2018-01-04 14:57:00

Kardinali Bassetti anasema vijana wasaidiwe katika miito yao ya maisha!


Kwa vijana inahitajika kuwasha cheche za matumaini ya kujitoa na si kujifunga binafsi. Kujitwisha mzigo kwa upendo  na kuwasaidia wengine, lakini wa bahati mbaya kadiri siku zinavyokwenda mbele, upo utambuzi ya kwamba, wapo vijana ambao ni kama sehemu za pembezoni, wenye kuhitaji msaada wa maisha. Hayo ni mawazo ya Kardinali Gualtiero Bassetti , Askofu Mkuu wa Perugia nchini Italia na Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Italia wakati wa tafakari ya masifu ya jioni katika siku ya kwanza ya Mkutano wa Kitaifa kuhusu miito ambao unafanyika mjini Roma siku hizi hadi tarehe 5 Januari 2018.

Katika tafakari ya masifu hayo, baada ya somo la Injili kutoka Mtakatifu Yohane akielezea juu ya Ubatizo wa Bwana,Kardinali Bassetti amesema kuwa alishangazwa na maneno ya Baba Mtakatifu Francisko katika Mkutano wa Kimataifa juu ya miito, ulioandaliwa kwa ajili ya watawa. Kardinali Bassetti amesema,  katika hotuba yake alisema,“wapo vijana wengi pamoja na kwamba ni kizazi cha utamaduni wa Selfie, ambao wanatafuta maana ya kweli ya maisha yao, hata kama wengine wanatafuta mahali ambapo hawawezi kuipata. Wito unapaswa kuwa na mapendekezo tofauti ambayo yanawawezesha kupata majibu ya kila mmoja”.  Na kwa maana hiyo Kardinali Bassetti anaongeza kusema: maneno ya hayo ni kama kaulimbiu, lakini ambayo kwa hakika ni yenye msingi na kutafakari kwa kina.

Baba Mtakatifu Francisko anapendelea  maneno kama vile: kusindikiza na kutembea na mwingine. Na kwa njia hiyo anawaalika wote kuamsha shauku kwa vijana na kuwafanya wahisi kweli  wanapendwa upendo upeo. Ili kufanya hivyo yapo mapendekezo  muhimu ambayo ni ubunifu wa kweli unaotakiwa  kutafakari kwa kina.Hata hivyo shughuli ya kichungaji  hawali ya yote inapaswa kuelekeza katika mantiki hiyo ya miito, kama ilivyokuwa tayari imeelezwa mwaka 1969. Kardinali Bassetti amethibitisha kuwa, katika kipindi hicho  ilikuwa ni ubunifu, japokuwa leo hii tayari inajieleza wazi na kwa kina zaidi, kwa maana shughuli za kichungaji  ki ukweli ni uchungaji wa kikristo.

Mafundisho au elimu ya miito Kardinali Bassetti anabainisha kuwa,  inaweza kabisa kujieleza kutokana na tabia ya ukaribu. Hiyo imawezekana iwapo tangu utoto wao,wanasindikizwa, wanaelekezwa ili watambua zaidi ulazima wa kuwa tayari, kujitoa sadaka kwa kila kitu, kama vile  kwa ndugu na wao binafsi. Maana ndiyo mafundisho na lengo la kikristo.Yesu mwenyewe alionesha kwa matendo ya kujitoa sadaka kwa ajili yetu. Ndiyo maana ya kusema,sehemu za pembezoni ambazo ni vijana zinaonekana kuwa na mipaka. Kwa maana hiyo vijana ni kama mishale na upinde wa Mungu. Kila tunachofanya lazima kilenge nia maalumu hasa ya kuelekeza mbele, kama upinde na Mshale kuvielekeza kwa Mungu!  amethibitisha.

Sr Angela Rwezaula

Vatican News!

 








All the contents on this site are copyrighted ©.