyuo vikuuu , parokia, na jumuiya zao. Vijana na familia zao,wanastahili kupata uhakika wa maisha, upendo wa Kanisa, ukarimu na haki zao. Haya ni maneno ya Askofu Joe S. Vásquez wa Jimbo la Austin huko Texas na Mwenyekiti wa Tume ya Baraza la Maaskofu wa Marekani kwa ajili ya wahamiaji akibainisha juu ya kuanzisha mambo mapya yaliyozuka katika nchi na ambayo yanaweza kugawanya familia.

Kutokana na hilo, Askofu Joe anasema, ni lazima uwepo ulinzi na  usalama  wa nchi.  Mafundisho ya maadili kijamii yanatambua na kuheshimu haki za mataifa yanayolinda hata  mipaka yake. Lakini ulinzi huo  lazima pia  usaidiwe kifedha bila kusababisha hasara au matatizo ya waathirika. Kama nchi , lazima kufuata maadili ya kibinadamu mbele ya wote wanaoota maisha ya baada ye na ambao maisha yao yako hatarini.

Hata katika siku ya kukumbuka Martin King, Katika Jimbo la Galverston-Houston huko Texas, Rais wa Baraza la Maaskofu wa Marekani Askofu Mkuu Daniel Di Nardo ametoa tafakari lake kuenzi siku  Kumbukumbu ambayo ni sikukuu ya Taifa kila ifikapo Jumatatu ya tatu ya kila mwezi wa  Januari ambapo mwaka huu ilikuwa ni tarehe 15 . Katika ujumbe wake anasema, miaka ya mwisho kwa mfano wakati wa kiangazi mwaka jana huko Charlottesville huko Virginia, wamejionea ukweli uliojificha kijuujuu katika utamaduni wa Marekani, pamoja na uwepo wa maendeleo ya hali ya juu katika nchi hiyo, suala la ubaguzi wa rangi bado linabaki kuwa hali halisia halisi ya changamoto hai. Kumbukumbu ya Siku ya Martin King Jr, inatoa fursa tena kwa mwaka huu kuanza kwa upya, hasa kujikita katika kutafakari thamani ya Kiinjili ambayo akiwa kiongozi alikuwa akitangaza, na ili kwa namna ya pekee dhambi kubwa ya ubaguzi wa rangi iweze kutokomezwa kabisa kwa upndo wa dhati na mwanga wa Imani.

Siku ya kumbukumbu ya Martin Luthe King Jr, iliwekwa  kila jumamatu ya tatu ya mwezi wa kwanza tangu mwaka 1986 na Rais Reagan wa wakati ule, kwa lengo la kutoa heshima ya kumbukumbu ya shujaa wa kupinga vurugu ambapo tarehe 4 Aprili mwaka huu itakuwa ni kumbumumu ya miaka 50 tangu alipouwawa huko Memphis. Lakini hadi kufikia mwaka 1993 kwa matashi ya  Rais Bill Clinton  ikaweza kuadhimishwa katika nchi 50 za Amerika.
Askofu Mkuu Di Nardo amechagua maandiko yake ya Martin King ya  mnamo mwaka 1958 , mahali ambapo anaandika kuwa : “katika njia ndefu ya maisha, kila mmoja lazima awe na nia njema  na  maadili mema ya kuweza kuvunja kabisa mnyororo wa chuki, lakini inawezakana tu kwa njia ya kuweka upendo kuwa kitovu cha maisha yetu”. 

Kwa mujibu wa maneno hayo, Kardinali Daniel N. Di Nardo, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Marekani anasema, mbiu hiyo ni wito mkuu wa kupokea changamoto za mchungaji King kwa wakati huu ambapo ni hai kabisa.  Mwenyekiti wa Baraza la Maskofu wa Marekani anamalizia kwamba, kuvunja mnyororo wa chuki unahitaji ujasiri ambao unatokana na jitihada kama vile za ushuhud wa Sista Mary Antona Ebo,mwanashirika wa Wafranskani wa Maria, ambaye alikuwa ni dada wa kwanza mweusi kufanya  maandamano na King tarehe 10 Machi 1965 huko Selma Alabama. 

Sista Ebo amekufana tarehe 11 Novemba 2017 akiwa na umri wa miaka 93. Lakini ni mtawa jasiri kwa uhodari wake wa utetezi wa haki za rai, shughuli aliyoifanya  maisha yote, na ushuhuda wake anongeza kusema , unapaswa kuigwa mfano katika maisha yetu wote. Amekumbuka maneno ya mtawa huyo siku ya maandamano, kwa wale wote waliokuwa wanauliza sababu ya kuwapo katika maandamano hayo kwamba aliwajibu, “ niko hapa kwa maana mimi ni  mweusi lakini pia mimi ni mtawa mkatoliki na zaidi ninataka kushuhudia” .

Hata hivyo  mfano wa Martin King  pia ulikuwa amezungumziwa mwaka jana,  mwana shirika wa Kijesuit George Murry, Askofu wa Youngstown na mwenyekiti wa Tume ya kupinga ubaguzi wa Rangi , tume iliyounda ndani ya Baraza la Maaskofu Marekani. Katika mkutano na waandishi wa habari tarehe 2 Oktoba 2017 mara baada ya matukio mabaya ya  huko Las Vegas, alisema, kuna vurugu nyingi katika jamii yao na kile kinacho zungumzwa hakitiliwi maanani wakati huohuo matukio yanajirudia. Kama jamii hawaachi tabia ya sintofahamu, kwa kujikita katika vyama vyama vya kupinga vurugu wote, jamii itaendelea kuwa na matukio kama hayo, na hivyo upo ulazima zaidi wa jambo muhimu hasa ule wa kufanya uongofu wa kweli. Upo ulazima wa kuwa na jamii ya kuishi na  watu wanao elewana na kuwa na kikundi cha watu wanaosikiliza muziki wa aina moja.

Iwapo jumuiya haiwezi kutambua kuwa pamoja,yaani utambuzi wa kuishi kama familia moja,ni wazi kuwa na hofu ya kutoweza kusimamisha vurugu hizo ambazo zinaendelea kuonekana. Pia alikumbuka maneo ya Baba Mtakatifu katika Ujumbe wa Laudato si kwamba,  Papa aliongea juu ya ardhi nyumba yetu ya pamoja na ni kweli; Lakini kama ndiyo hivyo hata jamii ni nyumba na  mahali ambapo kuna haja ya kulindwa na kuheshimiana hata kuwa na  upendo.  Akini katika njia ya vurugu  ni rahisi kutambua hadhi ya binadamu? 

Jibu: kuna zipo ishara za ndiyo japokuwa hazitoshi. Wito wa kutotumia nguvu mbele ya matukio yasiyo ya haki ndiyo ilikuwa kiini cha upendo wa kazi yote ya mchungaji Martin Luther King.  Kauli yake ya kutotumia nguvu ni msimamo wa kishujaa mbele ya dhambi kubwa ya ubaguzi wa ranngi  ambayo imeleta utofauti katika mataifa hasa huko Marekani. Matukio ya hivi karibuni yanaonesha bayana haja zaidi ya kurudia kutazama kwa upya upeo wa mchungaji Martin Luthe King. Na hivyo bado kuna safari ndefu ya kutambua lakini  isiyo rahizi ambayo  inahitaji juhudi , uvumilivu na matumaini.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.